punguza hasira mkuu shusha pumzi......... enhee kwani vipi maana huku tunakodolea moshi wa vibatarii... embu tujuze
Ile ya jana ilikuwa hivi kwa ufupi leo sijatazama
Ayanda alikuwa anamuaga sma kuwa ataondoka kwenda kwa kina dhlomo kijijini kumfanyia imbeleko sibahle, wakapeana ahadi nyingi na sma pia ayanda alimletea sma msosi.
Mangcobo akiwa na wanae mxo na nosi wakipiga story kuhusu zakele mwili wake kuchomwa moto (cremated) mama huyu anawaambia wanae kuwa akifa wamzike sio kumchoma moto. Wanacheka na kugonga cheers.
Pia wakati wa kufunga saloon gc anawapa Wenzie umbeya kuwa mwili wa zakele utachomwa moto.
Kwa mangcobo anakuja mmama mmoja mganga anadai katumwa na mamlahmbo maana mamlambo yeye yupo kijijini kwa kina dhlomo, mganga huyu anafukiza nyumba nzima huku akitaja neno zakele out!
Kijijini wakati wa utambulisho wa sibahle kwa wazee wengi wanamkubali anawasalimia kwa heshima ila anapofika kwa mke wa dhlomo aitwaye macele huwa anakaa kijijini, Anakuwa mkali na nyodo nyingi anakataa kuitikia salamu kabisa. Dhlomo anamvutia pembeni kuwa atulize munkari.
Mxo anamuagiza zweli aendelee kumtafuta sbu dhlomo akirudi asimpate, zweli anatafuta mpaka mapagaleni anamkosa sbu ila anakutana na yule dk aliyemchukua sbu naye anadai hajamuona muda to, zweli anarudi kwa mxo kutoa majibu kisha anaaga kwenda gateway kutafuta pisi kali imdangie hela zake.
Kijijini tena wwanamfanyia sibahle imbeleko yale majani impepo yanakubali kuwaka. Shughuli zinaendelea.
Wazee wanakusanyika na kunywa pombe na nyama, ayanda anakataa kunywa pombe na mzee mmoja kaka wa dhlomo anabishana na ayanda kiutani kuhusu dini anamwambia ayanda dini ni wizi ayanda anabishia kiustaarabu mwisho wanacheka wote na mjomba anasema siku moja atakuja kanisani kwa ayanda.
Sibahle anapewa makazi mengi kuosha vyombo na mke wa dhlomo, manzuza anakuja kumuokoa sibahle kwa kudai anamuhitaji mara moja..
Baby mama ex wife wa mondil asubuhi anabishana na mondil anaulizwa ulimwambia nn nosi Why aliondoka amekasirika, huyu ex wife (mbale) anadai alimwambia nosi kuwa yeye (mbale) na mondil nifamily wana bond kubwa, mondil anakasirika na kuacha kunywa chai anaondoka kuelekea kwa nosi kumuomba msamaha ila nosi anagoma na kumtaka achague moja mondil anajibebisha lakini wapi.
Dhlomo anaongea na manzuza mambo mbalimbali, katikati ya mazungumzo wanaulizana kuhusu ayanda na sibahle wakwapi,
Dhlomo anajibu kuwa watakuwa wameenda matembezi hivyo watarudi tu
Huku ayanda na sibahle wanaenda mtoni huko wanapiga story wanajuana background zao kisha wanatandika kitambaa chini wanakaa na ghafla wanapigana denda..
NB: dhlomo ana mke tumepigwa wote Za uso 😁😁😁