Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Hungry ghosts hawana nafasi tena na kama ipo huwachukua kipindi cha KALPA moja kuweza kurudi kuwa binadamu KALPA moja hupimwa kwa kipimo cha jiwe moja la tani tano limegwe kipande kidogo kisochozidi robo kilo kila mwaka maramoja mpaka liishe hiyo ndio KALPA
Tulikuwa tunafanya ibada za kuwalisha kwakuwa wana matumbo makubwa lakini makoromeo yao kila kinachotaka kupita huunguzwa na moto mkali na kuyeyuka hapohapo

Hivyo basi wakati wa chakula tulikuwa tunafanya ibada ya kupoza ule moto ili japo maji na chakula kidogo kipite ndio maana wanaitwa hungry ghost

Kuweza kushuka na kuwa katika kiwango cha mwisho cha u binadamu ni pale mtu anapo fanya matendo ya kinyama na kutisha kabisa kwa viumbe hai ambayo hayasemeki hasa kutoa uhai wa viumbe vingi kwa wakati mmoja

mkuuu sante saaana napata elimu kubwa saaana..

inakuwaje matendo ya mwanadamu adhabu inapewa roho...wakati kwenye maamuzi ni binadamu au mwili ndo hufanya hayo maovu???

roho huzikwa??..kama kuna reincarnation which meanz roho ikitoka kwenye kiumbe kimoja inaenda kwenye kiumbe kingine...je roho wakati wa hukumu viumbe vingapi vitahukumiwa kama soul 1 imepitia kwa viumbe 3??
 
wa kwako mamkwaningi yasingmdamtuliwa[/QUOTE]

Ndio, kitu kama hakina msaada wowote katika maisha ya binadamu, hakina haja ya kujifunza kwani ni kupoteza mda tu. Hasa pale mtu anayekijua kushindwa kukiprove bila kuacha mashaka.
 
mkuuu sante saaana napata elimu kubwa saaana..

inakuwaje matendo ya mwanadamu adhabu inapewa roho...wakati kwenye maamuzi ni binadamu au mwili ndo hufanya hayo maovu???

roho huzikwa??..kama kuna reincarnation which meanz roho ikitoka kwenye kiumbe kimoja inaenda kwenye kiumbe kingine...je roho wakati wa hukumu viumbe vingapi vitahukumiwa kama soul 1 imepitia kwa viumbe 3??

Roho haifi, roho haizikwi kinachoadhibiwa si mwili bali ni nafsi+roho, mwili ni boya tu la kubeba nafsi/ufahamu na uhai/roho
Reicarnation yaweza kufanyika kwa zaidi ya roho moja.Rejea tafsiri ya roho lakini vilevile waweza ishi zaidi ya reincarnation tatu kwa kulipa mabaya ya reincarnation moja

Kwenye Biblia takatifu mafundisho yanatuasa kulinda moyo kuliko kitu kingine chochote kile kwakuwa humo ndio chemchem ya uzima hutoka
 
Reincarnation ndo nini?

Ni tendo la kuzaliwa tena katika umbo tofauti baada ya kufa kulingana na matendo uliyofanya ukiwa hai

Tofautisha rebirth na reincarnation. Rebirth hutumika zaidi kwa imani za Mungu mmoja ikimaanisha kuzaliwa upya/mara ya pili kiroho huku mwili ukiwa ni uleule

Reicarnation ni kuzaliwa mara ya pili na kuendelea huku roho ikiwa ileile lakini mwili tofauti
 
neo1kwanza asante kwa kuiweka vizuri hiyo tafsiri ya energy, kinachotokea kwenye hiyo reincarnation ni roho tu kuingia kwenye umbo ilimokusudiwa
Reicarnation ipo ulimwenguni kote na nje au ndani ya hapo
Kwenye matabaka ya reincarnation kuna
1.Budhas-viumbe wa juu kabisa ambao ni sawa na roho
2.Bodhisativas wanaofuta kwa ubora, lakini bado wakiwa na uwezo kama budha
3.Arahants.-kundi la tatu kwa ubora, yaani ni kama malaika wakiwa na uwezo sawa na boddhisativas
Hayo makundi matatu hapo juu hujulikana kama heavenly beings/viumbe wa mbinguni

Halafu linafuata kundi la nne kwa ubora ambalo ni la binadamu wanaoishi maisha mazuri yasiyo na shida nyingi

Kisha kundi la tano binadamu wenye maisha magumu na matatizo ya kila aina

Kundi la mwisho ni hungry ghosts hawa matendo yao yalikuwa mabaya kiasi kwamba hawafai kabisa hata kupata mateso ya kawaida bali huko chini jehanam kwenye kila aina na mateso

Kwahiyo utaona kuwa kwa mtiririko huo hizi roho zipo popote pale ulimwenguni n beyond

Aiseeeeeeee
 
Last edited by a moderator:
Mmh mambo haya sitaki hats ku-comment lakini ndo nshapost hivyo
 
changamoto mkuu.....unaweza kuzaliwa katika mwili mara 2 ....yaan unakufa katika mwili m1 na unaenda kwenye mwili mwingine???

