Uwezo wa wataalam wa Bioteknolojia na Microbiolojia

Uwezo wa wataalam wa Bioteknolojia na Microbiolojia

Mkuu nchi hii wanasayansi hawatambuliki
MD's wamekuwa wao ndio wanajua kila kitu... nakumbuka nilimsikiliza Janabi akijikoroga pamoja na lile kind la MDS wa ITV..
Hawajui vitu na hawataki kukubaliana kuwa hiyo sio filed yao...
Hii unachanganya na waandishi vilaza pia
 
Original Thread by maroon 7

Wakuu nimekutana na habari hii kutoka gazeti la The citizen kuhusu maabara ya kisasa iliyogharimu zaidi ya Tsh 2 Billion kwa ufadhili kutoka Uturuki lakini cha kusikitisha inamiaka karibu miwili eti bila matumizi na badala yake sampuli zinapelekwa India licha ya maabara hiyo kutoa majibu sawasawa na yale ya India.

Tena bila aibu viongozi wa Muhimbili wanasema kabisa sample kupelekwa kwenye hiyo maabara na nyingine inapelekwa India na majibu kurudi yaleyale. Mtaalam kutoka Uturuki Prof Fatmahan Atalar ambae anasimamia mradi huo kuhakikisha wataalamu wetu wanajua kutumia maabara hiyo amelalamika hali ya kushangaza ya wataalamu wetu kukwepa kabisa kujifunza na kutumia maabara hiyo achilia mbali kupeleka tu sampuli hapo licha za juhudi zake binafsi kuzunguka idara zote kuwahamasisha lakini wote wanakacha.

Cha kushangaza zaidi hata reagents tu kuhudumia hiyo maabara hawataki kununua hali iliyopelekea mtaalam huyo kutoka Uturuki kutumia pesa yake binafsi kiasi cha shilingi milioni 140 ambazo aliahidiwa kurudishiwa lakini kapigwa changa la macho.
Maabara hiyo ya aina yake inaweza kuokoa maisha ya watu wengi afrika mashariki na kati kwa mujibu wa Prof huyo.

Waziri wa afya anapaswa kutoa tamko juu ya nini hasa kimepelekea hii hali na kwanini baada ya The citizen kuanika hii ndio waseme sasa wataanza kuitumia?

My take
Shida kubwa madaktari huwa hawapendi kujifunza zaidi na huwa wanafikiri kuwa wao ni superior kuliko wengine wakati hizi kada zinachangamana na kusaidiana ili kuleta matokeo mazuri

Nadeclare Interest kuwa Mimi ni daktari nimefanya MD MUHAS ila pia nimefanya Msc hapo UDSM Department of Molecular biology and Biotechnology. Magonjwa mengi sasa ili uweze kubaini ni kimelea gani kasababisha lazima utumie advanced biotechnological tools. Sasa iweje wizara ishindwe kuwathamini hawa wataalam au kisa wamejaza washauri ambao ni ma MD tu?

Sh2 billion lab stands idle for nearly 2 years
 
Nimejikuta napata hasira tu hapa.Kwamba watu wanafatwa wakasome wanakwepa.
Wachukue vijana toka A'LEVEL na vyuo vya kati huwa wako ambitious mno.
Ukichukua hawa walio kazini akiangalia salary,posho,safari na projects anazopata haoni kwa nini akasome maana kipato kinamtosha.
 
Kada ya afya na sayansi hata kada zingine haziko static zinabadilika na kuna vitu vinavyozuka na vinahitaji fikra mpya. Ninashangaa mtaalam asiyependa kujinoa upya. Vipi wale waliokuwa wanajua stomach ulcers zinasababishwa na stress? Je ni kweli na siyo bacteria? Vipi hadi leo njia nzuri ya kubainia progression ya HIV/AIDS ni CD4 cell count au viral load? Vipi RDT kama MRDT zilikuwepo wakati madaktari / wataalam wa maabara wanasoma? Wathink out of the box wasiwe na mawazo finyu, daktari mzuri ni yule anayependa kusoma.
Nenda MOI wanautaratibu mzuri wa kila siku kufanya presentation ya cases ili kujinoa.

Hao vijana wa A LEVEL hawataweza maana kunahitajika strong biomedical / medical foundation
 
Aseeeh inasikitisha...Afu hili suala la kuweka wakuu wa hizo Idara MDs huwa linaukakasi hivi...

Typed Using KIDOLE
 
Nimejikuta napata hasira tu hapa.Kwamba watu wanafatwa wakasome wanakwepa.
Wachukue vijana toka A'LEVEL na vyuo vya kati huwa wako ambitious mno.
Ukichukua hawa walio kazini akiangalia salary,posho,safari na projects anazopata haoni kwa nini akasome maana kipato kinamtosha.
Usione watu wanaandika kirahisi rahisi tu ukachukulia hayo masomo ni rahisi kama vile kula popcorn,

Hayo masomo ya molecular biology mziki wake sio wakitoto, madaktari wanajua igumu wake isitoshe wengi wana stress na ugumu wa maisha kutokana na makato kuwa makubwa mshahara kuwa mdogo hapo wanaona why aendelee kuumiza kichwa ilihali hafaidiki kiuchumi??

Ukitaka madaktari wetu wawe deep wasome hiyo molecular biology inalazimu kuongeza miaka ya masomo..kwa usawa huu wa ajira chache nani atakubali kukomaa nayo.

All in all serikali ingewakutanisha hawa watu wa hizi kada kwa pamoja wakajadili ni namna gani wataleta mabadiliko chanya ikiwemo hiyo ya kufanya qualitative research nzito nzito

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hongera kwa bandiko murua

Niliwah kupita wizara ya mifugo katika utafiti fulan na shirika fulan miaka kama mi4 iliyopita wale jamaa wanamaabara yao inaitwa CIDB Yaani center for infectious diseases and biotechnology vijana wengi wanauelewa Mkubwa juu ya hili la MOLECULAR BIOLOGY NA MICROBIOLOGY na wametatua matatzo mengi kipitia hyo technology sijajua upande Wa afya wanakwama wapi kuitambua hii kada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo field ili uzifaidi unatakiwa uwe mbunifu yaani utengeneze bio-products, tofauti na hapo utaziona sio nzuri
 
Usione watu wanaandika kirahisi rahisi tu ukachukulia hayo masomo ni rahisi kama vile kula popcorn,

Hayo masomo ya molecular biology mziki wake sio wakitoto, madaktari wanajua igumu wake isitoshe wengi wana stress na ugumu wa maisha kutokana na makato kuwa makubwa mshahara kuwa mdogo hapo wanaona why aendelee kuumiza kichwa ilihali hafaidiki kiuchumi??

Ukitaka madaktari wetu wawe deep wasome hiyo molecular biology inalazimu kuongeza miaka ya masomo..kwa usawa huu wa ajira chache nani atakubali kukomaa nayo.

All in all serikali ingewakutanisha hawa watu wa hizi kada kwa pamoja wakajadili ni namna gani wataleta mabadiliko chanya ikiwemo hiyo ya kufanya qualitative research nzito nzito

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaumiza kichwa unaishia kuburuzwa kazini kwa maslahi kiduchu, majungu, fitina juu na kurogwa. Kuna watu wana PhD huku makazini wanatamani aache kazi akafungue genge la nyanya vituko anavyokutana navyo huko maofisini, weee acha tu..
 
Leo nimeona msomi ameandika.Nimekukubali mkuu.Ninaheshimu sana hoja zako za msingi kabisa.

Wasomi wengi wapo kujisifia vyeti tu ila kiuhalisia hawana kitu kichwani.Vingi waliviacha kwenye karatasi za mtihani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu muhimu wizara ya Afya ingewaangalia,Wakemia,molecular biology na biotechnologist hawa watu ni muhimu sana,yani nchi yetu kuna wataalamu wengi halafu hatuwatumii vizuri.
Hahaha unadhani wakiajiriwa na wizara ya afya watafanya kazi wapi?!
Wanaohitajika wameshaajiriwa, kwa mkemia mkuu wapo,kule zamani ilikuwa TFDA wapo, pale TFNC walikuwepo sijui kwa sasa unadhani umuhimu wao huko wapi, hay aliyolist au outcome ya hayo aliyolist ?!
Mimi namshauri mleta mada kama anataka kuwa MD akaombe chuoni asome, Tanzania hakuna equivalent system.
 
