Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Dunia imekuwa kama kijiji kutokana na uwezo mkubwa aliounyesha mwanadamu wa kugundua hata ambavyo vilifikirika kwamba haviwezekani

Elimu na ufahamu kuhusu mwili wa mwanadamu kuanzia kuumbwa tumboni kuzaliwa hadi kufa umetafitiwa na kunyumbulishwa kwa mapana yake na wengi wamepata elimu ya juu kabisa PhD kwenye hili eneo, lakini wakashishindwa kitu kimoja tuu!!! Uwezo wa kumuita marehemu na kuongea naye

Zamani kabla ya dini za kigeni hazijaja Africa tulikuwa kwa kiasi fulani tuna uwezo wa kuwaita marehemu kwa njia ya matambiko na kuwaomba hili au lile, lakini ikumbukwe kwamba hawakuja live bali dalili na ishara kadha zilionyesha uwepo wao na kukubali au kukataa ombi husika

Tumekuwa tunaondokewa na wapendwa wetu na watu tunaowahitaji mno katika maisha yetu, tumekuwa na vipindi vigumu kabisa ambapo tunawahamu na kuwahitaji japo wajitokeze kwa dakika chache tu lakini haikuwezekana kabisa

Mfu ni mfu na hatuna uwezo wowote iwe wa kimwili au wa kiroho kuweza kumuita na kuongea naye lolote, hii ni kwakuwa roho inapotengana na mwili hakuna tena huyo MTU bali kunatokea vitu vitatu visivyoweza kuungana tena na kutengeneza kitu kimoja. vitu hivyo ni roho mwili na nafsi, vitatu hivi ndio vinatengeneza MTU nje ya hapo kuna 'mwili wake', 'roho yake' au 'nafsi yake'

Watu wamejaribu kutoa shuhuda nyingi za kutokewa na marehemu, hili linawezekana kwasababu baada ya kifo kuna roho huwa zinawayawaya duniani, zipo tu na hizi ndizo ambazo hugeuka mizimu mizuri au mibaya

Wakati mmoja tu marehemu anaweza kusikia sauti ya mwanadamu na kuitii ni pale tu anapoandaliwa kwa safari yake ya mwisho kaburini, hasa kwenye ishu ya kumsafirisha au kumvalisha nguo

Nikiwa mtu ambaye nilidili na miili ya marehemu kwa miaka mitatu mfululizo nilikutana mara nyingi tu na hizi hali, marehemu hataki dharau ubishi au kufokewa nguo hata iwe inamtosha Siku hiyo itakataa mpaka mumbembeleza

Tuna wajuaji wengi Siku hizi wanaojifanya wametokewa na marehemu fulani na kumpa maagizo Fulani hizi kwa asilimia 90 ni story tu kwakuwa hatujakuwa na uwezo wa kuwaita au wao kututokea tu na uchafu wote huu tulionao

GWAJIMA anasema Ana uwezo wa KUFUFUA WAFU.
Mbipu akusaidie.
 
roho ni pumzi tu, ukifa ikitoka imetoka, anayesemammengine ati roho ina akili sijui inatoka inatembeatembea ni fix tu, wanaosema wameona marehemu waende tu kumuona daktari, watu wengi ni wagonjwa wana hallucinatenzaidi ya watu mnavofikiri, ila kusema ati marehemu kamuongelesha hua ni story tu hakuna ukweli wowote.. Tumejazwa madudu washa toka utotoni, inabidi tusiendelee kuwajaza watoto wanaokuja wasiendeleze ujinga miaka ijayo

Wakati biblia yako imeeleza jinsi mwanamke mpiga ramli alivyoongea na roho ya nabii Samuel ambaye Alikuwa amekufa.
Soma biblia yako. Usiwe mtu wa kujazwa upumbavu.
 
Mmeacha dini, mila, disturi, tamaduni za mababu zenu mtawezaje kuwasiliana na wafu.?

Nilitegemea ungetoa ufafanuzi zaidi juu ya maswali niliuliza hapo. Sjui ni ujuaji au umbumbumbu tu!!!! Anyway, How could you know babu yangu alikuwa na hizo mila?
 
