Uwezo wa kuhoji kila kitu ni sifa muhimu ya ukuzaji wa ubinadamu na chachu ya maendeleo katika njia tofauti

Uwezo wa kuhoji kila kitu ni sifa muhimu ya ukuzaji wa ubinadamu na chachu ya maendeleo katika njia tofauti

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Binadamu ameumbwa kwa upekee unaomfanya kila mmoja kujuona kwa namna yake. Hitaji kubwa la mwanadamu ni uhuru dhidi ya kila kitu.

Taasisi nyingi zilizopo leo kwa upekee wake zina mazingira ya kupora uhuru na kujenga mazingira ya hofu kwa mwanadamu ili aweze kutawalika.

Baadhi ya maandiko ya vitabu vikubwa duniani yanamuweka mwanadamu katikati ya kila kitu “human centered”. Hivyo kutawala siyo jukumu la mtu au kikundi fulani tu cha watu ila ni jukumu la kila mtu.

Siyo jambo la ajabu kwakuta wanaoitwa watawala wakichukiwa na watawaliwa hata kama watawala hao wanafanya mambo wanaoyaona ni mazuri kwa sababu watawaliwa nao huona kama wamepokwa jukumu lao.

Hali hii ndiyo inayosababisha migogoro msingi ya kitabaka kutokupata suluhu za kudumu hivyo njia inayobaki ni ile ya kuizima uhuru kwa kumuamini njia yoyote ile kupandikiza hofu.

Watu wanapokosa uhuru wa kuhoji kila kitu wanakosa ladha halisi ya uwepo. Chini ya mwamvuli wa hofu na mashaka ni sauti chache mno zinazosikika.
 
Back
Top Bottom