This is too low.
Kama wewe ni daktari,unasikitisha
Hahaha unadhani wakiajiriwa na wizara ya afya watafanya kazi wapi?!
Wanaohitajika wameshaajiriwa, kwa mkemia mkuu wapo,kule zamani ilikuwa TFDA wapo, pale TFNC walikuwepo sijui kwa sasa unadhani umuhimu wao huko wapi, hay aliyolist au outcome ya hayo aliyolist ?!
Mimi namshauri mleta mada kama anataka kuwa MD akaombe chuoni asome, Tanzania hakuna equivalent system.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko clear kbsa science is wide
Kuna mdau wa JF alisema hawawezi tengeneza dawa. Ok

Nitaelekeza kwa mifano
Hakuna pharmaceutical compound inayoweza tumika kwenye mwili bila kua na knowledge ya drug target (receptors, ligands, Au microbial cellular parts kama cell walls, plasma membrane, Nucleus, au nucleic acid target) na mtaalamu wa kusoma hizo drug targets ni MOLECULAR biologist na moja ya njia zinazotumika kusoma hizo target ni Nuclear magnet resonance imaging (NMR), au X-ray crystallography for crystalline samples.

Kuna field ya biomedicine inaitwa bioinformatics mtu wa medical lab hasomi at all wala Daktari, mtu wa Biotechnology au Microbiology anasoma. Na hii ni kitovu cha medical research hasa katika kutafiti novel strain kwa computer simulations. JE WAJUA? hadi kufahamu kua SARS cov -2 (Corona virus 2) ametoka kundi la Virus wanaosababisha SARS na MERS ni application ya Molecular biology techniques kama Sequencing pamoja na Computational biology (Bioinformatics)? Mtu wa medical lab akiambiwa afanye hili zoezi dogo tu hatoweza kwa sababu hajaandaliwa kufanya hizo kazi.
How can you find out a viral or bacterial mutations kama haujui kitu kuhusu BIOINFORMATICS?

Medical personnel (medical labs, MDs) hawafanyi research za Molecular levels wanafanya tafiti za epidemiology, statistical based research, wakifanya experimental basi mwisho wao ni Cell Biolog kwa sababu hawasomi sayansi to the Molecular level.

How can you produce a Vaccine pasipo kujua Bioinformatics? Pasipo na knowledge ya Genetic engineering/Recombinant DNA technology? Pasipo na knowledge ya downstream processing? The same thing to Monoclonal antibodies, Insulin, enzymes na antibiotics.

Wapo madaktari wachache Tanzania waelewa sana na hao nadiliki kuwaita wanasayansi makini ukimpa facts za kisayansi kama hizi moja kwa moja anajifunza kitu na kutambua kua Biotechnology ni msaada mkubwa kwake ili akamilishe matibabu.

Wapo wasiotaka kukubali, I call them SELFISH scientists japo wanatumia immunosuppressant drugs eg. Alemtuzimab wakifanya solid organ transplantation, still hawataki kujua kuhusu nani anazalisha do you think it's such an easy task to target Cytokine receptors?? Like IL6R? Au akiprescribe dawa akaandika kutwa mara tatu anaona yeye ndie mgunduzi kwa sababu ndie aliemalizia kwa kumtibu mgonjwa?

Mbona sisi wanasayansi (Researchers) tunakili hatuwezi fanya surgery? , mbona tunakili hatuwezi Fanya consultations na wagonjwa?, Mbona tunakili haturuhusiwi kufanya prescription za madawa japo kua tunayatengeneza sisi wenyewe na tunayajua kuliko madaktari?
Jibu ni simple Tu tunaheshimu nafasi ya kila mmoja na hiyo ndio sayansi ya kweli. Maana sisi sio madaktari so hatuwezi deal na wagonjwa ila we can deal with samples.

Tatizo watu wengi hawajui vitu na hawaamini kua sayansi inaendelea wakisoma medical labs au Md wanahisi wamemaliza which is not true, sayansi inaendelea na iko deep.
Mtu wa biotechnology anasoma kuja kua researcher na sio kwaajili ya kufanya qualitative (negative or positive) and quantitative (how much) laboratory measurements.

Ntatoa tofauti ndogo ya coverage katika curriculum zetu.

Medical Lab technologists na MD wanasoma
Microbiology pamoja na immunology

Biotechnology wanasoma kozi sita separate ili wawe deep zaidi.

Medical bacteriology as a course
Medical Virology as a course
Medical mycology as a course
Parasitology as a course
Entomology as a course hapa Medical lab wanamix parasitology na entomology.
Biotechnology wanasoma Molecular virology, (Virology at Molecular Level) MD wala medical lab hawasomi molecular virology.

Huu ni uchambuzi wa microbiology Tu hizo courses unawezaje kua deep kwa kumix zote tena unasoma semester moja.

Immunology
Mtu wa biotechnology anasoma immunology yote.
Immunology 1 (Introduction to Immunology)
Immunology 2 (Molecular immunology)
Immunology 3 (Clinical immunology)
Tena usiombe ukafundishwa na PHD holder mmoja yuko UDSM anaitwa Dr. Victor Makene, haachi kitu hata nukta.
Do you know kama antibody molecule ambayo wewe unaishia kutambua kua ni Y shaped molecule kuna watu wanaisoma wiki 3? Uliwahi sikia kuhusu complementary determining regions (CDR)?

Kuna watu hawajui hata kirefu cha CD4 na wengine wanajua CD4 Ni cell ooooh My God. Embu tuacheni siasa tufanyeni SAYANSI.

Nina swali moja la kitaalamu kwa medical personnel ngazi yeyote ile hata kama ni professor.

Duniani kuna watu hawawezi kupata maambukizi ya HIV kutokana na kua na mutation kwenye CCR5 (Chemokine receptor 5) kitalamu inaitwa Delta 32 mutation, na ilimponya bwana timothy Brown aliekua intended kutibiwa cancer by Bone marrow transplantation method.

Swali. Unawezaje kutumia Clustered regularly interspaced palindromic repeats (CRISPR) System (Natural bacterial adaptive immune system used to fight phages) to introduce induced mutation ili Duniani sasa watu wawe immune to HIV? Nieleze na side effects zake.
Hili swali sijajitungia Tu ni project inayoendelea Kwa nchi za wenzetu waelewa wanaotambua mchango wa scientific research acha sisi Tanzania tuendelee kubishana nani bora zaidi.
Tuma jibu lako kwenye email #melchscience@gmail.com
Am pretty sure kama hujasoma Molecular biology hili ni zoezi zito sana.

Tunaendelea na coverage
Biochemistry 1
Biochemistry 2
Biochemistry 3

Molecular biology 1
Molecular biology 2
Molecular cell biology
Molecular developmental biology

Organic Chemistry 1
Organic Chemistry 2
Analytical chemistry

Biostatistics 1 &2
Bioinformatics 1 & 2

Applied Physics in Biology
Humu utasoma principles za vifaa vya laboratory mfano, Microscope, centrifuge, NMR, electronics etc

Watu wa medical lab Wanafanya antimicrobial sensitivity tests (kwa microbial culture technique) na bado hawataki graduate wa Bsc in microbiology afanye hii kazi #SELFISHNES

Wanafanya PCR, molecular biology tool ilogunduliwa na Biochemist Dr. Karry Mullis 1944. Lakini hawamtaki graduate wa Molecular biology afanye PCR. #SELFISHNESS

Hausomi downstream processing unawezaje zalisha enzymes au other proteins for medical use??

