Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Ulichopaswa kufanya ni kuongea tu na kumwambia kila kitu, asingeweza kukujibu kwakuwa tayari alishaachana na nafsi lakini amini usiamini ungeyapata majibu kwa namna ya ajabu kabisa

inaelekea wiki ya nne sasa natamani hata anitokee japo nimwambie jambo ambalo sikumwambia one day before hajaenda.duh
We were so close.Kaa two weeks ago nimemwota nipo naye kama kawaida yetu tunapiga story na kucheka.This time tulikua tunamcheka baba yake mdogo alivokua analia msibani.
R.I.P dear.
 
Naomba kujua kwa nn uliacha hiyo kazi jeeh kuongea na maini ni somo la darasani au ni upeo tu uliopewa na mwenyezi muumba...

Nilikuwa mafunzoni na baada ya kumaliza masomo yangu nilirudi kwenye maisha yangu ya kawaida

Kuongea na marehemu ni mafunzo ya kawaida kabisa ambayo kwa asilimia nyingi hutokana na uzoefu na kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu
 
Nduguyangu mshana nyagi ilikwisha jana hiyo,naswali mpenzi mamayangu alifariki takribani miaka mi 2 sasa na alikuwa ananipenda sana ila tangu afariki hajawahi kunitokea japo kwenye ndoto je nifanyeje anitokee?au kuna baya nimelifanya?

Kwanza pole sana kwa kuondokewa na mzazi ni pigo kubwa sana! Hakuna baya ulilofanya mwache apumzike huko aliko, anaweza kukutokea siku kukiwa na tatizo
 
Hadithi tu hizi ,hakuna lolote.Mtu akifa hawez tena kuwasiliana na walio hai.Kinachoendelea baada ya kifo ni ujanja wa shetani tu kuwadanganya wanadamu kuwa marehemu wao wapo sehemu fulani wanaishi.
 
Hadithi tu hizi ,hakuna lolote.Mtu akifa hawez tena kuwasiliana na walio hai.Kinachoendelea baada ya kifo ni ujanja wa shetani tu kuwadanganya wanadamu kuwa marehemu wao wapo sehemu fulani wanaishi.
wakikosi shetani hajawahi kusema hivyo kwakuwa shetani naye hana uwezo huo wa kuongea na wanadamu
 
Last edited by a moderator:
Kwani kuna baadhi ya watu huwainaaminika kuwa wanaongea na mizimu kwenye baadhi ya koo na familia fulani hapa nchini,utaona mtu anasema nimezungunza na marehemu babu yenu jana.
 
Kwani kuna baadhi ya watu huwainaaminika kuwa wanaongea na mizimu kwenye baadhi ya koo na familia fulani hapa nchini,utaona mtu anasema nimezungunza na marehemu babu yenu jana.

Wengine ni imaginations tu ambazo zikikomaa kwenye sense ya sita hujenga taswira halisi ya kitu
 
Mkuu mshana jr umetisha kwenye uzi huu, ila endelea kutiririka ujue tunakusoma kwa makini sana tuweze kufahamu haya ambayo wengi hatuyajui. Inaelekea katika mambo haya uelewa wako ni mkubwa sana kama ilivyo katika mambo mbali mbali ambayo huchangia hapa jamvini.

Nashukuru kaka japo kuna changamoto zake wakati mwingine lakini changamoto ni sehemu ya maisha
 
Last edited by a moderator:
Mshana habari mkuu...sante kwa somo nzuri..japo nadhani ni pana na gumu ila umejaribu kuliweka kwwnye wepesi...

Mkuu mshana niambie kuhusu roho..baada ya kifo huenda wapo..kuna sehemu nilisoma wanasema zinakuwa ni wondering soul...je mwisho wake ni nini...zinakufa

Kwenye kusoma soma kunasehem mtu alisema kuna watu hawaji ila zile soul zinatafuta mwili mwingine na kuishi...kuna ukweli gan???..

Kuna pengine wanasema soul zote duniani they are connected..kwamba this life unaweza kuwa mwanadamu next life unakuwa mti..next unakuwa labda mbwa...n so on n so on..kuna ukweli gani hapo!!!!.
Samahani mkuu mshana jr kama ntakuwa nje ya mada..napenda kujifunza na kufaham yaliyomo kwa ulimwengu.
 
Sabrina kiukweli ni kwamba roho haifi hata siku moja maandiko ya dini na imani zote yanathibitisha hivyo, kinachotofautiana ni maelezo tu na ufafanuzi kwamba
-Baada ya maisha haya kuna pepo na jehanam kutegemeana na matendo binafsi ya MTU
-kwamba ufufuko siku ya mwisho, roho zilizolala kaburini zitakapoamshwa kwa ajili ya hukumu
-kwamba kuna rebirth/reincarnation
-kwamba kuna mizimu majini vinyamkera mashetani na vizuka
-kwamba kuna miungu

Vyote hivyo hapo hakuna mahali popote panapoonyesha kuwa kuna siku roho itakufa, roho haifi kwakuwa ni energy/ vital energy ni kitu kisichoonekana kwa macho wala kwa darubini

Roho ipo potepote haina wakati SAA muda urefu ufupi unene ujazo rangi, nk! Roho haili hainywi haina hisia zozote haikamatiki wala haifugiki(sio kwa maana ile ya kunguru)
Roho ipo wakati wote na mahali pote , haitakaa itokee duniani roho ife never
 
Last edited by a moderator:
Roho na nafsi huwa havifi bali hubaki vikizunguka huko na huko na ndio maana kwasababu haijakamilika kuwa binadamu kamili basi huitwa mzimu/mizimu
Mizimu si majini wala vinyamkera bali ni roho za watu waliokuwa na maisha yao kama sisi
Zamani tukienda kutambika tulikuwa tunaimba hivi
Taaambaa tiase nkoba, tiombe Mungu mzimu wa Saita kagone
Yaani... tughani tutupe tunguli,tumuombe Mungu MZIMU wa Saita kalale
Haya ni mambo ya kimila.mizimu ilikuwepo na iliabudiwa

Zumbe nkwei kabisa mghoshi ne tivye tambika uko shambaai.
 
Sabrina ni kweli roho huko ziliko ni ready made yani kinachofanyika ni kutafutiwa maumbo tu ya kuingia na utambulisho/nafsi kwamba huyu ni mnyama, mdudu, mwanadamu, nk na hakuna roho inayoangamia hata siku moja bali kinachoangamia ni umbo, utambusho/ID hubaki kama kumbukumbu kwamba 'a'likuwepo mshana jr 'a'kawa hivi au vile 'a'kafariki maiti/mwili 'wake' 'u'kapotea/'u'kazikwa/'u'kaungua na Mungu 'a'ilaze roho yake mahali pema peponi huo ndio utambulisho unaobaki

Kwahiyo mimi ni muunganiko wa vitu vitatu mwili nafsi na roho, nje ya hapo kuna mwili wangu, roho yangu na nafsi yangu
 
sante saana mshana jr somo zuri...kama hutajali je tofauti ya roho na nafsi ni nini????,

mtu akifa na nafsi inakufa???..
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom