Anahitaji darasa kubwaKwa bwana johnthebaptist kwake yeye, mtu ambaye hajapita jesho lolote (Mgambo, JKT, Magereza, JWTZ, Police, Uhamiaji etc) hapa Tanzania, hawezi kuwa mzalendo..!! Huku ni kulishana matango pori
Ndio nimekupa mfano wa Zitto Kabwe, Dr Mwigullu Nchemba na Halima MdeeSasa niwe nimezaliwa miaka hiyo nisiende?
By the way, wale ambao hawakupita system za shule na JKT inamaana hawawezi kuwa wazalenda? Waza hili, wote mnasoma darasa moja lakini mmoja anakuwa wa kwanza na mwingine anakuwa wa mwisho..!!
Unachemka haswaNdio nimekupa mfano wa Zitto Kabwe, Dr Mwigullu Nchemba na Halima Mdee
Mzalendo atajiongeza tu ili ajikute jeshini vinginevyo huyo ni mfia itikadi tu
Narudia tena hakuna Uzalendo Bila jeshi
Pale Kenya kwa mfano kilimo cha Uzalendo ni kama Babu au baba Yako alipigania Uhuru basi unafaidi matunda ya Urithi
Uzalendo ni mbinu inayotumiwa na wanasiasa waovu wakiwatisha waache kuhoji maovu yao, wao huwaambia wananchi wawe wazalendo kwa nchi yao huku wao wakijitoa kwenye uzalendo huo! Matokeo ni viongozi kuwa matajiri na kepeana madaraka na familia na ndugu zao, ukihoji unaambiwa wewe si mzalendo, funga domo lako.Habari za Jumapili wananchi wenzangu, nimekuwa nikijiuliza maana halisi ya uzalendo.
Tumekuwa tukisikia viongozi mbalimbali wakisisitiza wananchi kuwa wazalendo, na wakati mwingine wakilalamikia kinachoitwa "kupungua kwa uzalendo."
Kwakuwa JF ni home of Great thinkers iwapendeze kunijibu, je uzalendo ni nini haswa?
a) Je, uzalendo ni kuvaa tai yenye bendera ya taifa?
b) Au uzalendo ni kuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi?
c) Je, ni mambo yapi hayapaswi kufanywa na mzalendo?
d) Je, mzalendo wa taifa letu ana haki zipi?
e) Au uzalendo ni kuzishabikia timu zetu katika mashindano ya kimataifa?
f) Je, uzalendo wetu unapimwaje?
g) Viongozi wetu wanaohubiri uzalendo, wanakidhi vigezo vya kuitwa wazalendo??
Nawakaribisha nipate kufahamishwa kwa kina maana halisi ya uzalendo na mzalendo.
Mtu anaogopa hata mafunzo ya mgambo anakuwaje mzalendo bwashee?Kwa bwana johnthebaptist kwake yeye, mtu ambaye hajapita jesho lolote (Mgambo, JKT, Magereza, JWTZ, Police, Uhamiaji etc) hapa Tanzania, hawezi kuwa mzalendo..!! Huku ni kulishana matango pori
Kwahiyo wanatupumbaza kwa kutuita wazalendo au siyo?Uzalendo ni mbinu inayotumiwa na wanasiasa waovu wakiwatisha waache kuhoji maovu yao, wao huwaambia wananchi wawe wazalendo kwa nchi yao huku wao wakijitoa kwenye uzalendo huo! Matokeo ni viongozi kuwa matajiri na kepeana madaraka na familia na ndugu zao, ukihoji unaambiwa wewe si mzalendo, funga domo lako.
Muulize Mmawia wa hapo Ufipa namna alivyoshiriki Vita ya Kagera ndio utawajua WazalendoUnachemka haswa
Wanajeshi kwa maana jwtz ni zaidi ya wazalendo kwa maana ya mafunzo na wajibu wao kwa taifa.Ingawa wapo wanaokwenda kinyume na matakwa ya kazi. Kwa sababu moja ya majukumu yao ni kutoa uhai wao kwa ajiri ya kulinda mipaka ya nchi yao. Hivyo mtu kutoa uhai wake kwa ajiri ya nchi yake ni zaidi ya uzalendoKwahiyo wazalendo wapo jeshini tu..!!??
Ndiyo raha yao ukiifurahia sifa hiyo, matokeo ni nchi kutoendelea miaka na miaka.Kwahiyo wanatupumbaza kwa kutuita wazalendo au siyo?
Ahsante sanaWanajeshi kwa maana jwtz ni zaidi ya wazalendo kwa maana ya mafunzo na wajibu wao kwa taifa.Ingawa wapo wanaokwenda kinyume na matakwa ya kazi. Kwa sababu moja ya majukumu yao ni kutoa uhai wao kwa ajiri ya kulinda mipaka ya nchi yao. Hivyo mtu kutoa uhai wake kwa ajiri ya nchi yake ni zaidi ya uzalendo
Hasa wale wanaoenda 'frontline'; wako tayari kufa kwa ajili ya nchi.Kwahiyo wazalendo wapo jeshini tu..!!??