Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Wakati fulani nilikuwa mkuu wa msafara wa kumsinfikiza mrehemu tulipata hitilafu kibao. Fikiria umbali wa km 90 mnasafiri kwa masaa 12. Mpaka dereva alivyoongea na mrehemu akimuuliza kwamba hutaki tukupeleke kweni? Ndiyo safari yetu ikawa nyepesi. Kwa hiyo hayo mambo yapo.
 
Hizo ni Imani tu,nakumbuka Kuna mtanzania alifariki huku,waoshaji ni wazungu mimi nilikua mmojawapo nilienda kupeleka nguo za kuuvalisha mwili, niliwaomba nishuhudie wakimuosha na kumuandaa,hayo sijayaona kabisa ya kubembelezana.
 
Kwahiyo unadhani yanatokea kwa kila marehemu?
 
Biblia inasema Wafu hawajui neno lolote, hapo kwenye red ni imani tu lakini hakuna uhalisia. "Mhubiri 9:5 kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa. 6 Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao, imepotea yote pamoja; wala hawana sehemu tena katika jambo lo lote lililofanyika chini ya jua."
Huwa sielew mtu kutumia biblia au quran kujibu hoja ya iman nyingine bila kwanza kuelewa hata biblia au quran ni mwongozo wa imani flan. jikite upande mmoja.
 
Binafsi huwa ni mbishi kuhusu mizimu na ushirikina. Sasa juzi tu nikaenda msiba wa ndugu yetu. Mtoto wa miaka 10 wa ma mdogo ana tatizo la kuwa marehemu wa ukoo wanamuingia anazimika kwanza macho yanageuka anaongea kwa sauti ya marehem ingawa hakuwai kumwona huyo babu niliyeshuhudia siku hiyo kamuingia.alitoa maelekezo dawa flan zitolewe sehem flan humo ndan ujomban na kweli tukazikuta zimechimbiwa kitambo. Akatoa maelekezo mjomba wangu flan kwake atoe dawa flan zinamdhuru na kweli zikawepo. niliitwa wa kwanza kusikiliza mana huwa nabisha sana. Kwa hali ile nahis miaka 6 niliyosoma seminari na majibu aliyowai kunipa Father kuhusu marehem kuongea tena kupitia mwili wa mtu mwingne kuwa ni tu kumtafakar sana .... nahisi nilidanganywa.
hali ile na uhalisia uliojitokeza niliamin wakolon walituziba kuyajua yetu mengi.
 
Mkuu,kuna watu waliwahi kufungua macho kabisa kwenye jeneza..anaombwa na anafunga Mara moja!!
Hata matukio ya marehemu kukunja uso kutabasamu kugeuza sura na hata kusonya
 
Kwahiyo unadhani yanatokea kwa kila marehemu?
Naona ni huko Tz,tu,mwisho leo hiii nimejaribu kumdodosa mama mmoja kuhisu suala Hilo, akaniambia hajawahi ku experience kitu kama hiko,naye ameajiriwa kwenye funeral service homes,kila siku wanaosha na kuwa valisha maiti.
 
Huko kwenye funeral homes ni ngumu hili ni suala la kifamilia na kindugu zaidi lakini hata kama hajapata ku experience hii kitu bado haiondoi uhalisia wake....kumbuka yeye ni sehemu ndogo sana kwenye ulimwengu mzima
 
Nimeamua usiku huu nije makaburini niisome hii thread. Nasubiri kuona kitu gani kitatokea hapa wakati naisoma.
 
Hahahaaaaa Zamaulid nimecheka hadi kidogo nipaliwe nakumbuka siku ya kwanza Kupewa maiti niiweke vizuri sikulala na kwakweli sikula nyama karibia wiki 2! Ilikuwa maiti iliyochomwa moto halafu ukazimwa kabla haijateketea yote

Na kuna wakati nikakosa mchumba hivi hivi baada ya kumwambia nafanya kazi gani hakulala aliaga na hakurudi tena
Ni kitu gani huongezeka au huizunguka maiti hata ikajenga taswira ya kuogopesha ndani ya jamii wakati kabla ya hapo alikua ni mpendwa wetu na mwenzetu tuliyempenda na kuvutiwa naye?
 
Ni kitu gani huongezeka au huizunguka maiti hata ikajenga taswira ya kuogopesha ndani ya jamii wakati kabla ya hapo alikua ni mpendwa wetu na mwenzetu tuliyempenda na kuvutiwa naye?
Ni dhana tuliyojengewa tangu zamani
 
Huko kwenye funeral homes ni ngumu hili ni suala la kifamilia na kindugu zaidi lakini hata kama hajapata ku experience hii kitu bado haiondoi uhalisia wake....kumbuka yeye ni sehemu ndogo sana kwenye ulimwengu mzima
The thing is hawana concept ya hivyo vitu,kwa hiyo uenda vikawepo lakini wakawa hawavitilii maanani.
 
ata mimi nakumbuka babu yangu alipofariki nilijikuta namwambia "BABU KUBARI TUKUSAFIRISHE KWENYE NYUMBA YAKO YA MILELE SALAMA" alifariki huku dar na tulikuwa tunasafirisha kuelekea huko singida saa ya kwenda tulisafiri salama tukazika salama ila kimbembe kilitokea muda wa kurudi tuligombana kwenye gari kufika dar kila mtu akashika njia yake bila maelewano na mwenzake....
 
Back
Top Bottom