Dunia imekuwa kama kijiji kutokana na uwezo mkubwa aliounyesha mwanadamu wa kugundua hata ambavyo vilifikirika kwamba haviwezekani
Elimu na ufahamu kuhusu mwili wa mwanadamu kuanzia kuumbwa tumboni kuzaliwa hadi kufa umetafitiwa na kunyumbulishwa kwa mapana yake na wengi wamepata elimu ya juu kabisa PhD kwenye hili eneo, lakini wakashishindwa kitu kimoja tuu!!! Uwezo wa kumuita marehemu na kuongea naye
Zamani kabla ya dini za kigeni hazijaja Africa tulikuwa kwa kiasi fulani tuna uwezo wa kuwaita marehemu kwa njia ya matambiko na kuwaomba hili au lile, lakini ikumbukwe kwamba hawakuja live bali dalili na ishara kadha zilionyesha uwepo wao na kukubali au kukataa ombi husika
Tumekuwa tunaondokewa na wapendwa wetu na watu tunaowahitaji mno katika maisha yetu, tumekuwa na vipindi vigumu kabisa ambapo tunawahamu na kuwahitaji japo wajitokeze kwa dakika chache tu lakini haikuwezekana kabisa
Mfu ni mfu na hatuna uwezo wowote iwe wa kimwili au wa kiroho kuweza kumuita na kuongea naye lolote, hii ni kwakuwa roho inapotengana na mwili hakuna tena huyo MTU bali kunatokea vitu vitatu visivyoweza kuungana tena na kutengeneza kitu kimoja. vitu hivyo ni roho mwili na nafsi, vitatu hivi ndio vinatengeneza MTU nje ya hapo kuna 'mwili wake', 'roho yake' au 'nafsi yake'
Watu wamejaribu kutoa shuhuda nyingi za kutokewa na marehemu, hili linawezekana kwasababu baada ya kifo kuna roho huwa zinawayawaya duniani, zipo tu na hizi ndizo ambazo hugeuka mizimu mizuri au mibaya
Wakati mmoja tu marehemu anaweza kusikia sauti ya mwanadamu na kuitii ni pale tu anapoandaliwa kwa safari yake ya mwisho kaburini, hasa kwenye ishu ya kumsafirisha au kumvalisha nguo
Nikiwa mtu ambaye nilidili na miili ya marehemu kwa miaka mitatu mfululizo nilikutana mara nyingi tu na hizi hali, marehemu hataki dharau ubishi au kufokewa nguo hata iwe inamtosha Siku hiyo itakataa mpaka mumbembeleza
Tuna wajuaji wengi Siku hizi wanaojifanya wametokewa na marehemu fulani na kumpa maagizo Fulani hizi kwa asilimia 90 ni story tu kwakuwa hatujakuwa na uwezo wa kuwaita au wao kututokea tu na uchafu wote huu tulionao
Uzi murua kabisa ndg mshana jr,hongera na ninashukuru sana kupitia eneo hili.
NISHAKUTANA NA VINGI ILA HIKI NI CHA KARIBUNI TU.
Hapa nyumbani kwetu tulikuwa na mpangaji(mwanamke) ambaye alipanga kwa kitambo kidogo.Alikuwa akiishi na mtoto(umri kati ya miaka 13) wa ndg yake lakin baadae wakahamia kwny nyumba yao mpya.
Walipohama niliweza kukutana mara kadhaa na mama huyo na kumsalimiana nae na mara moja moja sana nilikutana na yule mtoto.
.......HISIA MBAYA.....
Siku moja asubuh kama saa tatu asubuh nilitoka nyumban kuelekea mjini nikiwaza pia nipitie nmsalim yule mama pia nkakumbuka kuwa yule mtoto sjamuona muda kidogo...hivyo nikawa na shauku ya kutaka kumwona yule mtoto,nikiwa njian hali ya ajabu ikaanza kunijia. nkaanza kutojisikia amani,kuhisi roho kama inanichomoka,mara kama kuna mtu ananifata na upepo kunizongazonga hivi(eneo hilo pia kuna majeneza yalikuwa yaktengezwa na kuuzwa)....nliendelea na safar nkafika kwa yule mama kwel nkamsalm nkapiga soga kidogo afu nkaondoka...umbali wa dakika tatu tu toka ofisini kwa yule mama nkakutana na yule mtoto moyo ulishtuka kiasi(sikujua kwa nn),nkasalim,nakumsihi ajitahid na masomo....tukaachana yy akielekea ofisini kwa yule mama....
.......MSIBA SIKU YA PILI YAKE....
Asubuhi saa 2 tulipokea habar za msiba za mtoto yule maana tairi la semitrela lilichomoka na kumkuta yy wakati akivuka barabara anavoenda shule...ni yy tu ndo lilimkuta tairi lile...
......SIKU TATU BAADAE...
Siku hiyo niliota ndoto nko nyumbani pale ndani ya banda la kuku.Nilitazama nje ya banda hilo nkamwona mtoto yule,nakumbuka sikuwa nasikia sauti ya kitu chochote...ulikuwa ni utulivu mwanana sana...mtoto yule alikuwa akitabasam.(moyoni mwangu nkakumbuka kuwa yule ni alishafariki).Sjui nilijuaje ila tu nakumbuka nilimwambia kimoyonimoyoni UPUMZIKE KWA AMANI,naye alitikisa kichwa kwa ishara ya kukubali..akapotea...
SIJAMUOTA TENA MPAKA LEO.
Mungu ampumzishe kwa amani.Amen