Hoja za huu uzalendo wa ajabu wa baadhi ya Watanzania wenzetu, bado unaendelea, sasa uzalendo huu umehamia Twitter, watu wanafurahia hadi kushangilia wakati siri za ndani kwenu, nyumbani na chumbani kwa baba na mama, zinaanikwa hadharani!.
Baadhi ya siri hizi za taifa letu zinazomwagwa Twitter ni classified information, nyingine ni secrets, na hali hii ikiachwa iendelee hivi hivi inavyoendelea, kuna siku folder la top secrets za ile Idara yetu, zitakujashuka kwenye public domain!, kiti ambacho ni threat to our national security, mfano itokee yule jamaa akute kumbe wale 'jamaa', waliofanya kile kitendo cha lile shambulio, pale 'mahali' ni inside job!, kutakuwa na usalama, amani na utulivu?.
Kitendo cha kupublish taarifa classified information kuhusu nchi yako, hivyo kuzifanya zionekane nje ya nchi, ni uhaini, ila uhaini huu sio wa kusambaza tuu, bali hata wale wanafurahia taarifa hizo, ni kuufurahia uhaini, hivyo huu uhaini wa kufurahia uhaini kwa nchi yako, japo haina any criminal liability lakini it has something to do with uzalendo wako.
Huu ni uzalendo wa aina gani?.
P