Uwepo wa Rev. Fr. Charles Kitima kwenye utiwaji saini wa Mkataba wa DP World unahitaji majibu

US ni Super Power kuna maeneo ili kulinda hadhi yake lazima atumie mlango wa nyuma kuyaingia, ni kama alivyo na makampuni kule China.
Kuwa super power ni sawa mkuu, ila waarabu hawana njaa ya kushindwa kuwa na kampuni kama DP world.
 
wamebadilisha vipengele, kwanini wasiende?
MABORESHO YA MKATABA
Wamebadilisha vipengere vyote tata…

1. Mkataba maximum miaka 30

2. Watalipa kodi zote za Serikali kwa mujibu wa Sheria

3. Wamewekewa performance key indicators na watakuwa accessed kila baada ya miaka 5

4. Serikali itachukua 60% ya mapato ya faida

5. Serikali inauwezo wa kuvunja mkataba muda wowote

6. Mkataba huu sio wa gati zote za Bandari ya Dar es Salaam gati ambazo hazipo kwenye mkataba huu zinatafutiwa Mwekezaji mwingine (hata huyu wa sasa)

7. Mkataba huu hauhusishi Bandari yoyote mwambao Bahari ya Hindi wala maziwa makuu.
Kwani tangu mwanzo mlipokuwa mnaekezwa kwamba hayo yote mnayolalamikia huoneshwa kwenye HGA na siyo IGA,mlikuwa mnabisha nini?.
IGA hipo vilevile ilivyokuwa, kwa maana ilisainiwa muda mrefu kabla ya kuingizwa kwenye kukubaliwa Bungeni.
 
Tumsifu Yesu Kristu.

Leo tarehe 22.10.2023 umehudhuria kikao cha utiaji saini HGA kwa ajili ya uendeshwaji na uendelezwaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa wewe ndo uliyekuwa kinara wa kupinga uwekezaji wa DP World hapa Nchini, na leo umehudhuria kikao cha utiaji saini jambo lile lile ulilolipinga kwa nguvu zote, Waamini wa Kanisa Katoliki Tanzania tunaomba utoe ufafanuzi wa kina tena bila kupepesa macho kuhusu suala hili. Kama ufafanuzi wa kina hautatolewa haraka:-

(1) Binafsi sitatoa sadaka wala mchango wowote ule Kanisani, kwani sitakuwa tena na Imani na Kasisi yeyote yule. Lakini pia nitawashawishi na Waamini wengine kuchukua hatua nilizochukua.

(2) Nitajiuzuru nyadhifa zangu zote katika Kanisa na kuwashawishi wengine kufanya hivyo.

Tunaomba bila kupoteza muda mwingi jitokezeni kutoa maelezo ya kina.
Tuna watu kama hawa kwa kweli ni shida kubwa hapa nchini.! Nenda ww basi BANDARI ukatoe hizo meli zinazokaa hapo siku kumi

Nyambafu.
 
Tumsifu Yesu Kristu.

Leo tarehe 22.10.2023 umehudhuria kikao cha utiaji saini HGA kwa ajili ya uendeshwaji na uendelezwaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa wewe ndo uliyekuwa kinara wa kupinga uwekezaji wa DP World hapa Nchini, na leo umehudhuria kikao cha utiaji saini jambo lile lile ulilolipinga kwa nguvu zote, Waamini wa Kanisa Katoliki Tanzania tunaomba utoe ufafanuzi wa kina tena bila kupepesa macho kuhusu suala hili. Kama ufafanuzi wa kina hautatolewa haraka:-

(1) Binafsi sitatoa sadaka wala mchango wowote ule Kanisani, kwani sitakuwa tena na Imani na Kasisi yeyote yule. Lakini pia nitawashawishi na Waamini wengine kuchukua hatua nilizochukua.

(2) Nitajiuzuru nyadhifa zangu zote katika Kanisa na kuwashawishi wengine kufanya hivyo.

Tunaomba bila kupoteza muda mwingi jitokezeni kutoa maelezo ya kina.
Watu wengine Bwana! SEMA mimi na si sisi.watu walikuwa hawapingi uwekezaji,waliplnga ulle mkataba,Sasa kama ulimsikiliza vizuri Mh.Rais walipokea maoni mbalimbali na wakauboresha ule mkataba,sio wa milele Tena ni WA miaka 30 nakupitiwa Kila baada 5yrs,na mengine mazuri Inamaana Bado wewe hukubaliani?
 
Kuwa super power ni sawa mkuu, ila waarabu hawana njaa ya kushindwa kuwa na kampuni kama DP world.
Nakuambia ingekuwa Huo uwekezaji wa bandari yetu ni Waarabu pekee ungeona makelele ya huko duniani na isingewezekana, kumbuka Zanziba nini kilitokea baada ya kuona Zanziba itachukuliwa na Waarabu Nyerere aliambiwa aichukue iwesehemu ya Tanganyika.
Pia kumbuka US hili endeo lote la Afrika mashariki lipo chini yake kama sehemu ya kulinda usalama nk. Sasa hawezi kuwa mjinga kuachia eneo kama Bandari liangukie kwa Waarabu wakati anajua yaliyomkuta kipindi kile balozi zake zilivyo shambuliwa.
 
