Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Mkuu humu wataanza kukuogopa...

Hahahaaaaa Zamaulid nimecheka hadi kidogo nipaliwe nakumbuka siku ya kwanza Kupewa maiti niiweke vizuri sikulala na kwakweli sikula nyama karibia wiki 2! Ilikuwa maiti iliyochomwa moto halafu ukazimwa kabla haijateketea yote.

Na kuna wakati nikakosa mchumba hivi hivi baada ya kumwambia nafanya kazi gani hakulala aliaga na hakurudi tena.
 
Last edited by a moderator:
Ninaamini kuongea na wafu ni kweli, kuota ni moja ya kuongea nao hebu nieleweshe zaidi mshana

Kwanza lazima tukubaliane kuwa ndoto ni vague memories ya matukio yote ya kila siku yawe ya kuwaza kunena na kutenda lakini inapotokea marehemu kakutokea ndoroni na ujumbe fulani kwako hiyo ni ndoto ya ujumbe yenye uhalisia

Binafsi babu yangu mzaa mama aliniaga, nakumbuka ilikuwa kwenye saa nane usiku hivi nikajikuta niko nyumbani kwa babu tumekaa naye kuna kitu ananianbia

Kuamka asubuhi zikaja taarifa za kifo chake na sehemu tulipokuwa tumekaa ule usiku ndipo alipozikwa
 
Last edited by a moderator:
Roho na nafsi huwa havifi bali hubaki vikizunguka huko na huko na ndio maana kwasababu haijakamilika kuwa binadamu kamili basi huitwa mzimu/mizimu
Mizimu si majini wala vinyamkera bali ni roho za watu waliokuwa na maisha yao kama sisi
Zamani tukienda kutambika tulikuwa tunaimba hivi
Taaambaa tiase nkoba, tiombe Mungu mzimu wa Saita kagone
Yaani... tughani tutupe tunguli,tumuombe Mungu MZIMU wa Saita kalale
Haya ni mambo ya kimila.mizimu ilikuwepo na iliabudiwa

Mkuu wamissionari walikataza hiyo!
 
mkuu mshana jr ni jins gani naweza zungumza na marehem?hasa niliempendaa

Hakuna ufundi mkubwa zaidi ya kumsogelea na kumwambia taratibu kile unachotaka kumwambia
Kumbuka hatakujibu wala kugeuka au kushtuka lakini akikubaliana na ombi lako utagundua tu tofauti
Kwa mfano kama mikono ilikuwa inakakamaa kwenye kumvalisha mikono hiyo hiyo hulainika
 
Last edited by a moderator:
Mkuu naomba ufafanuzi hapo; Hivi zamani si walikua wakiongea na mizimu ya marehemu!!! Marehemu hao walikuaje? walioneka vipi? waliwasiliana vipi?
 
Mkuu naomba ufafanuzi hapo;
Ivi zamani si walikua wakiongea na mizimu ya marehemu!!! Marehemu hao walikuaje? walioneka vipi? waliwasiliana vipi?

Mawasiliano yalikuwapo kwa njia ya matambiko haya matambiko yalikuwa kwa njia tofauti na kwa vipindi tofauti
Yalikuwapo ya kumtakia mtu safari njema masomo mema ndoa njema nk
Yalikuwepo ya kuombea mvua na amani pia
Yalikuwepo ya shukrani za kumaliza mwaka salama na matukio mengine makubwa

Na hapa ulitumika 'mzimu' wa fulani ambaye katika maisha yake alikuwa mahiri kwenye hicho kitu

Mizimu haionekani na wala mwanadamu hana uwezo wa kusemeshana au kujibishana nao bali kwa kutumia matambiko hayo kuna dalili zilijitokeza kuonyesha kwamba ombi limekubaliwa ama kukataliwa
 
Mimi nakubaliana na wewe katika hili.Ni kweli kabisa unayosema maana nimewahi kusikia hivi kutoka kwa bibi yangu akinihadithia mikasa aliyoiona kwa macho yake.
Pia marehemu babu yangu amewahi kufanya hivi pale alipoingia adui yake katika chumba alichokua anaoshewa.
Kwahili ni dhahiri marehemu hua wanasikia.

Loh binamu mpaka kwenye ushirikina upo? Nimekuvulia kofia
 
Binafsi siamini hata kidogo au kwa point ndogo tu, maana naamini kadiri unavyoiweka nafsi yako ndipo pale na wewe utakapokuwepo. Kwa vile nimewahi kuhusika kwa namna moja kwenye habari ya maiti nadhani hii imekaa sivyo.
Mshana Jr.

Hiyo imekaa kimizimu zaidi si reality, maana wafu hawana mawasiliano yoyote na mtu aliye hai labda ni mizimu hiyo, ndo maana nikasema unavoamini ndivo inavokuwa ktk maisha yako.
 
Hakuna ufundi mkubwa zaidi ya kumsogelea na kumwambia taratibu kile unachotaka kumwambia
Kumbuka hatakujibu wala kugeuka au kushtuka lakini akikubaliana na ombi lako utagundua tu tofauti
Kwa mfano kama mikono ilikuwa inakakamaa kwenye kumvalisha mikono hiyo hiyo hulainika

Kwhy ikiwa mtu ashazikwa hivyo hakuna namna tena ya kumwambia nilichotaka kumwambia?
 
Hamua kuweka nafsi yako kuongea na mizimu itakuwa na utaweza kumwambia.
Maana kila nafsi ikijizatiti kwa jambo na kuweka nafsi yako kwa hilo utaweza tu, lakini siyo umekurupuka toka zako sehemu ndo ukawaambia watu msibani "... ngojeni nimesahahu kumuuuliza mjomba kuhusu urithi wa ..."

Hapo ni Noooo.


Kwhy ikiwa mtu ashazikwa hivyo hakuna namna tena ya kumwambia nilichotaka kumwambia?
 
Mkuu mshana jr umetisha kwenye uzi huu, ila endelea kutiririka ujue tunakusoma kwa makini sana tuweze kufahamu haya ambayo wengi hatuyajui. Inaelekea katika mambo haya uelewa wako ni mkubwa sana kama ilivyo katika mambo mbali mbali ambayo huchangia hapa jamvini.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom