Uwezo wa wataalam wa Bioteknolojia na Microbiolojia

Mkuu nchi hii wanasayansi hawatambuliki
MD's wamekuwa wao ndio wanajua kila kitu... nakumbuka nilimsikiliza Janabi akijikoroga pamoja na lile kind la MDS wa ITV..
Hawajui vitu na hawataki kukubaliana kuwa hiyo sio filed yao...
Hii unachanganya na waandishi vilaza pia
 
Original Thread by maroon 7

Wakuu nimekutana na habari hii kutoka gazeti la The citizen kuhusu maabara ya kisasa iliyogharimu zaidi ya Tsh 2 Billion kwa ufadhili kutoka Uturuki lakini cha kusikitisha inamiaka karibu miwili eti bila matumizi na badala yake sampuli zinapelekwa India licha ya maabara hiyo kutoa majibu sawasawa na yale ya India.

Tena bila aibu viongozi wa Muhimbili wanasema kabisa sample kupelekwa kwenye hiyo maabara na nyingine inapelekwa India na majibu kurudi yaleyale. Mtaalam kutoka Uturuki Prof Fatmahan Atalar ambae anasimamia mradi huo kuhakikisha wataalamu wetu wanajua kutumia maabara hiyo amelalamika hali ya kushangaza ya wataalamu wetu kukwepa kabisa kujifunza na kutumia maabara hiyo achilia mbali kupeleka tu sampuli hapo licha za juhudi zake binafsi kuzunguka idara zote kuwahamasisha lakini wote wanakacha.

Cha kushangaza zaidi hata reagents tu kuhudumia hiyo maabara hawataki kununua hali iliyopelekea mtaalam huyo kutoka Uturuki kutumia pesa yake binafsi kiasi cha shilingi milioni 140 ambazo aliahidiwa kurudishiwa lakini kapigwa changa la macho.
Maabara hiyo ya aina yake inaweza kuokoa maisha ya watu wengi afrika mashariki na kati kwa mujibu wa Prof huyo.

Waziri wa afya anapaswa kutoa tamko juu ya nini hasa kimepelekea hii hali na kwanini baada ya The citizen kuanika hii ndio waseme sasa wataanza kuitumia?

My take
Shida kubwa madaktari huwa hawapendi kujifunza zaidi na huwa wanafikiri kuwa wao ni superior kuliko wengine wakati hizi kada zinachangamana na kusaidiana ili kuleta matokeo mazuri

Nadeclare Interest kuwa Mimi ni daktari nimefanya MD MUHAS ila pia nimefanya Msc hapo UDSM Department of Molecular biology and Biotechnology. Magonjwa mengi sasa ili uweze kubaini ni kimelea gani kasababisha lazima utumie advanced biotechnological tools. Sasa iweje wizara ishindwe kuwathamini hawa wataalam au kisa wamejaza washauri ambao ni ma MD tu?

Sh2 billion lab stands idle for nearly 2 years
 
Nimejikuta napata hasira tu hapa.Kwamba watu wanafatwa wakasome wanakwepa.
Wachukue vijana toka A'LEVEL na vyuo vya kati huwa wako ambitious mno.
Ukichukua hawa walio kazini akiangalia salary,posho,safari na projects anazopata haoni kwa nini akasome maana kipato kinamtosha.
 
Kada ya afya na sayansi hata kada zingine haziko static zinabadilika na kuna vitu vinavyozuka na vinahitaji fikra mpya. Ninashangaa mtaalam asiyependa kujinoa upya. Vipi wale waliokuwa wanajua stomach ulcers zinasababishwa na stress? Je ni kweli na siyo bacteria? Vipi hadi leo njia nzuri ya kubainia progression ya HIV/AIDS ni CD4 cell count au viral load? Vipi RDT kama MRDT zilikuwepo wakati madaktari / wataalam wa maabara wanasoma? Wathink out of the box wasiwe na mawazo finyu, daktari mzuri ni yule anayependa kusoma.
Nenda MOI wanautaratibu mzuri wa kila siku kufanya presentation ya cases ili kujinoa.