Naomba usikwazike ni jukwaa hivyo mitazamo ni mingi na inatofautiana kwenye kuiwakilisha
 
Wakati biblia yako imeeleza jinsi mwanamke mpiga ramli alivyoongea na roho ya nabii Samuel ambaye Alikuwa amekufa.
Soma biblia yako. Usiwe mtu wa kujazwa upumbavu.

Mkuu em kasome upya urudi unambie panasemaje, afu njoo na uandike kabisa tukufafanulie sio unakurupuka kusema upumbavu, hakuna upumbavu wowote nliojazwa, we ndo umejazwa maana umekariri tu vitu ndivyo sivyo
 
Mkuu mshana Jr hiyo elimu ya kuongea na wafu IPO na inawezekana,mfano sisi waha tuna matambiko yetu huwa tunayafanya mto lugohe au mgandazi kulingana na ukoo sasa kwetu tuna mizimu ya mtusi kazi mhambwe na mtanganyika unapofanya tambiko na likakubaliwa utawaona hao mizimu na kula utakula nao na watakueleza Maisha yao kingine mtu anaweza kufa ktk mazingira ya kutatanisha na mkazika hapa sizungumzii misukule nazungumuzia mtu alikufa kabisa unaweza kwenda kabulini kwake na kumfufua kisha ukaongea nae hapa unatakiwa kujua mtu huyo unampomfufua anakuja duniani kulipa kisasi hivyo lazima ujue kuwa huyu mtu kauliwa iwe kwa uchawi au kwa kupigwa na watu mana anapofufuliwa huja kwa kisasi kisha akimaliza hurudi kuwa mfu milele kuna vingi vya kuongea ila mengine ni siri hasa ukizingatia humu kuna waumini wa dini nyingi
 
Hapana usijali tuongee tu kwa uwazi ndio maana hii mada ikatolewa kule mchanganyiko na kuletwa huku intelligence kaka
Nafahamu hizo za namna hiyo zipo lakini mimi nilikuwa namaanisha kuwa katika hali ya kawaida kabisa mtoto amemkumbuka sana mzazi wake, basi kungekuwa na aina fulani ya elimu inayomwezesha mtoto kuweza kumuita mzazi aliyefariki na kuongea naye japo kidogo halafu huyo mzazi akatoweka, akarudi kuzimu...! Naamini hii elimu ya namna hii imeshindikana
 
Nimekuelewa kaka mshana Jr kwa sisi tunaomini ktk mizimu uwezo wa kumuita mzee wako na kuongea nae upo ila inategemea unamuita kwa kusudio lipi nitakupa mfano Mimi kipindi nazaliwa miaka 25 nyuma ilitokea kukataa jina mana baba yangu alikua mganga mkubwa tu hivyo jina nililopewa mizimu ikakataa wakitka nipewe jina watakalopendeza wao kilichotokea ni kuitwa kwa mizimu ya mababu na majini ya mzee likatoka jina moja kwa mizimu na lingine kwa majini nikawa natumia yote hiyo ndio namna unavyoweza kuita mtu aliyekufa na kuongea nae ila mila nyingi zimehalibiwa na utamaduni wa hizi dini ila kungekuwa na utamaduni wetu kuna vitu watu wangejifunza na kuvijua na kuulewa ulimwengu huu ila wale wanaojua wanatumia na wamenufaika sana ila tutafundishana taratibu na kila mtu atajifunza na kuelewa ili tunufaike wote mana najua kuna watu wangependa kuongea na ndugu zao waliokufa ila hawajui waanzie wapi
 
Hapana usijali tuongee tu kwa uwazi ndio maana hii mada ikatolewa kule mchanganyiko na kuletwa huku intelligence kaka
Nafahamu hizo za namna hiyo zipo lakini mimi nilikuwa namaanisha kuwa katika hali ya kawaida kabisa mtoto amemkumbuka sana mzazi wake, basi kungekuwa na aina fulani ya elimu inayomwezesha mtoto kuweza kumuita mzazi aliyefariki na kuongea naye japo kidogo halafu huyo mzazi akatoweka, akarudi kuzimu...! Naamini hii elimu ya namna hii imeshindikana

Mkitoa huo ujuzi hapa mtakuwa mmetusaidia na sisi tuliofiwa na wapendwa wetu. Angalau mara moja kwa miezi sita kuongea nae si mbaya.
 