Tanzania ifike wakati tukubaliane katika sayansi kila mmoja anaumuhimu kwenye eneo lake. TUACHE UPOTOSHAJI wa jamii, wengine wanadiliki kutanganya kua Biotechnology ni kwajili ya viwanda tu, wengine wanapotosha wakisema wataalamu wa biotechnology ni watu wa Mafuta na Gesi are they petroleum geologists?

Nisikilize kwa makini.
Biotechnology Ina makundi manne White biotech(industrial biotechnology)
Red /Medical biotechnology
Green /Agricultural biotechnology

So they can do a lot kila eneo.
Watu wa MD, na Medical labs wameandaliwa kwaajili ya Clinical environment, kutoa huduma kwa wagonjwa.
Bio technologists and other scientists kama microbiologist wameamdaliwa kwaajili ya research laboratories huko watafanya uvumbuzi utakao kua applied na medical personnel. Mbinu zote za upimaji magonjwa maabara zinatokea kwenye biotechnology. Watu wa Medical lab wanatumia monoclonal antibodies kupima blood group lakini maskini ya Mungu hawajui nani anazalisha Hizo antibodies

Kwa ufupi hiyo ni hybridoma technology (Cancer cell + normal cell fusion) najua sio rahisi kuelewa lakini ifike wakati mjue mwanasayansi makini sio SELFISH, Mwanasayansi makini anathamini mchango wa mwenzie kama ambavyo watu wa biotechnology wanavowategemea MD na Medical labs au Pharmacists kutibu wagonjwa.
THINK BIG THINK BIG THINK BIG

Na huu ujinga bado upo Tanzania Tu nenda US, nenda China, India, Italy nenda Kenya au fuatilia google utagundua Biotechnology ndio kitovu cha Life Sciences reseach. Bill gates aliwahi ulizwa akirudi shule Leo ataamua kusoma nini akajibu Biotechnology and computer science coz ndo fields zinazokua kwa kasi sana. TUBADILIKE TANZANIA TUKO NYUMA SANA KWA SABABU ZA UJINGA TU NA UBINAFSI.

Swali TANZANIA IKIPIGWA NA BIOLOGICAL WEAPON ya virus au engineered bacteria MD au MEDICAL LAB scientist ataanzia wapi ikiwa hajui hata kufanya DNA extraction?

Ikiwa hajui hata Bioinformatics (Computational biology) hajui chochote kuhusu Nucleic acid Sequencing?

Ikiwa hajui chochote kuhusu Downstream processing anawezaje hata purify antibodies?

Ikiwa hajui chochote kubusu NMR
Au Mass spectroscopy anawezaje hata kutambua poisonous proteins?

Guys kila mtu aheshimu profession ya mwenzie. Sayansi hakuna anaeijua yote ndo mana kuna specialization. Sasa Tanzania mtu akisoma tu medical school anaona mtu alietokea UDSM au SUA hajui kitu kumzidi yeye huo ni ufinyu wa fikra. Sayansi is wide.

Kauli yangu ya mwisho:

TUTHAMINIANE HII DUNIA HATUISHI MILELE TUACHE UBINAFSI, UNASABABU IPI YA KUPINGA BIOTECHNOLOGY ISIWE CHINI YA WIZARA YA AFYA? IKIWA HAPO ULIPO UNASUBIRI CHANJO (VACCINE) YA COVID 19 KUTOKA KWA WESTERN BIOTECHNOLOGICAL CAMPANIES?

Prepared by Modern scientist.
Contact: 0758406251
Email #melchscience@gmail.com
Instagram scientist_melch

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kada ya afya na sayansi hata kada zingine haziko static zinabadilika na kuna vitu vinavyozuka na vinahitaji fikra mpya. Ninashangaa mtaalam asiyependa kujinoa upya. Vipi wale waliokuwa wanajua stomach ulcers zinasababishwa na stress? Je ni kweli na siyo bacteria? Vipi hadi leo njia nzuri ya kubainia progression ya HIV/AIDS ni CD4 cell count au viral load? Vipi RDT kama MRDT zilikuwepo wakati madaktari / wataalam wa maabara wanasoma? Wathink out of the box wasiwe na mawazo finyu, daktari mzuri ni yule anayependa kusoma.
Nenda MOI wanautaratibu mzuri wa kila siku kufanya presentation ya cases ili kujinoa.

