Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Ndugu umekuwaje nowadays tangu uitwe kikaoni na nduGUY asee umekuwa toothless... siri gani hataki zijulikane au hizi za watu kugawama mabilioni ya hela
 
Ni kweli CHADEMA siyo liberals ni Social democrats zao la the Paris Commune, lakini wanafuata the NORDIC MODEL.

Liberals pekee hapa nchini walikuwa ni CUF ambao kwa sasa wamepoteza mwelekeo wa kujenga itikadi yao hiyo toka mauaji ya mwaka 2001.

Hakuna popote CHADEMA waliwahi kutangaza itikadi ya uliberali haipo hata kwenye katiba yao itikadi yao imesemwa wazi wazi.

Unajua nini maana ya kuwa social democrats ( Center Party) juu ya haki za watu na sera za kiuchumi.
 
Endeleeni kutumia risasi kama kwa lissu ndy njia pekee ya kuwafanya watu wawe wazalendo.
Tofauti ya ivo mayalla utapiga kelele sana.
Watendeeni watu iliyo haki yao, watakuwa tu wazalendo.
 
Ongeza mahaba ndugu ipo cku nawe utaonekana tu
 
Hata hiki kinachoendelea sasa kuhusu alipo rais Magufuli na uvumi kuhusu afya yake, sio kitu cha kunyamazia!. Where is responsible journalism?, where is our media?. Kwanini tunanyamaza?.

Paskali
 
Hata hiki kinachoendelea sasa kuhusu alipo rais Magufuli na uvumi kuhusu afya yake, sio kitu cha kunyamazia!. Where is responsible journalism?, where is our media?. Kwanini tunanyamaza?.

Paskali
Wakati tulipoamua kujiimarisha kwenye utamaduni wa ki communist , hukuelewa athari zake Pascal Mayalla ?!. Magazeti, redio na TV vilivyojaribu kuwa fair kwa wananzengo unaviona hewani ?!. Na kama vipo hewani ni kwa fine kubwa. Unakumbuka kisa cha RIP Dr Mengi na dogo Spencer Lameck kupigwa mawe pale Lumumba siku ya kukabidhiwa cheti cha ushindi ?! Ikishakuwa vile ni mwandishi gani, atathubutu kusogeza pua ?!

Wewe mwenyewe ulijaribu kuuliza swali zuri kabisa . Lakini kilichofuata ni tafsiri ya jina lako na kuitwa Dodoma. U communist ni laana duniani . Kwenye u communist tunakuwa na zaidi ya wafalme.
 
Hata hiki kinachoendelea sasa kuhusu alipo rais Magufuli na uvumi kuhusu afya yake, sio kitu cha kunyamazia!. Where is responsible journalism?, where is our media?. Kwanini tunanyamaza?.

Paskali
Paskali, media zinaogopa kufungiwa kwa kuuliza tu wapo alipo mpendwa rais wetu, Mhe.Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Imekuwa ni taboo kwa yeyote atakayeuliza ataadhibiwa kwa kuuliza tu. Sisi wananchi wa nchi hii tunataka kujua yupo wapi ili to clear the rumours about his whereabout, it is our core duties and responsibility as responsible citizens of this country to know where is our president and how is faring? Please i am going to start hashtag #Where is our president-TZ.
Tunataka kujua maana tunasikia uvumi kuwa anaumwa, lakini pia kuumwa si kosa la jinai, na siyo taboo, tunataka kujua anaendeleaje? Hiyo siyo privacy...Huyo ni kiongozi wa umma na sisi watanzania wote ni waajiri wake. Tunataka kujua yupo wapi...ni haki yetu, waziri mkuu Majaliwa umekosea, rais ni mwajiriwa wetu ikiwa pamoja na wewe kwani hujui mheshiwa premier kuwa mnalipwa kwa kodi zetu.
#Where is our president-TZ.
 
Nyie mnaokula vizuri na kutembea na magari mazuri ndo kazi yenu hyo!!

Mbona sisi huku mmoja anapigwa marisasi na wengine hawamtetei na ukitaka kufanya hvyo unapigwa burn na polis huo moyo wa kulitetea taifa utatoka wapi!!?

Kama viongozi wetu wanachafuliwa wachafuliwe tuu wataenda kuoga. Sie wavimba macho hatuna hata time nao😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Au nasema uongo ndugu zangu!!?
 
Husemi uongo kaka kula tano
 
Yan mtu anadhulumu uchaguzi wa nchi nzima,watu wameuza Mali zao wagombee,wakapiga kampeni, watu wakadamka asubuhi kwenda kupanga mstari kutwa nzima wapo juani ili kupiga kura,halaf mtu mmoja tu akaamue wadhulumiwe haki zao. Leo huyo mtu apatwe na majanga ya dunia watu wafurahi na kumtukana mimi nijitokeze kumkingia kifua kweli!? Uzalendo huo wa kinafiki sina..
 
Mayalla! Sote tunafahamu kilichojiri kwa miaka 6 sasa...

Wewe ni shahidi wa namna ambavyo hadi kampuni yako ilivyopunguza wafanyakazi..

Ni nyakati za viongozi kushuka na kujenga ule mshikamano halisi wa kitanzania...

Ni katika awamu hii unashuhudia kiongozi anasema ubebe msalaba wako umepatwa na janga asili kama tetemeko la ardhi unaambiwa serikali haina shamba na hakuna chakula cha msaada kitaletwa , pia walau kujengewa nyumba zingine..

Ukweli unafahamika haina haja ya kufanya sugar coating kweli ukweli usiopingika chuki hii ilifugwa muda mrefu na isipotafutiwa ufumbuzi itaendelea hata miaka kenda...leo hii tunaombeana kifo ujue tumefika hatua mbaya kama taifa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…