Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Dunia imekuwa kama kijiji kutokana na uwezo mkubwa aliounyesha mwanadamu wa kugundua hata ambavyo vilifikirika kwamba haviwezekani

Elimu na ufahamu kuhusu mwili wa mwanadamu kuanzia kuumbwa tumboni kuzaliwa hadi kufa umetafitiwa na kunyumbulishwa kwa mapana yake na wengi wamepata elimu ya juu kabisa PhD kwenye hili eneo, lakini wakashishindwa kitu kimoja tuu!!! Uwezo wa kumuita marehemu na kuongea naye

Zamani kabla ya dini za kigeni hazijaja Africa tulikuwa kwa kiasi fulani tuna uwezo wa kuwaita marehemu kwa njia ya matambiko na kuwaomba hili au lile, lakini ikumbukwe kwamba hawakuja live bali dalili na ishara kadha zilionyesha uwepo wao na kukubali au kukataa ombi husika

Tumekuwa tunaondokewa na wapendwa wetu na watu tunaowahitaji mno katika maisha yetu, tumekuwa na vipindi vigumu kabisa ambapo tunawahamu na kuwahitaji japo wajitokeze kwa dakika chache tu lakini haikuwezekana kabisa

Mfu ni mfu na hatuna uwezo wowote iwe wa kimwili au wa kiroho kuweza kumuita na kuongea naye lolote, hii ni kwakuwa roho inapotengana na mwili hakuna tena huyo MTU bali kunatokea vitu vitatu visivyoweza kuungana tena na kutengeneza kitu kimoja. vitu hivyo ni roho mwili na nafsi, vitatu hivi ndio vinatengeneza MTU nje ya hapo kuna 'mwili wake', 'roho yake' au 'nafsi yake'

Watu wamejaribu kutoa shuhuda nyingi za kutokewa na marehemu, hili linawezekana kwasababu baada ya kifo kuna roho huwa zinawayawaya duniani, zipo tu na hizi ndizo ambazo hugeuka mizimu mizuri au mibaya

Wakati mmoja tu marehemu anaweza kusikia sauti ya mwanadamu na kuitii ni pale tu anapoandaliwa kwa safari yake ya mwisho kaburini, hasa kwenye ishu ya kumsafirisha au kumvalisha nguo

Nikiwa mtu ambaye nilidili na miili ya marehemu kwa miaka mitatu mfululizo nilikutana mara nyingi tu na hizi hali, marehemu hataki dharau ubishi au kufokewa nguo hata iwe inamtosha Siku hiyo itakataa mpaka mumbembeleza

Tuna wajuaji wengi Siku hizi wanaojifanya wametokewa na marehemu fulani na kumpa maagizo Fulani hizi kwa asilimia 90 ni story tu kwakuwa hatujakuwa na uwezo wa kuwaita au wao kututokea tu na uchafu wote huu tulionao
 
Hebu fafanua kidogo hapo kwenye blue mkuu,....

Hii ngumu kidogo. Kma anaweza kataa nguo ina maana hubaki na mawasiliano katika ya nafsi, roho na mwili?

Iko hivi sikuwa anakataa live bali wakati wa kumvisha kama ni koti shati au hata suruali kuna kiungo kimoja hukakamaa kwa mfano kama ni mkono haunyanyuki au haukunjiki, kama ni mguu unajipinda au unakuwa mzito kunyanyua
Hivi vitu vinafanyika kwa namna ya ajabu na ya kipekee kabisa

Vilevile kuna kukosea vifungo au zipu kujichanganya! Yani mnaanza kufunga kifungo cha kwanza vizuri kabisa mkifika mwisho aidha vimepishana au mmeruka matundu, tulishawahi kukosea vifungo Mara SABA
Ni mpaka nilipotumia elimu niliyojifunza kuongea na marehemu kwa upole na kwa kumbembeleza ndio mambo yakawa sawa, na pia ndani ya chumba husika kama yupo mtu alikuwa na ugomvi na marehemu hakuna kitakachokwenda sawa hapo mpaka yule mtu atoke
 
Iko hivi sikuwa anakataa live bali wakati wa kumvisha kama ni koti shati au hata suruali kuna kiungo kimoja hukakamaa kwa mfano kama ni mkono haunyanyuki au haukunjiki, kama ni mguu unajipinda au unakuwa mzito kunyanyua
Hivi vitu vinafanyika kwa namna ya ajabu na ya kipekee kabisa

Vilevile kuna kukosea vifungo au zipu kujichanganya! Yani mnaanza kufunga kifungo cha kwanza vizuri kabisa mkifika mwisho aidha vimepishana au mmeruka matundu, tulishawahi kukosea vifungo Mara SABA
Ni mpaka nilipotumia elimu niliyojifunza kuongea na marehemu kwa upole na kwa kumbembeleza ndio mambo yakawa sawa, na pia ndani ya chumba husika kama yupo mtu alikuwa na ugomvi na marehemu hakuna kitakachokwenda sawa hapo mpaka yule mtu atoke

Mimi nakubaliana na wewe katika hili.Ni kweli kabisa unayosema maana nimewahi kusikia hivi kutoka kwa bibi yangu akinihadithia mikasa aliyoiona kwa macho yake.

