Hbr wapendwa
Nimekuwa nikiona jitihada zinazofanyika kurudisha umoja, ushirikiano na upendo miongoni mwa Watanzania na kwa nchi yao.
Ni jambo zuri na lenye kuhitajika sana.Kinachonipa shida ni
Njia tunazozitumia ktk ujenzi mpya wa uzalendo.
Uzalendo ni zao la hamasa.Hamasa hutokana na kujifunza na kutenda.
Hebu Turejee nyuma na kuona jinsi ya hatua za awali za Mwl ktk kujenga uzalendo.
Kwanza
Aliondoa uasili kwa vijana wadogo.
Elimu ilitumika kuwakusanya na kuwajenga ktk maadili ya Taifa. Na ndio sababu ya uwepo wa shule za bweni zilizowakusanya vijana wa maeneo mbalimbali ktk Tanzania na kufunzwa maadili na kuishi pamoja.
Pili
Kufunzwa kazi nje ya masomo. Kama vile ufugaji na kilimo. Hii iliwajenga vijana kwa kuwapa ujuzi na pia kuona kilimo kama sehemu ya maisha.
Tatu
Elimu ya siasa ,maisha halisi na historia za kila eneo zilijadiliwa kwa uhuru na uwazi hivyo vijana waliweza kujua nini Taifa lao lilihitaji kutoka kwao. Liliwapa ujasri wa kujifunza na kujenga hoja zilizozaa wanasiasa kwa asili na sio wababaishaji.
JKT
Baada ya kufunzwa yote,waliwekwa makambini kuivishwa ujasiri ili kuwajengea uwezo wa kujiamini na kusimamia wanachokiamini.
Leo vyote tunaharibu kwa sababu ya pesa lkn tunataka wasanii wawaimbishe watanzania ili wawe wazalendo.
Tujitafakari.