Mkuu humu wataanza kukuogopa...
Na kuna wakati nikakosa mchumba hivi hivi baada ya kumwambia nafanya kazi gani hakulala aliaga na hakurudi tena
Ninaamini kuongea na wafu ni kweli, kuota ni moja ya kuongea nao hebu nieleweshe zaidi mshana
Roho na nafsi huwa havifi bali hubaki vikizunguka huko na huko na ndio maana kwasababu haijakamilika kuwa binadamu kamili basi huitwa mzimu/mizimu
Mizimu si majini wala vinyamkera bali ni roho za watu waliokuwa na maisha yao kama sisi
Zamani tukienda kutambika tulikuwa tunaimba hivi
Taaambaa tiase nkoba, tiombe Mungu mzimu wa Saita kagone
Yaani... tughani tutupe tunguli,tumuombe Mungu MZIMU wa Saita kalale
Haya ni mambo ya kimila.mizimu ilikuwepo na iliabudiwa
mkuu mshana jr ni jins gani naweza zungumza na marehem?hasa niliempendaa
mkuu mshana jr ni jins gani naweza zungumza na marehem?hasa niliempendaa
Mkuu naomba ufafanuzi hapo;
Ivi zamani si walikua wakiongea na mizimu ya marehemu!!! Marehemu hao walikuaje? walioneka vipi? waliwasiliana vipi?
Mimi nakubaliana na wewe katika hili.Ni kweli kabisa unayosema maana nimewahi kusikia hivi kutoka kwa bibi yangu akinihadithia mikasa aliyoiona kwa macho yake.
Pia marehemu babu yangu amewahi kufanya hivi pale alipoingia adui yake katika chumba alichokua anaoshewa.
Kwahili ni dhahiri marehemu hua wanasikia.
Hakuna ufundi mkubwa zaidi ya kumsogelea na kumwambia taratibu kile unachotaka kumwambia
Kumbuka hatakujibu wala kugeuka au kushtuka lakini akikubaliana na ombi lako utagundua tu tofauti
Kwa mfano kama mikono ilikuwa inakakamaa kwenye kumvalisha mikono hiyo hiyo hulainika
Kwhy ikiwa mtu ashazikwa hivyo hakuna namna tena ya kumwambia nilichotaka kumwambia?