Pia marehemu babu yangu amewahi kufanya hivi pale alipoingia adui yake katika chumba alichokua anaoshewa.
Kwahili ni dhahiri marehemu hua wanasikia.
 
Japo mwili hutawanyika na kuwa kitu kisicho kamili lakini maneno yoyote ya marehemu hubebwa na roho na nafsi yake.

Hizi habari za wosia si kitu cha kupuuza hata maramoja waliopuuza walipata habari yake mifano halisi ipo mingi kama marehemu alisema sitaki hivi na mkafanya tofauti baada ya yeye kufa maafa hutokea mara zote
 
Siku niliyopata msiba wa mtu wangu wa karibu ndio siku niliyotaman nipate ht uwezo mdogo wa kuongea nae angalau nipate mawazo yake kwa baadhi ya mambo.

Ulichopaswa kufanya ni kuongea tu na kumwambia kila kitu, asingeweza kukujibu kwakuwa tayari alishaachana na nafsi lakini amini usiamini ungeyapata majibu kwa namna ya ajabu kabisa
 
Roho ni pumzi tu, ukifa ikitoka imetoka, anayesema roho ina akili sijui inatoka inatembeatembea ni fix tu, wanaosema wameona marehemu waende tu kumuona daktari, watu wengi ni wagonjwa wana hallucinate zaidi ya watu mnavofikiri, kusema marehemu kamuongelesha hua ni story tu hakuna ukweli wowote.

Tumejazwa madudu washa toka utotoni, inabidi tusiendelee kuwajaza watoto wanaokuja wasiendeleze ujinga miaka ijayo
 
mshana jn ufahamu wangu unanipelekea kusema Roho ndio nyama yaani ni mwili, Nafsi ndio utu wa hiyo Roho, kwa maana hiyo kuna viwili na sii vitatu

"Roho na Nafsi"

Ukidhani siko sawa tutenganishie kwa maelezo ya kila kimoja.
 
Last edited by a moderator:
Mbona huwa inatokea sana tu mfano marehemu alisema nikifa nizikwe sehemu flani. Halafu nyie wanandugu mlete ujuaji mumzike mnapotaka ninyi hapo ndio mtatia akili. Kipindi flani nilisindikiza maiti kutoka Mbeya kwenda Moshi, Acha kabisa majanga yake kumbe Marehemu alishawahi kusema akifa azikwe kwenye eneo la nyumba yake ambayo ilikua Mbeya. Ilibidi mzee mmoja wa kichaga afanye mambo ndio ngoma ikakubali.
 
mshana jn ufahamu wangu unanipelekea kusema Roho ndio nyama yaani ni mwili, Nafsi ndio utu wa hiyo Roho, kwa maana hiyo kuna viwili na sii vitatu

"Roho na Nafsi"

Ukidhani siko sawa tutenganishie kwa maelezo ya kila kimoja.

Viko vitatu vinavyotengeneza ID/utambulisho wa kiumbe hai/mwanadamu! Kimoja (mwili)kinaonekana viwili nafsi na roho haionekani

1. mwili ni jumba la kubeba roho/uhai
2. roho ndio inayofanya mwili uwe na uhai
3. nafsi/kujitambua ndio huleta ufahamu kwenye mwili wenye roho

Kuna wakati nafsi inakosekana lakini mwili na roho vina endelea kuwa live, tendo la kukosa fahamu hufanya mtu kukosa kujitambua kuwa yuko wapi na anafanya nini
Kwa kiingereza ni ME, MYSELF and I
 
Last edited by a moderator:
Roho na nafsi huwa havifi bali hubaki vikizunguka huko na huko na ndio maana kwasababu haijakamilika kuwa binadamu kamili basi huitwa mzimu/mizimu
Mizimu si majini wala vinyamkera bali ni roho za watu waliokuwa na maisha yao kama sisi
Zamani tukienda kutambika tulikuwa tunaimba hivi
Taaambaa tiase nkoba, tiombe Mungu mzimu wa Saita kagone
Yaani tughani tutupe tunguli, tumuombe Mungu MZIMU wa Saita kalale
Haya ni mambo ya kimila.mizimu ilikuwepo na iliabudiwa
 
Inawezakana ikawa kweli. Siyo ya kusimuliwa nimeshuhudia kuna marehemu mmoja alikata kulala na kunyoshwa akawa kama kakaa. Mpaka watu wakaulizana jamani kuna ambae ana ubaya na marehemu hapa. Mzee mmoja akajitokea nje ndiyo marehemu akanyoshwa bila hata kutumia nguvu.
 
Back
Top Bottom