Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani


Kwan kazi yako ni nini
 
Last edited by a moderator:
TODAYS Tunaweza kuwa na misimamo na maono tofauti katika hili lakini binafsi nimekutana na mengi zaidi ya haya hasa kwenye kumuandaa marehemu

Sisemi kwamba ni kila marehemu la hasha ila wale wenye mushkeli haya mambo yapo na nimeyashuhudia live bila ya kusimuliwa
 
Last edited by a moderator:

Dah! Hapo kwenye mizimu ndipo panaponichanganya!!!

Ivi mzimu si ni jini aliekuwa anamilikiwa/anatumiwa na marehemu. Au?
 
Mshana jr.
Umetoa wapi mawazo haya leo? Au babu yako kakutembelea? Siku ya arusi yangu, bibi mzaa baba aliyekuwa amefariki miaka kama 12 hivi iliyokuwa imepita alinijia usiku. Sisemi ilikuwa ndoto kwani nilikuwa sija lala na kibatari kilikuwa kinawaka. Akasimama karibu na kitanda changu akanikumbusha alivyokuwa ananipenda mjukuu wake.
Akasema; Nasikia unaoa, ninataka nitoe mchango wangu. Nitakupa weye mchango wangu kesho. Aka[otea, nilifadhaika kidogo ila kwa kuwa hakuna mtu mwingine aliyesikia sauti ya bibi nkaogopa kusema wasinicheke.
Keshoye, tulipotoka tu kanisani, tukapitia sehemu tupate chakula kidogo kwani mambo ya harusi wayajua. Ghafula pale chini sakafuni nikaona noti ya shs 10. Enzi hizo za '70 hiyo ilikuwa hela kubwa sana. Kama laki+ leo.
Je huo haukuwa mchango wa bibi yangu? Nafsi bado zipo hapa ila roho imerudi kwa mwenyewe ka mwili ulivyo rudi kuwa mavumbi
 
mangatara hii habari yako imenifanya nisisimke, haya mambo yapo na watu wana shuhuda nyingi basi tu hawataki kuziweka wazi
 
Last edited by a moderator:
mangatara hii habari yako imenifanya nisisimke, haya mambo yapo na watu wana shuhuda nyingi basi tu hawataki kuziweka wazi

mshan jr;
Siamimi habari za mizimu kuwa rafiki ila najua ipo, na inafanya mengi tu. Kwetu tumezaliwa wengi kidogo. Mdogo wangu anayenifuata siku alipofariki ghafula niliona maajab.
Kwanza ilikuwa hivi; Jana yake tuligombana tukapigana ka watoto wafanyavyo. Kwa kuwa nilikuwa sikubali kupigwa na mdogo, nikamshikisha adab. Keshoye kafariki ghafula, japo si kwa kipigo changu kwani naye alinitwanga si kidogo. Ni kwa ugonjwa sikuujua kwani tulikuwa wadogo tu. Umri wa 12 kwa 10.
Cha ajab, usiku wa alipozikwa, nikiwa nimelala kitanda kimoja na baba mzazi, jamaa alikuja, akaniamsha, alianza kunipiga mangumi, mateke mpaka damu zikanitoka puani. Nikapiga yowe, baba akaamka ghafula, akawasha taa. Damu zinatiririka puani, kuuliza kisa nikamwambia kuwa ni jamaa alikuja akanipiga. Baba akaona kuwa ni ndoto. Akaamuru nilale.
Mara tukasikia hodi zinapigwa huko nje. Mama mdogo kamleta mdogo wangu mwingine kutoka kwake, ati alienda kupiga hodi huko anataka chakula. Alipoulizwa amekuja na nani usiku ule, akasema ni huyo jamaa alimfungulia mlango wa chumba cha mama yetu na kumleta huko ili wale chakula.
Je, ni ndoto au ni kweli? Mimi nasema ni kweli kwani nilimwona na alinipiga ngumi ya pua damu zikatoka. Believe it or not, this is a true story
 

Mmh kuna mengi kwenye hii habari ngoja nitarudi nipo mahali sitaweza kuwa makini kwenye kupost kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…