Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahahaaaaa Zamaulid nimecheka hadi kidogo nipaliwe nakumbuka siku ya kwanza Kupewa maiti niiweke vizuri sikulala na kwakweli sikula nyama karibia wiki 2! Ilikuwa maiti iliyochomwa moto halafu ukazimwa kabla haijateketea yote
Na kuna wakati nikakosa mchumba hivi hivi baada ya kumwambia nafanya kazi gani hakulala aliaga na hakurudi tena
TODAYS Tunaweza kuwa na misimamo na maono tofauti katika hili lakini binafsi nimekutana na mengi zaidi ya haya hasa kwenye kumuandaa marehemuBinafsi siamini hata kidogo au kwa point ndogo tu, maana naamini kadiri utakavyoiweka nafsi yako ndipo pale na wewe utakapokuwepo. Kwa vile nimewahi kuhusika kwa namna moja kwenye habari ya maiti nadhani hii imekaa sivyo.
Mshana Jr.
Hiyo imekaa kimizimu zaidi si reality, maana wafu hawana mawasiliano yoyote na mtu aliye hai labda ni mizimu hiyo, ndo maana nikasema unavoamini ndivo inavokuwa ktk maisha yako.
Kwasasa mimi ni mjasiriamali
Mawasiliano yalikuwapo kwa njia ya matambiko haya matambiko yalikuwa kwa njia tofauti na kwa vipindi tofauti
Yalikuwapo ya kumtakia mtu safari njema masomo mema ndoa njema nk
Yalikuwepo ya kuombea mvua na amani pia
Yalikuwepo ya shukrani za kumaliza mwaka salama na matukio mengine makubwa
Na hapa ulitumika 'mzimu' wa fulani ambaye katika maisha yake alikuwa mahiri kwenye hicho kitu
Mizimu haionekani na wala mwanadamu hana uwezo wa kusemeshana au kujibishana nao bali kwa kutumia matambiko hayo kuna dalili zilijitokeza kuonyesha kwamba ombi limekubaliwa ama kukataliwa
Loh binamu mpaka kwenye ushirikina upo? Nimekuvulia kofia
Nilikuwa msimamizi wa kuchoma maiti wenzetu kule mashariki ya mbali hawaziki wanachoma
mangatara hii habari yako imenifanya nisisimke, haya mambo yapo na watu wana shuhuda nyingi basi tu hawataki kuziweka waziMshana jr.
Umetoa wapi mawazo haya leo? Au babu yako kakutembelea? Siku ya arusi yangu, bibi mzaa baba aliyekuwa amefariki miaka kama 12 hivi iliyokuwa imepita alinijia usiku. Sisemi ilikuwa ndoto kwani nilikuwa sija lala na kibatari kilikuwa kinawaka. Akasimama karibu na kitanda changu akanikumbusha alivyokuwa ananipenda mjukuu wake.
Akasema; Nasikia unaoa, ninataka nitoe mchango wangu. Nitakupa weye mchango wangu kesho. Aka[otea, nilifadhaika kidogo ila kwa kuwa hakuna mtu mwingine aliyesikia sauti ya bibi nkaogopa kusema wasinicheke.
Keshoye, tulipotoka tu kanisani, tukapitia sehemu tupate chakula kidogo kwani mambo ya harusi wayajua. Ghafula pale chini sakafuni nikaona noti ya shs 10. Enzi hizo za '70 hiyo ilikuwa hela kubwa sana. Kama laki+ leo.
Je huo haukuwa mchango wa bibi yangu? Nafsi bado zipo hapa ila roho imerudi kwa mwenyewe ka mwili ulivyo rudi kuwa mavumbi
Hapana majini ni viumbe tofauti kabisa
mangatara hii habari yako imenifanya nisisimke, haya mambo yapo na watu wana shuhuda nyingi basi tu hawataki kuziweka wazi
mshan jr;
Siamimi habari za mizimu kuwa rafiki ila najua ipo, na inafanya mengi tu. Kwetu tumezaliwa wengi kidogo. Mdogo wangu anayenifuata siku alipofariki ghafula niliona maajab.
Kwanza ilikuwa hivi; Jana yake tuligombana tukapigana ka watoto wafanyavyo. Kwa kuwa nilikuwa sikubali kupigwa na mdogo, nikamshikisha adab. Keshoye kafariki ghafula, japo si kwa kipigo changu kwani naye alinitwanga si kidogo. Ni kwa ugonjwa sikuujua kwani tulikuwa wadogo tu. Umri wa 12 kwa 10.
Cha ajab, usiku wa alipozikwa, nikiwa nimelala kitanda kimoja na baba mzazi, jamaa alikuja, akaniamsha, alianza kunipiga mangumi, mateke mpaka damu zikanitoka puani. Nikapiga yowe, baba akaamka ghafula, akawasha taa. Damu zinatiririka puani, kuuliza kisa nikamwambia kuwa ni jamaa alikuja akanipiga. Baba akaona kuwa ni ndoto. Akaamuru nilale.
Mara tukasikia hodi zinapigwa huko nje. Mama mdogo kamleta mdogo wangu mwingine kutoka kwake, ati alienda kupiga hodi huko anataka chakula. Alipoulizwa amekuja na nani usiku ule, akasema ni huyo jamaa alimfungulia mlango wa chumba cha mama yetu na kumleta huko ili wale chakula.
Je, ni ndoto au ni kweli? Mimi nasema ni kweli kwani nilimwona na alinipiga ngumi ya pua damu zikatoka. Believe it or not, this is a true story