Uzalendo ni nini?

Uzalendo ni nini?

Ni kichaka cha kufichia upigaji kwa maneno ya majukwaani
 
Habari wanajamvi. Kama kuna kitu kinanitatiza sana miaka hii ni matumizi ya neno "UZALENDO". nikiwa shule ya msingi niliwahi fundishwa kuwa mzalendo ni "mtu anaeipenda NCHI yake, na kuwa tayari kuipigania na hata kufa kwa maslahi ya nchi yake". Labda kama walimu wangu walinidanganya maana nachokiona leo ni tofauti na nilichofundishwa. Sikuhizi nasikia hawa wanasiasa wetu wakikusikia unaikosoa serikalo au kuwa na maoni tofauti na wao juu ya mambo fulani watasema WEWE SIO MZALENDO. mfano, lissu,zitto na wengineo walipokua wakikemea mambo mbalimbali kama mauaji n.k .. Baadae pia nikasikia UZALENDO ni ile hali ya kuhama toka upinzani na kuiunga mkono SERIKALI iliyopo madarakani. Mnaojua maana ya uzalendo msaada please. Nataka kuelewa.


Ndugu zangu tujadili mambo machache yatakayotupa fursa ya kujadili mzalendo halisi kati ya hawa ndugu wawili.

Tundu Lissu amekuwa akitetea madini yetu miaka 20 iliyopita na kupinga kwa nguvu sera zote na sheria zinazopelekea nchi kukosa faidi ya uchimbaji wa madini.

JPM amekuwa akiunga mkono sera zote na sheria mbovu zilizokuwa zikiandaliwa na chama chake cha ccm na kupata baraka zote za baraza la mawaziri akiwa miongoni mwao. Ni lini mliwahi kumsikia JPM akisimama bungeni na kupinga hata kwa maneno machache kuwa hakubaliani na sera na sheria za madini?

Tundu Lissu hajawahi kuliingizia hasara taifa na kusababisha kulipa fedha nyingi za kigeni kwa ajili ya kushindwa kesi yoyote iliyosababishwa na maamuzi ya kuvunja mikataba bila utarataribu.

JPM amewahi kusababishia nchi hasara lukuki za kufanya kutokana na kuvunja mikataba holela bila kufata sheria za mikataba. eg meli ya uvuvi ambayo anasingizia kuwa wakubwa fulani walienda kulipa pesa ndio maana alishindwa kesi, hajawahi kuwataja kuwa hao wakubwa ni wakina nani na wametoka chama gani. Kivuko chakavu alichonunua na kuaminisha watu kuwa ni kipya. Makinikia ambayo bila utaratibu aliyazuia na kitakachotokea ni kuliingizia taifa hasara. NK yapo mengi sana.

Ni lini JPM aliwahi kusema hadharani kuwa chama chake hakiongozi nchi vizuri kinasababishia taifa hasara, badala ya kusifia na kupiga makofi na baadae kusema ndiyoooooo naunga mkono hoja?

Ni nani aliyeliaambia taifa kuwa ndege iliyonunuliwa na serikali imekamatwa kutokana na deni la kesi iliyosababishwa na JPM kama siyo Tundu Lissu?

Hivi kati ya hawa wawili ni yupi mzalendo halisi wa taifa hili?

Karibuni
 
Uzalendo ni kuipenda na kuitetea nchi (siyo watawala wala vyama)
 
Habari wanajamvi. Kama kuna kitu kinanitatiza sana miaka hii ni matumizi ya neno "UZALENDO". nikiwa shule ya msingi niliwahi fundishwa kuwa mzalendo ni "mtu anaeipenda NCHI yake, na kuwa tayari kuipigania na hata kufa kwa maslahi ya nchi yake". Labda kama walimu wangu walinidanganya maana nachokiona leo ni tofauti na nilichofundishwa. Sikuhizi nasikia hawa wanasiasa wetu wakikusikia unaikosoa serikalo au kuwa na maoni tofauti na wao juu ya mambo fulani watasema WEWE SIO MZALENDO. mfano, lissu,zitto na wengineo walipokua wakikemea mambo mbalimbali kama mauaji n.k .. Baadae pia nikasikia UZALENDO ni ile hali ya kuhama toka upinzani na kuiunga mkono SERIKALI iliyopo madarakani. Mnaojua maana ya uzalendo msaada please. Nataka kuelewa.


1-Uzalendo ni kutukana wapinzani na kuwafanyia kila jambo baya
2-Uzalendo ni kusifia ccm na serikali ya awamu ya tano hata kwa kusingizia watu kama anavyofanya Musiba
 
Ni kumuunga mkono raisi magufuli (Revised Version ya sasa).
 
Uzalendo, according ya wazee wa chama na wenye mawazo ya kale, ni kupaza sauti na kusema "Zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti".

Wazee wa Mlimani waliobebeshwa vitabu vya Karl Marx na kumuimba Kambona wanaamini uzalendo ni kutii mawazo ya Mwenyekiti. Wazee hawa ndiyo maprofessa, wakuu wa vitengo, wachambuzi mashuhuri na watu wenye heshima nchini. Kasumba hii wanarithishwa vijana kwa sasa.

Wazee hawa wanaamini Tajiri au Mfanyabiashara si mzalendo lakini maskini kapuku ni mzalendo.
 
JE, UZALENDO NI NINI NA NI WAKATI GANI HASA MTU UNATAKIWA KUONYESHA UZALENDO WAKO KWA VITENDO?

Ndugu wanajukwaa poleni kwa kwa kazi ya kuijenga Tanzania yetu. Kama kichwa cha habari kilivyo hapo juu, kipo kwa mtindo wa swali naomba mnisaidie kunipa ufafanuzi wake.

Mara kwa mara nikipitia post mbalimbali humu jukwaani, na mijadala mbalimbali kwenye media zetu na hata vijiweni watu wamekuwa wakijinasibu kuwa wao ni wazalendo, au kuwaelezea watu wengine ambao ni wa kundi lao kuwa ni wazalendo wa kweli.

Akitokea mtu akawa hakubaliani na tafasiri yao kuhusu uzalendo au kutokubaliana nao juu ya uzalendo wao au wa watu wao basi mtu huyo anaweza kubatizwa majina ya msaliti, na au kibaraka wa Mabeberu.

Wanajukwaa naomba mnisaidie ufafanuzi kama maswali ya kichwa cha habari yanavyouliza. Ili uweze ku-qualify kuwa mzalendo unatakiwa kufanyaje? Na ni wakati gani hasa unatakiwa ku-practice huo uzalendo?

Kwa mfano watu wengi wamekuwa wakimwelezea Hayati kuwa alikuwa Mzalendo namba 1. Wakitolea mfano jinsi alivyojitoa katika kulinda raslimali za nchi ili ziwanufaishe Watanzania.

Pia, katika kuuthibitisha uzalendo wake alihakikisha hatumii madaraka yake kujinufaisha binafsi bali aliwaletea maendeleo watanzania katika kuboresha miundo mbinu na huduma za kijamii ikiwemo kutoa elimu bure kwa watoto wa wanyonge.

Wakati huo wanapotokea watu wengine kuelezea negativity za Hayati, kama kutokuheshimu katiba, kubomoa demokrasi, kuharibu diplomasia, kuharibu uchumi kwa kuwavuruga wafanyabiashara na badala yake kuwa entertain wamachinga, kufumbia macho vitendo vinavyokiuka haki za binadamu, kama watu kutekwa, kupotea kuuawa, kupigwa risai na zaidi walengwa wakiwa ni wakosoaji wake na serikali yake.

Hao wanaambiwa sio wazalendo. Sasa naomba mnisaidie uzalendo ni nini, na ili uitwe mzalendo unatakiwa ufanye nini?

WAKATI GANI NDIO MUAFAKA WA KUONYESHA UZALENDO WAKO?

Je inawezekana kuwa mzalendo ukiwa ni raia wa kawaida au hata kama upo kwenye wadhifa mdogo ambao haukupi nafasi ya kufanya maamuzi yoyote kwa ajili ya nchi yako?

Najaribu kuuliza swali hili japo linaweza kuonekana la kijinga hii ni kutokana na historia ya Hayati. Akiwa mtumishi wa serikali tena kwenye ngazi ya uwaziri kwa takribani miaka 20, ukiachana na bidii ya kazi aliyokuwa nayo, lakini hakuwahi kuuonyesha uzalendo wake waziwazi kwa kukemea vitendo vya ubahilifu, rushwa na ufisadi kufuatia kashfa mbalimbali zilizokuwa zimetokea kipindi cha uongozi wa Rais Mkapa na Kikwete.

Tofauti na ilivyokuwa kwa akina Dr. Slaa, Zito Kabwe, Kafulila, Selelii, Lembeni, Sendeka, Mwakyembe, Lissu, Mnyika, Filikunjombe, Mpina na wengine wengi, Hayati hakuwahi kufumbua kinywa chake kukemea hivyo vitendo.

Kuna baadhi ya watetezi wake wanasema kama angethubutu kufanya hivyo asingeweza kupata nafasi ya kuwa mgombea na hatimae rais. Sasa swali ni je ili kuwa Mzalendo unatakiwa usubiri mpaka uwe rais? Kama jibu ni ndio je hawa wengine wote wanaojiita Wazalendo wakati kumbe uzalendo ni wa rais peke yake wanapata wapi huo ujasiri wa kujiita wazalendo?

Na uzalendo ni sifa anayoweza kuwa nayo mtu yeyote, kwanini basi Hayati alizinyamazia kimya kashfa zile za akina Kagoda, Tegeta Escrow, Richmond nk?
 
Neno Uzalendo huwa linanipa tabu kidogo kutofautisha kati ya mzalendo na mwananchi.

Uzalendo naona ni upendo wa nchi yako kwa dhati na kuitetea kwa nguvu zote na kulifanya taifa lako kuwa na nguvu na upendo kwa wenzako haijalisha awe Kabila gani au dini gani.

Mzalendo ni yule anaependa wenzake kwa kutumia ardhi pamoja na rasilimali zake. Ila kama una chuki na wenzio kwa kuwaumiza au kuwaudhi mkiwa nchi moja huo sio Uzalendo.

Mzalendo anahakikisha tunaishi kwa misingi ya umoja na kuheshimu bendera yetu popote pale kwa kuipenda nchi.

Nafikiri huo upendo maana yake kusaidiana na kuilinda misingi yetu na kukataa maovu bali mazuri.

Sasa hapo ndio linapoingia MWANANCHI wala rushwa na waizi wa Mali za umma, wanyanyasaji na wauwaji wataingia kwenye hii na sio Mzalendo tena.
 
ili uwe mzalendo wa kweli ni lazima kwanza upende kutenda haki kwa wananchi wote bila upendeleo wala ubaguzi. uwapende wanabchi wenzako.lkn pia mara zote uwe tayari kuwetanguliza masilahi ya Nchi kwanza kuliko masilahi yako binafsi au ya ndugu au rafiki zako.
 
____________________________________
[emoji842]Kuvaa vazi lenye bendera ya Taifa sio Uzalendo.
[emoji842] Kuvaa skafu ya bendera ya Taifa sio Uzalendo
[emoji842] Kuwa chama tawala na kusifia kila kitu sio Uzalendo
[emoji842]Kuwa chama Cha Upinzani na kupinga kila kitu sio Uzalendo
[emoji842]Kuwa mwanaharakati na kupinga ama kutukana serikali sio Uzalendo
_____________________________________

Uzalendo ni nini?

Kwangu mimi Uzalendo ni kuipenda nchi yako. Je, kuipenda nchi yako inatosha? Jibu ni hapana. Ni kuipenda nchi, kuilinda na kuitetea kwa hali yoyote popote unapokuwa kwa maslahi ya Umma. Hii ni pamoja na watu wake, rasilimali zake na vyote vilivyomo ndani ya nchi. Kulinda na kutetea nchi na watu wake dhidi ya unyonyaji, uporaji wa nguvu au wa mikataba, wizi, ufisadi, upendeleo pamoja na ukandamizaji na uonevu kwa watu wasio na Sauti.

Kwako Uzalendo unamaanisha nini?
Screenshot_20210805-164924.jpg
 
Back
Top Bottom