Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
WAANDISHI MAKANJANJA NI HATARI NDANI YA NCHI.
Anaandika Robert Heriel.
Leo nitatumia lugha ngumu kidogo, nafahamu nazungumzia kazi za watu ambazo zinawaingizia kipato. Hata hivyo Nia yangu sio kuonyesha ubinafsi, kuwaonea kijicho, isipokuwa kuwataka wabadilike, ili tujenge jamii Bora na taifa bora kabisa.
Nafahamu wapo waandishi WA habari(watangazaji nikiwahusisha), ambao ni wapumbavu na ambao watajifanya kutoa povu hapa. Hawa sitawajali na wala hawatabadili lolote Katika andiko hili. Nafahaku hata wapumbavu wanahaki ya kutoa maoni Yao.
Watangazaji wengi ambao nitawajumuisha katika kundi moja la waandishi WA habari ni makanjanja, watu wa hovyo kabisa,
Taifa au jamii lolote future yake inabebwa na mambo makuu mawili, Mosi, elimu itolewayo shuleni, lapili, ni Media(vyombo vya habari), serikali makini lazima izingatie Maeneo hayo mawili Kwa mustakabali WA kizazi kinachokuja.
Yametokea mapinduzi makubwa katika sekta ya habari, uwepo wa mitandao ya kijamii, ongezeko la vyombo vya habari vya luningani na Redioni vimechochea Kasi ya kusambaa Kwa habari Kwa wepesi na Kwa watu wengi zaidi. Hii inaweza kuwa faida Kwa kizazi hiki lakini pia Kama tahadhari hazitachukuliwa inaweza kuwa hatari Kwa maadili ya jamii.
Watangazaji wengi uwezo wao wa kiakili na elimu upo chini Sana, ninayomifano dhahiri yakutosha Kwa hili nilisemalo, wapo marafiki zangu ambao elimu zao ni Tia maji Tia maji, elimu za kuunga Unga, elimu viraka.
Uwezo wao mdogo wakufikiri hawawezi kuleta Jambo lenye tija ya maana katika jamii.
Mtu yeyote atagundua kuwa Waandishi WA habari wengi siku hizi wamejikuta wakiandaa content nyepesi na zenye maudhui zaidi ya ngono, matusi, umbeya, Kick za kitoto miongoni mwa mambo mengine.
Siwalaumu Kwa kujikita huko kwani uwezo wao ndipo ulipoishia, siku zote waandishi makanjanja hujikita katika mambo mepesi Kwa kisingizio ati ni burudani.
Wao hujaribu kuieleza jamii na kizazi kijacho kuwa Umbeya ni burudani,
Watangazaji karibu wengi sasa, ni hovyo! Hovyo! Hopeless kabisa.
Wao ngono zembe kuielezea kwenye interview kwao ati ni burudani,😥😥
Unakuta liandishi la hovyo linauliza swali Kama hili; Mpaka sasa umetembea na wanaume wangapi?
Shenzi kabisa!!
Na linaloulizwa Kwa vile ni zwazwa linajibu badala ya kumchapa hata kibao kimoja huyo mwandishi Kwa kuuliza maswali ya kipuuzi.
Lengo la kuuliza maswali ya ngono zembe ni nini Kama sio kufanya Kwa kukusudia kuiharibu jamii. Swali hilo kunafanya Vijana wanaokua kuona ngono zembe ni Jambo la kawaida. Serikali nayo imezubaa zubaa haioni Hilo.
Nataka kusema, tunaowajibu WA kulinda jamii yetu Sisi wenyewe. Hatuwezi kuendelea hivi.
Niliwahi kusikia mtu mmoja akihojiwa kuwa aliwahi kutoa mimba, muuliza swali zwazwa na anayeulizwa naye zwazwa likajibu ndio. Yaani mambo mengine ni Fedheha.
Ninyi mnaomiliki vyombo vya habari lazima muelewe kuwa mmebeba dhamana kubwa ndani ya jamii. Tafuteni watu wenye akili zilizojitosheleza, hata Kama Elimu walikimbia basi walau hata akili wawe nazo.
Sasa mnaokoteza wahuni wahuni huko ambao kwao ngono zembe ni sifa, kwao kuzungumzia ishu zisizojenga jamii ndio wanaona huo ndio ujanja na kuwa maarufu, msiajiri vichaa walioathirika kisaikolojia.
Na Kama mtaajiri basi tafuteni Wataalamu wawa-brash saikolojia zao ziwe Sawa.
Wapo waandishi WA habari ambao wanaheshimu kazi zao, wanazipenda na wanatamani Taaluma ya uandishi wa habari iheshimiwe, lakini wanaharibiwa na Hawa wahuni ambao wanadhani kupiga piga mdomo bila akili ndio uandishi wa habari.
Ndio matokeo yake mnahoji watu wanakuambia Yesu alikuwa Tapeli.
Hivi mpaka unamhoji mtu si ushasoma saikolojia yake na kuona mtu huyu akili hamnazo au zinachaji.
Unamhoji alafu unacheka Cheka Kama Mpumbavu.
WAANDISHI MAKANJANJA mubadilike, msituletee mambo ya kipuuzi, jifunzeni kuiheshimu jamii Kama ninyi mmeshindwa kujiheshimu. Heshimuni kazi.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro