Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Enyi Watanzania mmelaaniwa? Aliyesoma vizuri hii mada ya Paskali na atoe maoni. Naona baadhi tunatukana tuu kinyume na kilichomo humu. Tusome wakuu. Hekima IPO kwenye maandishi. Bravo Paskali
 
Tatizo hapa Paskali baadhi yetu Watanzania toka 2015 kabla na baada ya uchaguzi tulijiaminisha kupata matokeo tofauti na yaliyotokea.

Kuna wafuasi wa chama cha siasa waliongoza kampeni ki kanda na kuwalazimisha wenzao wa ukanda huo wawaunge mkono hata kama hawakuwa wameandaliwa vya kutosha kufanya ivo. Ni kweli walifanikiwa kuligawa Taifa na kuuaminisha umma wa Tz kuwa chama fulani ktk kanda yao kimekufa na kwamba yyte asiyewaunga mkono kwao alionekana msaliti wa kanda hyo.

Walifanya ivo bila ya kuwa na hesabu za kutosha kwamba Je idadi yao ilikuwa inatosha kuwapa ushindi wa uchaguzi wa Rais?.

Walishinda vzr ubunge na udiwani lkn Urais waliukosa. Kwa kushinda wabunge wengi ni dhahiri rais alishindwa kuchagua wabunge ili wawe mawaziri kutoka ktk kanda yao sbb hakuwa na wabunge wa kuchaguliwa huko.

Hata wa kuteuliwa na Rais kwa wakati ule haikuwa rahisi kuwateua kwani ilionekana kabisa wapo ki usaliti usaliti na uvuaji wa uanachana unathibitisha hilo.

Hoja yangu ni kwamba wenzetu wa kaskazini ndio chimbuko la ubaguzi wa kikanda kufuatia uchaguzi wa 2015 na kwa kuwa wamekosa nafasi za uteuzi serkalini wamegeuka sasa na kudai kuwa wanabaguliwa na kuwa chanzo cha malalamiko yote uliyoeleza hapo juu.

Na ni wao kwa kupitia taasis zao kisiasa na zenye maslah nao wameenda mbali na kuamua kuitangaza nchi vibaya ktk anga la kimataifa kuwa haitawaliki.

Wakati mwingine unaweza kujiuliza kwa nini serikali haijibu tuhuma hizi lkn pia ni busara mtu kujiuliza na anaesambaza taswira mbaya tena ya uongo au mkwamo ambao yeye na taasis yake wameuanzisha anakuwa anafanya kwa maslahi ya nani hasa?

Ni wakati sasa wa ninyi akina PASKALI kuacha kuwa sehemu ya upande fulani na kuileza dunia ukweli wa kinachoendelea nchini na sbb zake.

Kuna watu wenye uchumi mkubwa ambao wamebanwa na utawala huu ktk mabiashara yao kodi na kadhalika hawa pia ni waathirika wa utawala huu kwa nguvu zao wanaweza kuichongea nchi yetu kimataifa ili tu Rais aonekana mbaya na atoke madarakani lkn je ni kweli Rais huyu ni mbaya??

Miradi yote ya maendeleo anayofanya nchi nzima ni kwa faida ya nani hapo kesho na keshokutwa.

Kumwambia mwananchi afanyekazi kwa bidii ndipo apate kula yake ni kosa? Kama ni kosa mbona hata maandiko ya dini yanatuhimiza tufanyekazi?

Kuna tuhuma nyinginie hutolewa na wapinzani wa Rais aidha kisiasa au kimaslah binafsi kuwa anafanya miradi yote mikubwa kwa kutumia pesa za walipakodi anamaliza tu pesa. Je hili ni kweli?. Kuna Mtanzania muelewa asiyejua makuasanyo ya nchi kwa sasa yanaenda wapi?

Nafikiri kwa kuwa wanachi wenyewe tunaona na tunajua sbb za hizi kelele ni wakati wa kumpa moyo Rais wetu ili aendelee na majukumu yake alioahidi kututimizia na tunaona anafanya kwa vitendo.

Kutatuliwa kwa kero nyingi za Watanzania kwa wakati mmoja nayo imekuwa nongwa kwa baadhi ya wanaojiita wanasiasa kwamba sasa ktk chaguzi zijazo watawakilisha kero gani kwa wananchi kuonesha kushindwa kwa serikali?. Wanasiasa wa aina hii mimi huwa ninawadharau sana na tena wanapaswa kuingia kwenye kundi la watesaji kama si wauaji wanaogeuza shida za wananchi kuwa mitaji ya kisiasa.
 
Umeandika meeeengi ambayo ni point less!!

Swali moja tuu kwako hali ya kitaifa yanayoendelea hapo Tanzania wewe waona sawa???

