Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Yamepita na wewe sasa subiri mwingine ufanye unafiki kwake.
 
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuoga rasmi.
Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x 3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 
Hili nimekuwa nikishauri kwa muda mrefu tuu, lakini halifanyiwi kazi, sijui kwa nini?!.
P
 
Hata bunge lilipotupandishia tozo za simu na mwigulu akatudhiaka,tumenyamaza
kwa hiyo ni kawaida yetu kunyamaza,wewe unayeweza kusema endelea,ukimaliza utujulishe napo tutanyamaza
nani anataka kuvunjwa miguu?
 
Wanabodi, kwa uteuzi wa mwanahabari nguli wa BBC, Zuhura Yunus kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, mimi naamini mambo kama haya hayata nyamaziwa, yatajibiwa kikamilifu.

Huyu binti ana uwezo, weledi na exposure, atamsaidia sana Mama Yetu na ataisaidia sana nchi yetu. Tumempata mtu well experienced mwenye good exposureä, mwenye the ability, the capacity na the capabilities za kuwa sio Mkurugenzi Press Release, Mkurugenzi Msemaji wa Rais .
Hongera Zuhura Yunus.
Welcome on Board.
Paskali
 
Mkuu Paskali , heshima yako kwanza.

Naomba nichangie kwanza kwa kusema umuhimu wa katiba mpya ndio unaonekana sasa .

Tanzania why Rais aonekane malaika ?

Kwamba watanzania wanamtukana Rais je ni wazalendo?

Yaani watanzania wamtukanapo rais ndio uzalendo wao unapoanza kuhojiwa?

Je rais akiwatukana watanzania tumuhoji wapi na tumshitaki wapi?

Au pia atakuwa sio mzalendo.

Kwangu naona hiyo ni double standard

Tuweke sheria ya kukata kotekote.

Watu waliambiwa ukimwi nyie, katerero nyie, mto ngono nyie, tetemeko nyie and walikua kwenye disaster was that right?

Only truth shall set you free.
 
Wewe KILA mtu anayetuliwa unamsifia na kumpamba! Unalenga kufanikisha nini?
 
Pia waliambiwa walio upande wa Lowassa ni malofa na wapumbavu!
 
 
Wanabodi,

Makala za Kwa Maslahi ya Taifa na Pascal Mayalla
Naendelea na Makala zangu ziitwazo Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo huchapishwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la kila siku za Jumatatu.

Hoja ya Udikiteta
Jumamosi Njema.
Paskali

Uzalendo wetu unapitia mtihani!.
P
 
Hata Ndugai alikuwa Spika mzuri mpaka alipokubambikia kesi ya kudharau bunge lake "takatifu".
Angekuwa Spika mzuri asingempiga rungu mgombea mwenzake ambae sasa ni marehemu, angekuwa Spika mzuri asingejijengea hofu na kujiwekea kinga! Ya kushitakiwa. Angekuwa Spika mzuri asingeshindwa kuelewa neno " huenda au inawezekana" na kupelekea wewe kufungishwa safari ya utalii wa ndani Bungeni. Kwa kifupi alikuwa Spika kwa sababu Tanzania kila kinachopitishwa na CCM ni bora liende.
Na yule msukuma mkonongo is PROBABLY THE LAST DICTATOR.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…