Hao vijana wa A LEVEL hawataweza maana kunahitajika strong biomedical / medical foundation
 
Aseeeh inasikitisha...Afu hili suala la kuweka wakuu wa hizo Idara MDs huwa linaukakasi hivi...

Typed Using KIDOLE
 
Usione watu wanaandika kirahisi rahisi tu ukachukulia hayo masomo ni rahisi kama vile kula popcorn,

Hayo masomo ya molecular biology mziki wake sio wakitoto, madaktari wanajua igumu wake isitoshe wengi wana stress na ugumu wa maisha kutokana na makato kuwa makubwa mshahara kuwa mdogo hapo wanaona why aendelee kuumiza kichwa ilihali hafaidiki kiuchumi??

Ukitaka madaktari wetu wawe deep wasome hiyo molecular biology inalazimu kuongeza miaka ya masomo..kwa usawa huu wa ajira chache nani atakubali kukomaa nayo.

All in all serikali ingewakutanisha hawa watu wa hizi kada kwa pamoja wakajadili ni namna gani wataleta mabadiliko chanya ikiwemo hiyo ya kufanya qualitative research nzito nzito

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hongera kwa bandiko murua

Niliwah kupita wizara ya mifugo katika utafiti fulan na shirika fulan miaka kama mi4 iliyopita wale jamaa wanamaabara yao inaitwa CIDB Yaani center for infectious diseases and biotechnology vijana wengi wanauelewa Mkubwa juu ya hili la MOLECULAR BIOLOGY NA MICROBIOLOGY na wametatua matatzo mengi kipitia hyo technology sijajua upande Wa afya wanakwama wapi kuitambua hii kada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo field ili uzifaidi unatakiwa uwe mbunifu yaani utengeneze bio-products, tofauti na hapo utaziona sio nzuri
 
Unaumiza kichwa unaishia kuburuzwa kazini kwa maslahi kiduchu, majungu, fitina juu na kurogwa. Kuna watu wana PhD huku makazini wanatamani aache kazi akafungue genge la nyanya vituko anavyokutana navyo huko maofisini, weee acha tu..
 
Leo nimeona msomi ameandika.Nimekukubali mkuu.Ninaheshimu sana hoja zako za msingi kabisa.

Wasomi wengi wapo kujisifia vyeti tu ila kiuhalisia hawana kitu kichwani.Vingi waliviacha kwenye karatasi za mtihani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna watu muhimu wizara ya Afya ingewaangalia,Wakemia,molecular biology na biotechnologist hawa watu ni muhimu sana,yani nchi yetu kuna wataalamu wengi halafu hatuwatumii vizuri.
Hahaha unadhani wakiajiriwa na wizara ya afya watafanya kazi wapi?!
Wanaohitajika wameshaajiriwa, kwa mkemia mkuu wapo,kule zamani ilikuwa TFDA wapo, pale TFNC walikuwepo sijui kwa sasa unadhani umuhimu wao huko wapi, hay aliyolist au outcome ya hayo aliyolist ?!
Mimi namshauri mleta mada kama anataka kuwa MD akaombe chuoni asome, Tanzania hakuna equivalent system.
 
This is too low.
Kama wewe ni daktari,unasikitisha
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko clear kbsa science is wide
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi kabisa. Kuhusu hao A'LEVEL nilitaka wapewe hyo foundation kisha wapande ngazi taratibu.
 
Kelele nyingi hamna any logical point hapo ndugu researcher.. au kwa sababu nyie bio technologist hamruhusiwi kufanya kazi kwenye hospitali za binadamu ndo kinachokusumbua? Usiringe sana na hiyo biotechnology yako. Hao wote uliowataja hapo unaosema hawajui chochote wanaweza wakaenda kupiga masters ya Microbiology molecular and immunology (MMIU ) miaka miwili tu na wakaweza kufanya research. Take several seats.

Sent From Galaxy S9
 
Bottom line is mtu yeyote hawezi kufanya kazi na binadamu ( hospitali etc) kama hana foundation course ya Anatomy. Hapo ndo hao biotechnologists na microbiologist wa UD na SUA wanapofeli. Simple as that

Sent From Galaxy S9
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…