Hao vijana wa A LEVEL hawataweza maana kunahitajika strong biomedical / medical foundation
Uko sahihi kabisa. Kuhusu hao A'LEVEL nilitaka wapewe hyo foundation kisha wapande ngazi taratibu.
 
Kelele nyingi hamna any logical point hapo ndugu researcher.. au kwa sababu nyie bio technologist hamruhusiwi kufanya kazi kwenye hospitali za binadamu ndo kinachokusumbua? Usiringe sana na hiyo biotechnology yako. Hao wote uliowataja hapo unaosema hawajui chochote wanaweza wakaenda kupiga masters ya Microbiology molecular and immunology (MMIU ) miaka miwili tu na wakaweza kufanya research. Take several seats.

Sent From Galaxy S9
 
Umesema kwamba
Watu wa medical lab Wanafanya antimicrobial sensitivity tests (kwa microbial culture technique) na bado hawataki graduate wa Bsc in microbiology afanye hii kazi #SELFISHNES.

Sidhani kwamba kuna mtaalamu yoyote wa maabara atazuia mtu kufanya kile kitu alichobobea ila hospitali zetu zinataka kuajiri mtu aliyesomea medical laboratory science kwa sababu mtu huyo atakua amesoma;

Parasitology & entomology
Histopathology
Microbiology & immunology
Clinical chemistry
Hematology and blood transfusion
Serological tests
Quality systems in lab

Hivyo hospitali zinaona haziwezi kuajiri mtu aliyebobea sehemu moja tu ya Bsc microbiology wakati ikichukua mtu aliyesomea Bachelor of MLS, hiyo microbiology iko ndani yake ingawa sio deep kama ya aliyesomea Bsc microbiology ila iko sufficient enough kwa mahitaji ya kutibu wagonjwa mahospitalini. Na hospitali zinaajiri hivyo kwa sababu mtu huyo unaweza ukampanga afanye kazi microbiology ikitokea dept nyingine mfano hematology &BT basi unampeleka na anapiga kazi kwa sababu amecover vitu vyote.

Mgonjwa anakuja baada ya vipimo labda amehisiwa atakua na bacteria kwenye damu hivyo daktari atarequest blood culture ili kuisolate & kupata drug of choice ya kumtibu mgonjwa na after few days culture ikiota itafanyiwa sensitivity test then majibu yanatoka. Haijitajiki kufanya extraction ya molecular compounds ndani ya bacteria ili kupata dawa ya kumtibu mgonjwa kwa hospital settings kwa sababu tayari kuna ready made disks za dawa.

Fields zote zinaheshimu mchango wa taaluma nyingine ndio maana PCR aligundua Karry mullis inatumiwa mpaka leo mahospitalini.

Biotechnology inaweza kuwa chini ya wizara ya afya ila haiwezi kuwa applicable kwenye maabara za hospitalini labda kwa zile chache sana zenye vitengo vya molecular biology ila hizi nyingi za kwetu sidhani, inakua applicable kwenye research labs bahati mbaya research labs hapa nchini ziko chache sana .

Nakubaliana na wewe ulivyosema 'Mtu wa biotechnology anasoma kuja kua researcher na sio kwaajili ya kufanya qualitative (negative or positive) and quantitative (how much) laboratory measurements'

kazi nyingi za maabara za hospitalini ni qualitative (mfano RDT kuonyesha pos/neg) & quantitative (mfano malaria parasite quantification, hormone, electrolyte levels, n.k.)
Bottom line is mtu yeyote hawezi kufanya kazi na binadamu ( hospitali etc) kama hana foundation course ya Anatomy. Hapo ndo hao biotechnologists na microbiologist wa UD na SUA wanapofeli. Simple as that

Sent From Galaxy S9
 
Back
Top Bottom