Unatishia hutatoa sadaka! Sadaka ni kwa ajili Muumba sio Reverend.
Pia kaona ushauri aliotoa umefanyiwa kazi ndio maana kaamua kufungua ukurasa mpya.
Kama ushauri walioutoa TEC umezingatiwa, mimi sina shaka hata kidogo, lakini sasa watuambie kwamba, ushauri wetu umezingatiwa ndo maana tumeshiriki kwenye utiaji saini. Ni hilo tu, wala hakuna shida nyingine.
 
Tumsifu Yesu Kristu.

Leo tarehe 22.10.2023 umehudhuria kikao cha utiaji saini HGA kwa ajili ya uendeshwaji na uendelezwaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa wewe ndo uliyekuwa kinara wa kupinga uwekezaji wa DP World hapa Nchini, na leo umehudhuria kikao cha utiaji saini jambo lile lile ulilolipinga kwa nguvu zote, Waamini wa Kanisa Katoliki Tanzania tunaomba utoe ufafanuzi wa kina tena bila kupepesa macho kuhusu suala hili. Kama ufafanuzi wa kina hautatolewa haraka:-

(1) Binafsi sitatoa sadaka wala mchango wowote ule Kanisani, kwani sitakuwa tena na Imani na Kasisi yeyote yule. Lakini pia nitawashawishi na Waamini wengine kuchukua hatua nilizochukua.

(2) Nitajiuzuru nyadhifa zangu zote katika Kanisa na kuwashawishi wengine kufanya hivyo.

Tunaomba bila kupoteza muda mwingi jitokezeni kutoa maelezo ya kina.
Ni akili finyu kumgeuza mshenga kuwa bwanaharusi, TEC ni kusanyiko hivyo ni lazima liwe na msemaji mmoja, kaa na sadaka yako ila ujue kanisa Katoliki haliishi kwa sadaka yako wewe panya unayelitisha kanisa.
 
Tumsifu Yesu Kristu.

Leo tarehe 22.10.2023 umehudhuria kikao cha utiaji saini HGA kwa ajili ya uendeshwaji na uendelezwaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa wewe ndo uliyekuwa kinara wa kupinga uwekezaji wa DP World hapa Nchini, na leo umehudhuria kikao cha utiaji saini jambo lile lile ulilolipinga kwa nguvu zote, Waamini wa Kanisa Katoliki Tanzania tunaomba utoe ufafanuzi wa kina tena bila kupepesa macho kuhusu suala hili. Kama ufafanuzi wa kina hautatolewa haraka:-

(1) Binafsi sitatoa sadaka wala mchango wowote ule Kanisani, kwani sitakuwa tena na Imani na Kasisi yeyote yule. Lakini pia nitawashawishi na Waamini wengine kuchukua hatua nilizochukua.

(2) Nitajiuzuru nyadhifa zangu zote katika Kanisa na kuwashawishi wengine kufanya hivyo.

Tunaomba bila kupoteza muda mwingi jitokezeni kutoa maelezo ya kina.
Screenshot_20231022-214337.jpg
 
Kama ushauri walioutoa TEC umezingatiwa, mimi sina shaka hata kidogo, lakini sasa watuambie kwamba, ushauri wetu umezingatiwa ndo maana tumeshiriki kwenye utiaji saini. Ni hilo tu, wala hakuna shida nyingine.
Kama ulikuwa mfuatiliaji wa hili sakata, TEC na Taasisi nyingine za dini (not sure kama Waislamu //Bakwata walikuwapo)waliitwa na their main concern was kurekebishwa mapungufu ya mkataba
Na hiyo nadhani ndio hekima ya mwenye akili yoyote duniani

Lakini ghafla ukavuma upepo ambapo tukaona Chadema na TEC wote wamebadilisha gear angani hawautaki kabisa uwekezaji ktk Bandari na sio tena marekebisho

Mara woote wamenyamaa kimya

Mara mmoja anahudhuria utiaji saini

Hii inatia shaka sana hasa kwa aina ya viongozi wa kidini tulio nao walivyo wepesi wepesi kununulika
 
Nilifikiri wote waliopaza sauti kupinga waliweka wazi kuwa hawapingi uwekezaji, bali vipengele katika mkataba. So kama kwa sasa vipengele vimemridhisha mhusika, sioni ubaya kwake kushirikiana nao. Mtazamo wangu.
Hata mimi kama vipengele vyenye utata vimerekebishwa, sina shaka hata kidogo na naunga mkono hoja.
 
Hahaha mkuu usinitafutie ugomvi na Mnafiki Wa Kujitegemea
Hapana mkuu,ni muhimu kujadili suala la maendeleo ya watu kijamii,kiuchumi na kiutamaduni pasipo kuhusisha dini.

Kuhusu uwekezaji wa Dubai Ports World kwenye bandari yetu/zetu shida si muwekezaji,bali shida ni aina ya mkataba ulivyokuwa/ulivyo.

Sijauona huo unaotajwa kufanyiwa marekebisho lkn km umefanyiwa marekebisho ni jambo jema kwani kwa ninavyosikia kwa sasa ni wazi kwamba jamaa wamepewa miaka 30,ni ktk bandari moja tu na tathimini itakuwa ikifanyika kila baada ya miaka mi 5.

Sasa km hayo marekebisho yamefanyika na ninyi hamkupenda iwe hivyo basi ni maono yenu km ambavyo sisi Watanganyika tulio wengi tulitamani iwe hivyo.

Si hivyo tu,mimi ni Msabato kwa imani lkn siwezi kukubaliana na unyanyasaji ambao wamekuwa wakifanyiwa watu wa Palestine na kwingineko duniani kwa kigezo cha imani za kidini.

Ni upumbavu wa kiwango cha juu sana mimi kuwaunga mkono Israel eti kwa sababu ya vivutio vya utalii wao huku wakitulaghai kuwa ndiko alikozaliwa,zikwa Yesu.

Si hivyo tu,hata vile vivutio vya utalii kule Maka na Madina ambako watu kwa kulazimishwa wanapeleka kokoto eti wanaambiwa kuwa ni kumrushia jiwe shetani,wanatoa fedha nyingi na kuambulia jina eti El Hadji.

Simo ndani ya upuuzi wa dini mimi,ninacho kujua mimi dini ni taasisi za kifedha zenye mifumo ya unyinyaji,hivyo huwa ninaenda ili tufahamiane na kuimarisha upendo kati yetu na jirani zetu.
 
Serikali ya CCM imeipiga TEC "chenga ya mwili " .Mbinu nzuri ya kupata uungwaji mkono ni kumtumia mkosoaji "critic "

Sasa kanisa na wasomi wake wote wameufyata mbele ya Chama, sijui wataambia nini waumini
Wakaendelee kuwasomea waraka wao makanisani
 
Mkataba ulikua changa la macho tu, katoliki wabaya wake walikua ni wale wa zamu yetu, maana hadi walishalivamia katoliki na kuanza kulibomoa kwa ndani,,, naona kwa sasa dawa yao imeshapatikana mambo yananyooka,,,, RC ni kubwa sana kwenye hii nchi hasa yanapokuja maswala ya kiusalama na maslahi yake
 
Ni IGA ipi unaizungumzia, mkuu 'Missile'. IGA ile ilikufa. Mikataba hii haina uhusiano wowote na IGA ya aina yoyote ile.

Nitakachowalaumu juu yake hawa maTEC na wengineo, ni kuwa na kichwa kama cha kuku.
Wakihadaiwa na hivi vi-Tsh100 milioni hapa na pale, na makanzu; halafu wasahau mtego unaowekwa ili uwanase tena hapo 2025; hawatakuwa na tofauti yoyote na kuku anayetupiwa punje za mchele ili awe kitoweo.
Hilo litasikitisha sana.
Kwa ufupi, Kitima anatakiwa atoe maelezo , aitishe press kufafanua nini kilijiri.
 
Tumsifu Yesu Kristu.

Leo tarehe 22.10.2023 umehudhuria kikao cha utiaji saini HGA kwa ajili ya uendeshwaji na uendelezwaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Kwa kuwa wewe ndo uliyekuwa kinara wa kupinga uwekezaji wa DP World hapa Nchini, na leo umehudhuria kikao cha utiaji saini jambo lile lile ulilolipinga kwa nguvu zote, Waamini wa Kanisa Katoliki Tanzania tunaomba utoe ufafanuzi wa kina tena bila kupepesa macho kuhusu suala hili. Kama ufafanuzi wa kina hautatolewa haraka:-

(1) Binafsi sitatoa sadaka wala mchango wowote ule Kanisani, kwani sitakuwa tena na Imani na Kasisi yeyote yule. Lakini pia nitawashawishi na Waamini wengine kuchukua hatua nilizochukua.

(2) Nitajiuzuru nyadhifa zangu zote katika Kanisa na kuwashawishi wengine kufanya hivyo.

Tunaomba bila kupoteza muda mwingi jitokezeni kutoa maelezo ya kina.
Angekuwa ana mawazo kama yako hangeenda kwenye hafla.Kwa sababu huwa wanaalikwa.Yule ni mwakilishi ukiona ameenda ujue yale yaliyokuwa yanalalamikiwa yamefanyiwa maboresho
 
Back
Top Bottom