Wanabodi,
Makala za Kwa Maslahi ya Taifa na Pascal Mayalla.
Naendelea na Makala zangu ziitwazo Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo huchapishwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la kila siku za Jumatatu. Hizi Makala zitafuatiwa na Kipindi cha TV chenye jina hilo hilo ambacho kitaanza kutoka kwenye vituo kadhaa vya TV hivi karibuni baada ya taratibu za udhamini kukamilika, vikiangazia hoja mbalimbali muhimu kwa maslahi ya taifa letu la Tanzania.
Hoja ya Udikiteta Tanzania.
Kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa nikijadili hoja ya Udikiteta Tanzania. mada ya leo ni kuhusu uzalendo wa ajabu wa Watanzania kuunyamazia uongo unaoenezwa kimataifa kuhusu huu udikiteta Tanzania. Jee Sisi Watanzania, Tuna Uzalendo Gani Kunyamazia Huu Uongo Unaonezwa Kimataifa Kuwa Rais wa Tanzania ni Dikiteta na Tunatawaliwa Kidikiteta?. Au Kwa Kunyamaza Huku Ndio Kukubali Kwenyewe Kuwa ni Kweli Taifa Letu Tanzania Tuko Kwenye Udikiteta?
Kama ni Kweli Tanzania Tuna Udikiteta na Sisi Wenyewe Tumeukubali, Kwa Nini Watuingilie?.
Kama ni kweli rais wetu Magufuli anatenda kinyume cha katiba na sheria, na taratibu za kumshughulikia zipo lakini sisi Watanzania wenyewe tumeridhika naye na utendaji wake huo huo, hivyo hivyo anavyotenda iwe kwa kuvunja katiba au kinyume cha sheria, Watanzania wenyewe tumeridhika na kukubali, who the hell is jirani yasiyomhusu, anayekuja kutusemea kwenye media yao kuwa rais wetu amekosea?. Kama wenyewe tumekubali na tumeridhika, huyu jirani anamsemea nani?!. Kwa nini Watanzania tunanyamasia uongo huu?.
Wiki ijayo, nitakuja na set ya maswali kuhusu hoja za udikiteta ambayo nitayaelekeza kwa Waziri wa Sheria na Katiba. Prof. Palamagamba Kabudi.
Jumamosi Njema.
Paskali
Update
Nitauapdate uzi huu kwa michango michache objective.