Watu wachache haiwezekani wakakiuka Sheria wajibu na maadili kwa kusingizia uzalendo,

Naweza nikasena huko ni taifa la wajinga na siku zote mtakuwa wajinga mpaka atakaporejea mkombozi
 
Nikisoma comments za watu wengi humu najiona mtu mwenyewe akili sana! Watanzania ni nani alituloga? Mnaombeza Paskali Hivi mmesoma kwa umakini alichoandika kweli?
 

Raisi kwako aisee yupo kwa maslahi yake na jamii inayomzunguka

Mimi bianafsi hanihusu
 
Yaani kwa mara ya kwanza makala yako nimeisoma kidogo nikaacha huku nimechukia. Hivi unajua kuwa kikatiba Rais akitenda mambo yanayodhalilisha nafasi yake bunge Lima uwezo wa kumtoa madarakani?
Sasa hayo mambo yanayosababisha atukanwe ndio hayo yaliyo paswa Bunge kuwa washamtoa. Bunge ndio linakosa uzalendo kumuacha MTU anayevunja katiba aliyoiapa. Hivyo akitukanwa huko nje tunaona tumepata wa kutusemea maana nyie mnaopata nafasi hizo mnazitumia kusifia tuu hata kama mtawala anatawala kijuha
 
kwan alivoitwa "authoritarian" uongo upo wap?
kwa tuliosahau maana ya authoritarian ina maana mtu asiyetumia katiba na kubana uhuru wa mmoja mmoja ivyo anataka aheshimike kwa lolote"

nakumbuka mkulu alivoulizwa kuhusiana na katiba alijibu kuwa katika kampeni zake hakuongelea katiba hivyo anataka kuinyosha nchi then katiba baadae....'

sasa anavoitwa authoritarian wap umeona uongo?
bwana paschal uzalendo ni kulitumikia taifa na sio mtu mmoja
 
Safi sana nilichokiona hapo ni kuwa hakutakuwana maandamano wakuandamana hawapo ni porojo urojo za mitandanoni
 
mkuu Paskali, waambie hao wakuu kwanza waache kutuita sisi wananchi ma-lofa na vi-laza, ndiposa nasi tutapigana hadi tone letu la mwisho la damu kwa ajili yao!
 
Ndugu yangu Pascal Mayalla,
Ni kitu kigumu kumeza, lakini kwa sababu chi ni ya watu wawili, Bashite na Sizonje, ngoja watukanwe. Nadhani tupo wengi tunaoweza kujibu lakini kwa sasa ngoja tukan nyuma tuangalie mwisho wa, maana hata sisi wenyewe tunatishwa sana na hawa watu wawili. Bora wachafuke ili mwisho wao uje haraka
 
Paskali, baba akiwa mlevi na akienda kilabuni akilewa ana kunya juu ya meza akitukanwa utatoka na kumtetea kuwa hayo sio ma.. bali ni keki?
Hapo sii unataka nawe ujumuishwe kwenye matusi! Kama watoto hatuwezi kushiriki kumtukana bora tunyamaze wamtukane ajirekebishe maana hata watoto anatuuzi.
Huo ndio uzalendo tunaoweza kuuonyesha
 
On one side unasema wew ni Rais anaye jiamini kwelikweli on the other side una haras wananchi wako hadi kwenye misiba eti wanafanya siasa. Una ratibu vikundi vyakuteka kutisha na kuua watu. Huko ndo kujiamini kweli? Kuna mijitu inashangilia matendo hayo ati ndo uzalendo. Mpendeni wenyewe
 
Inawezekana wengi hawakuelewi lakini mimi huwa nakuelewa sana.
Aina ya uandishi wako kama mtu ni kichwa maji hawezi kukuelewa kabisa, na ndo maana jf nayo imejaza wengi wasio waelewa.

Kwanza ile makala iliandikwa kwa kingereza na isingeweza kuwafikia wengi, wewe umeamua kuisambaza tena kwa kiswahili kwenye jf na kwenye gazeti ili wengi ambao hawakusoma wapate kusoma na kuujua ukweli.. Heko Bwana ukame.
 
Sijakuelewa! Yaani unamaanisha kuwaeliminate na kuwaerrase from the earth surface au? Na kwanini unashauri njia potofu kiasi hiki as if mnaotuhumiwa mna hati miliki ya kufanya mtakavyo bila kukosolewa? Hapana na hapana tena kwa njia hii unayoishauri bali zingatieni sheria na katiba kwani uongozi tuliwapa sisi na msijifanye malaika au miunguwatu katika uongozi! Na hizi njia unazozishauri ndizo hizi zinazosababisha msemwe na kila mpenda haki! Hebu jisome umeandika nini kama hujajikataa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…