Siku niliyopata msiba wa mtu wangu wa karibu ndio siku niliyotaman nipate ht uwezo mdogo wa kuongea nae angalau nipate mawazo yake kwa baadhi ya mambo.

Pole sukula.upo!!!?
 
Kuna tofauti ya roho na nafsi? nilijua ni kitu kimoja...., hizo habari za marehemu kukataa au kutii kuvaa ni porojo..., peleka sokoni
 
Dunia imekuwa kama kijiji kutokana na uwezo mkubwa aliounyesha mwanadamu wa kugundua hata ambavyo vilifikirika kwamba haviwezekani

Elimu na ufahamu kuhusu mwili wa mwanadamu kuanzia kuumbwa tumboni kuzaliwa hadi kufa umetafitiwa na kunyumbulishwa kwa mapana yake na wengi wamepata elimu ya juu kabisa PhD kwenye hili eneo, lakini wakashishindwa kitu kimoja tuu!!! Uwezo wa kumuita marehemu na kuongea naye

Zamani kabla ya dini za kigeni hazijaja Africa tulikuwa kwa kiasi fulani tuna uwezo wa kuwaita marehemu kwa njia ya matambiko na kuwaomba hili au lile, lakini ikumbukwe kwamba hawakuja live bali dalili na ishara kadha zilionyesha uwepo wao na kukubali au kukataa ombi husika

Tumekuwa tunaondokewa na wapendwa wetu na watu tunaowahitaji mno katika maisha yetu, tumekuwa na vipindi vigumu kabisa ambapo tunawahamu na kuwahitaji japo wajitokeze kwa dakika chache tu lakini haikuwezekana kabisa

Mfu ni mfu na hatuna uwezo wowote iwe wa kimwili au wa kiroho kuweza kumuita na kuongea naye lolote, hii ni kwakuwa roho inapotengana na mwili hakuna tena huyo MTU bali kunatokea vitu vitatu visivyoweza kuungana tena na kutengeneza kitu kimoja. vitu hivyo ni roho mwili na nafsi, vitatu hivi ndio vinatengeneza MTU nje ya hapo kuna 'mwili wake', 'roho yake' au 'nafsi yake'

Watu wamejaribu kutoa shuhuda nyingi za kutokewa na marehemu, hili linawezekana kwasababu baada ya kifo kuna roho huwa zinawayawaya duniani, zipo tu na hizi ndizo ambazo hugeuka mizimu mizuri au mibaya

Wakati mmoja tu marehemu anaweza kusikia sauti ya mwanadamu na kuitii ni pale tu anapoandaliwa kwa safari yake ya mwisho kaburini, hasa kwenye ishu ya kumsafirisha au kumvalisha nguo

Nikiwa mtu ambaye nilidili na miili ya marehemu kwa miaka mitatu mfululizo nilikutana mara nyingi tu na hizi hali, marehemu hataki dharau ubishi au kufokewa nguo hata iwe inamtosha Siku hiyo itakataa mpaka mumbembeleza

Tuna wajuaji wengi Siku hizi wanaojifanya wametokewa na marehemu fulani na kumpa maagizo Fulani hizi kwa asilimia 90 ni story tu kwakuwa hatujakuwa na uwezo wa kuwaita au wao kututokea tu na uchafu wote huu tulionao

Biblia inasema Wafu hawajui neno lolote, hapo kwenye red ni imani tu lakini hakuna uhalisia. "Mhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. 6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua."
 
Hiyo sio tafsiri yake na hapa unazungumzia neno wakati mimi nazungumzia nilichokutana nacho katika uhalisia wake
 
Back
Top Bottom