je unaweza beba kumbukumbu zako kwenye previous life??? mshana jr
 
Last edited by a moderator:
changamoto mkuu.....unaweza kuzaliwa katika mwili mara 2 ....yaan unakufa katika mwili m1 na unaenda kwenye mwili mwingine???

je unaweza beba kumbukumbu zako kwenye previous life??? mshana jr

Hapana kumbukumbu zinabaki na nafsi/ufahamu roho kazi yake ni uhai tu
 
Last edited by a moderator:
Hapana kumbukumbu zinabaki na nafsi/ufahamu roho kazi yake ni uhai tu

So it means roho yangunkwa mfano nikifa itakuwa haina kumbu kumbu yeyote ya maisha niliyoishi walau kukumbuka nilipotokea?
 
So it means roho yangunkwa mfano nikifa itakuwa haina kumbu kumbu yeyote ya maisha niliyoishi walau kukumbuka nilipotokea?

Kuna coicedence chache kwa wale waaminio katika reicarnation kuhusu past life lakini ishu ya kubeba kumbukumbu ni ubongo na ufahamu
Ndio maana ujinga au werevu wa mtu hutanabahishwa na ubongo na si moyo
 
Only in Africa ndipo watu wanaweza kupoteza muda namna hii.Sijaona hoja ya maana hapa kuhusu wafu.Ukisha kufa umekufa hakuna kuongea kinafsi wala chochote ,kinachobaki ni hisia zenu mliobaki tu zinazoongozwa na emotions.

Niwape mfano mmoja unaohusiana na hicho mkisemacho hasa pale kwamba marehem anaacha wosia.,mfano marehemu aache wosia kwamba akifa azikwe kijijini kwao Lindi lakini kwa bahati mbaya kafia majini akiwa safarini kwenda znz.Kutokana na mait yake kuharibuka serikal ikaamua wazikwe kabur la pamoja huko znz.,Hakuna chochote kitakacho tokea kinachohusiana na maneno /maagizo ya marehemu.

Wakati mwingine mnatakiwa mfikiria kama watu mlioko karne ya 21 na msiturudishe nyuma.Hivyo vitu vingine ni kuendekeza tu na kuendelea kufanya jamii kuwa maskini kwa fikra za zamani.

Only in Africa ambapo utaona mtu anamshika mtu kichwa na kutamka et shetani toka kisha mtu yule akaanza kurusha miguu juu.Huu ni upuuzi na umaskini wa mawazo,kwani ni waafrica tu ndiyo walio na majini?.Hii ni hatar sana.

Only in africa ndipo utakuwa watu wameacha kufanya kazi ama kupumzika na familia zao wameenda kukusanyana wakisali ,kuimba na kutoa pesa huku wakiamini kwamba wanaondolewa dhambi zao na eti wakifa wataenda mbinguni.
 
Je mkuu mshana jr ikiwa mtu keshazikwa je inawezekanaaa
 
Last edited by a moderator:
Astral body ni practice mizimu ni roho, zinahusiana tu kiroho kuwa moja ni roho hai na moja ni roho mfu

Ni Sawa mkuu but nachofahamu roho ni Union haina utenganifu
Naomba ufafanuzi kidogo
 
Ni Sawa mkuu but nachofahamu roho ni Union haina utenganifu
Naomba ufafanuzi kidogo
yang astral practice ni practice kwa maana ya kwamba mtu anaamua sasa roho iachane na mwili, hapo mwili unakuwa domant lakini una uhai wakati roho ya pili inaachana na mwili milele na mwili hauko domant tena bali huwa mfu
 
Last edited by a moderator:
habari ya muda huu mshana jr,

sante kwa somo zuri kuhusu roho....ila.bado nina maswali mawili yana nitatiza...

inakuaje mpaka roho inageuka inakuwa bad ghost...nini kinaamua roho kwenda kwenye kiumbe kingine???...au what make reincarnation???

je roho za kawaida zinaweza fika level za Buddha???..au kuna selected number ya kuwa Buddha??.....
 
Last edited by a moderator:
hiyo app ndio ninayotumia kuhabarika hapa kwa kusoma habari na kucomment, ninachohitaji ni jinsi ya kuweza kupost na watu wakasoma kile nilichoandika. Nadhani nimejibu vyema kaka mshana jr.
 
habari ya muda huu mshana jr,

sante kwa somo zuri kuhusu roho....ila.bado nina maswali mawili yana nitatiza...

inakuaje mpaka roho inageuka inakuwa bad ghost...nini kinaamua roho kwenda kwenye kiumbe kingine???...au what make reincarnation???

je roho za kawaida zinaweza fika level za Buddha???..au kuna selected number ya kuwa Buddha??.....

Kinacholeta haya yote ni matendo yetu ya kila siku, cause n effect yani kila ufanyalo lina malipo yake hakuna msamaha
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom