Uzamiaji Afrika Kusini: Mikasa katika harakati za kuzamia Afrika Kusini kwa njia za panya

Uzamiaji Afrika Kusini: Mikasa katika harakati za kuzamia Afrika Kusini kwa njia za panya

Haya na mm Niko ApA mnk kote uliko taja kuanzia namanjere na mji wa sumbawanga na hicho kijiji Cha chiwanda tunduma kote uko nimaeneo yangu ...sas bas uje baadae ueleze jins ulivyopata hela za safari
 
Huu uzi una matatizo gani? Story kama ya gazeti la udaku, haiishi
 
Story tamu sana
Hasa hapo kwa simba
Sipati picha ningekua mimi mhhh
 
Mwingine tena kaja na mastori ya S.A

Wazee wa kukimbia nyuzi zao
 
Sehemu ya 3.

Majira ya saa sita mchana ilifika ‘defender’ ya polisi ikiwa na polisi 7 wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu, walikuwa wamevaa kivita wakiwa na sura zilizo sheheni hasira na silaha nzito nzito. Baada
ya kuwasili walienda moja kwa moja hadi kwenye ofisi kuu kwa ajili ya mak- abidhiano baada ya hilo zoezi kukamilika tulitolewa sehemu tuliyokuwa tume- fungiwa tukapigwa pingu na kisha kuingizwa kwenye gari, askari walionekana kuwa na tahadhari kubwa dhidi yetu utadhani wanasafirisha magaidi.
Haraka sana safari ya kuanza kurejeswa makao makuu ya wilaya sehemu am- bayo tulitoroka baada ya kisa cha yule askari kumwagiwa kinyesi na bwana Rodrik Chanda. Ilikuwa kama sinema na pia ilikuwa siku ngumu sana kwangu, wakati wote wa safari yetu gari ilikuwa inakimbia sana, ndipo baada ya Kama saa moja hivi tangu tuianze safari na tukiwa kwenye mwendo mkali Sana nili- sikia mlio mkubwa wa kitu kupasuka puuuu mlio huo uliambatana na kishindo cha hali ya juu sana, kisha sikujua kilichoendelea tena lakini baada ya sekunde kadhaa hivi niliona vumbi jingi sana na damu nyingi pembeni yangu, kuhama- ki nikagundua tumepata ajali mbaya.
Baada ya sekunde chache tena niliona Rodrik Chanda yule mhalifu na yule Mganda bwana Kiteba wanainuka wakiniuliza are you okay, nikasema my be. Chanda akasema ‘lets Go.’ Baada ya kuona hakuna askari anaeinuka wala ku- tikisika tulianza kuondoka.
Tulipotembea kama hatua kumi hivi bwana Rodrik Chanda alirudi tena kwenye gari na kuchukua silaha, ambazo ilikua ni bunduki aina ya SMG nne akasema twendeni hizi zina kazi huko mbele ya safari. Askari wote Saba waliokuwa kwenye ile Gari walifariki pale pale ilikuwa ajali mbaya ambayo ni vigumu kuielezea na hata sisi kupona ni mapenzi ya Mungu tu, sisi tulipona kwenye ajili hiyo bila hata mkwaruzo ilikuwa ni kama muujiza tu, na kwa kweli hilo tukio likanifanya nianze kuwa Sugu kiasi fulani.
Thomas Simkanga | 11

Tulipotembea mwendo wa saa moja pori kwa pori tangu tutoke pale kwenye ajali tulifika sehemu na gafla tu bila ya kutegemea, bwana Rodriki Chanda akatwambia simameni. Tukasimama akasema leta silaha hapa zile tulizo msaidia kubeba, akasema jamani ninyi mnanitia mkosi mtaacha nikamatwe kwa hivyo kila mtu ajue zake, tukamuomba sana asituache lakini akatutisha na bunduki, basi tukamwambia nenda tu mkuu. Baada ya kubaki Mimi na Kiteba kwa kiasi tuliona mambo sasa yamekuwa magumu sana kutokana na ugeni wetu kwenye lile pori na nchi ya watu kwa ujumla. Lakini kwa upande mwingine tuliona ni afadhali tumejitenga na jambazi sugu tukajisemea bila shaka matatizo yatapungua.
Tulianza tu kutembea kwenda mbele huku tukiwa hatujui tunakoelekea, Zam- bia bado ina misitu mingi sana ya asili mizito kwa hivyo ilikuwa ni vigumu sana kujua tunakoelekea, lakini bada ya mwendo wa kama saa moja hivi tuli- tokezea barabarani, tena barabara kuu iendayo Lusaka.
Mbele kidogo tuliona Gari aina ya Lori imepaki imeharibika watu wanaten- geneza, nilipata faraja baada ya kuona lile gari likiwa na namba ‘plate’ za Tan- zania. Tukalisogelea lile gari, na baada ya kufika pale nikaongea Kiswahili na wale jamaa wakaitikia vizuri. Jamaa wakaniuliza umefikaje hapo, nikawaeleza, na baada ya maelezo yangu mmoja akaingia ndani ya gari akatoka na gazeti moja la nchini Zambia linalotoka alasiri, juu kabisa likiwa limeandikwa polisi saba wafa kwa ajali wakiwa wanawasafirisha majambazi sugu.
Gazeti liliandikwa kwamba majambazi hao waliwaua askari waliokuwa wame- jeruhiwa kwa kuwamalizia na kisha kutoweka na silaha nne za kivita. Chini kulikuwa na picha zetu ambazo tulipiga siku ya kwanza wakati tupo pale kituo cha polisi siku ya kwanza tulipokamatwa.
Yule dereva wa lile lori alisema bwana mdogo najua inawezekana hujayatenda haya lakini sijui kama utatoka salama kwenye hii nchi, kwa kweli niliiona ha- tari iliyokuwa mbele yangu kuwa ni kubwa sana. Kwa kuwa tulikuwa hatujala muda mrefu, wale jamaa walitupa mkate na maji, wakatwambia kwamba wa- natarajia gari yao itapona usiku, na hivyo watatubeba nyuma ya Lori lao hadi Lusaka, na baada ya hapo tutajua wenyewe tufanyaje.
Saa sita usiku tulianza safari ya kutoka pale nahisi itakuwa ilikuwa ni karibu na maeneo ya mji wa Mpika kuelekea Lusaka. Hatukupata tatizo lolote njiani hadi Lusaka ambapo tulifika pale majira ya saa kumina mbili asubuhi, tukaachana
Thomas Simkanga | 12

na wale jamaa wa Lori. Kwa hivyo nilikuwa nimetumia siku sita kutoka Tun- duma hadi Lusaka safari ambayo ningeweza kutumia siku moja tu. Pia ilikuwa ni safari ambayo ilikuwa imeambatana na majanga na mikasa mingi sana na kibaya zaidi nilikuwa tayari nimeanza kutafutwa na polisi nikiwa naonekana hadi kwenye kurasa za mbele za magazeti.
Kwa hivyo kilichofuata hapo Lusaka ni kutafuta maeneo ya maficho na kuanza kujipanga kwa safari ya kuanza kuitafuta Harare Zimbabwe, kumbuka pamoja na majanga yote hayo sikuwa na wazo hata kidogo la kurejea nyuma nilikoto- ka yaani Tanzania.
Baada ya kukaa siku kama sita hivi siku ya saba tukapata Gazeti moja hivi liki- wa na habari kwamba yule jambazi tuliechana nae kule mstuni Rodrick Chan- da, ameuawa na polisi kwa kupingwa risasi wakati wanafanya majibizano ya Risasi na kikosi maalumu cha kupambana na majambazi, taarifa hiyo ilisema polisi wamejiridhisha kwamba wale wengine yaani mimi na yule Mganda ha- wakuwa majambazi isipokuwa walijikuta kwenye mtego baada ya kukamatwa pamoja na marehemu. Hata hivyo polisi itahakikisha inawatafuta, kuwakama- ta na kuwakomesha ili iwe fundisho kwa watu wanaoshirikiana na majambazi na wanaoingia nchini bila taratibu zilizowekwa kwa mjibu wa sheria.
Baada ya kusoma hilo tangazo tulipata moyo kwamba walau kosa letu sio la ujambazi sungu wala mauaji, tulikuwa tumejificha kwenye kitongoji cha John Lenge Compaund, wakati wote huo. Tulipoona kama kuna watu wanatufuatilia tukahamia kitongoji cha Kamwala vitongoji vyote hivi jijini Lusaka wanaishi watu wa kipato cha chini na vina watu wengi sana.
Tukiwa kamwala siku kama ya saba tangu tufike pale eneo letu lilivamiwa na polisi, kwa bahati nzuri mimi nilikuwa bafuni naoga niliposikia zile pu- rukushani nikaruka ukuta taratibu bila kishindo nikakimbia na sabuni zangu, hadi kwa dada mmoja hivi ambae yeye alikuwa ni Mmalawi ambae aliwahi kuishi Mbeya, aliitwa Anne, akanificha chumbani kwake, sikuwa na wasiwasi sana kwa sababu yule Mganda sikuwahi kufika nae pale. Mganda akawa ame- kamatwa Mimi nikaserve lakini nikajua nafuatiliwa sana na polisi, nikakaka pale kwa yule dada kwa wasiwasi sana kwa muda wa siku nne, nikaona hap- ana hapa polisi wanaweza kurudi nikamtuma yule dada kule tulikokuwa tuna kaa mwanzo akaenda kunichukulia kibegi changu ambacho nahisi polisi ita- kuwa walikiacha kama chambo. Nilipo pata kile kibegi usiku ule ule nika Hama
Thomas Simkanga | 13

kwenda Linda Compaundi, Kwa rafiki yake na Anne mdada mwingine alieitwa Muwanga.
Nikakaa pale kwenye room moja, tunalala kama vile mume na mke lakini hatukuwa na hayo mahusiano, kwa hivyo tulikuwa tunalala tu, nakumbuka siku moja lilikuja danga lake ikabidi niwapishe nikae nje kwa masaa mengi tu, walipomaliza mambo yao nikarudi kulala palepale kitandani “kuna wakati maisha huhama kabisa kwenye utaratibu wa kawaida, na huwezi kugundua kuwa yamehama”.
Baada ya siku tano tangu nitoke kule kwa yule dada Anne maeneo ya Kawabwa, siku ya juma pili kukiwa na utulivu wa kutosha kabisa askari walifika kwa dada Anne na kumkamata kwa sababu walidai kwamba wamepata taarifa kwamba yeye ndie aliekwenda kuchukua lile Begi langu la nguo. Baada ya kukamatwa kutishwa na kupata kipigo kidogo alikiri madai hayo na pia akakubali kuwa- onesha sehemu niliyokuwa nimejificha.
Siku hiyo hiyo jioni polisi waliongozana nae kutoka Kawabwa compound kuja eneo la Linda compound sehemu ambapo nilikuwa, aliwaongoza moja kwa moja hadi kwenye nyumba ndogo yenye muonekano kama kibanda hivi pem- beni ya nyumba nyingine, tulikuwa ndani na dada Muwanga, bahati nzuri tu- likuwa tumefunga Mlango.
Kwa hivyo Polisi walipofika kwenye hiyo nyumba ilibidi wagonge mlango, ku- tokana na namna mlango ulivyogongwa kwa nguvu nikamwambia yule dada asiufungue. Nikaenda kwenye kiupenyo kidogo pembeni ya mlango, nilipo- chungulia nikaona Askari watatu mmoja akiwa na silaha bunduki aina SMG. Pembeni kidogo nikamuona dada Anne nikajua tayari hapa nimeshasalitiwa na mlengwa ni mimi. Nikarudi ndani, akili ikazunguka haraka, moyoni nikase- ma siwezi kukamatwa kirahisi na kizembe namna ile, wakati nawaza hivyo nje ikasikika sauti ya askari akisema fungua mara moja usipofanya hivyo tunavunja.
 
Sehemu ya 4


Polisi wakiwa wanaendelea kugonga mlango kwa nguvu huku wakitishia kuuvunja mlango, haraka haraka nilimwambia yule dada aitikie kwamba karibu nakuja tunafungua, wakati polisi wanasubilia kufungua nikamua-
muru yule dada anipe gauni lake refu na ushungi na kitege akanipa namimi kwa haraka sana bila ya yule dada kujua nataka kufanya nini, nikalivaa lile gauni haraka, nikafunga ushungi kichwani na kisha nikajitanda kitenge.
Nikamuamuru tena yule dada alale na ajifunike mwili wote kwa blanketi, kisha nikauendea ule mlango taratibu,huku naiga sauti ya yule dada na kusema kari- buni jamani kuna nini tena, polisi hawakuwa na habari na mimi waliingia wote ndani kwa kasi wakijua wananiwahi mimi kule ndani, hawakujua kuwa mleng- wa wao ndio nimepishana nao mlangoni. Nikazunguka nyumba nikaingia kwenye vichochoro na kwa kuwa Linda compound ni nje kidogo ya mji wa Lusaka haikuchukua muda nikalikamata pori, nikavua zile nguo za yule dada, nikazitupa korongoni nikaendelea kukata mbuga.
Ndivyo nilivyopona kwenye mikono ya polisi wenye hasira kali, sikujua kilicho endelea kwa wale wadada wafadhili wangu ila wakati natoka nilisikia milio ya bunduki kama risasi tatu hivi zilisikika, sina uhakika kama waliuawa au zilipig- wa juu kunitisha mimi.
Baada ya kutembea saa nzima mwendo wa kawaida kabisa nikiwa peke yangu safari hii bila yule Mganda (Chiteba) ambae alikuwa amekamatwa na polisi, nilitokeza kwenye barabara ya njia kuu iendayo Harare Zimbabwe, nikaona nikianza kuifuata kwa miguu nitakamatwa na nikipanda gari pia nitakamatwa, nikaamua kuiacha barabara na kurudi porini. Lengo langu lilikuwa ni kuson- gea mbali na mji wa Lusaka.
Nikatembea umbali mrefu hadi sehemu Moja hivi inaitwa Chikakanta mission umbali wa kama Km 141 kutoka Lusaka, ilikuwa safari ya masaa 11 bila kula wala kunywa, hakika nilichoka sana. Lakini nia ya kufika Johannesburg Afrika
Thomas Simkanga | 15

ya kusini ilikuwa palepale, pamoja na shida na tabu nia yangu haikupungua hata kidogo.
Ili nisikamatwe nilipofika Chikakata Mission nikajifanya natafuta kazi kwenye mashamba ya wazungu ambao ndio wakulima wakubwa katika maeneo yale, nikapata kazi ya kibarua kwa mzungu mmoja hivi alieitwa Joe, nilifanya hivyo ili nisome ramani ya safari yangu kwa siku kadhaa na pia nipate fedha kidogo, hadi hapo nilikua nimebaki na K 400,000 tu ambazo zingeweza tu kunifikisha Harare Zimbabwe, pesa yangu nyingi ilitumika wakati wa pirika pirika za Lu- saka. Yule mzungu aliniahidi kwamba iwapo nitafanya nae kazi vizuri atanilipa K 700,000 kwa mwezi.
Basi nikaanza kazi pale kazi ngumu ya kusawazisha matuta yanayolimwa na trekta ili kuwe na level moja. Tunaamka saa 12 asubuhi tunafunga kazi saa 10 jioni, kila siku, nilifanya kazi mwezi mmoja pale yule mzungu akaniita aka- niambia nataka nikubadilishie kazi nimeona wewe ni kijana makini sana. Kwa hivyo nataka tufanye dili, nikapewa maelezo marefu kuhusu hilo dili ndipo nikaelewa kwamba mzungu anataka tufanye biashara ya mihadarati, yaani niwe punda wake. Niliambiwa kwamba anataka aniunganishe kwa vijana wake wanao safirisha mzigo kati ya Afrika kusini, Angola, Mozambique, Zimbabwe, Malawi na Dar es salaam.
Baada ya kupewa maelekezo kwa kina nilikubaliana na dili hilo hatari, saba- bu ilikuwa moja tu moyoni mwangu niliona kwa kufanya hivyo yule mzungu atakuwa amenirahisishia kufika Afrika Kusini bila ya kutegemea na ya yeye kujua. Nilimuelezea mikasa yangu yote hadi kufika pale, cha ajabu pamoja na kwamba nilimwambia natafutwa na polisi alifurahi sana, akaniambia anataka watu kama mimi ambao ni makini na wanatumia akili kama mimi.
Baada ya wiki hivi vijana wake walio kuwa wameenda kufuata mzigo Afrika ya kusini walirejea wakiwa na mzigo wa kutosha. Walipokewa kishujaa sana na bosi na kufanyiwa pati ya kishua sana usiku ule ule, kisha bosi alinitambulisha kwa wale jamaa, akawambia wakae na mimi wiki moja ili wanipe mafunzo ya kanuni za kazi na ukakamavu, baada ya hapo waungane na mimi tupeleke mzigo Tanzania kupitia Malawi.
Safari hii sikuifurahia sana kwa sababu ilikuwa inanirudisha Tanzania tena kwa huu utaratibu wa kazi yangu mpya, nilidhani tutaanza na safari ya Afrika ya kusini na nilipanga kwamba nikifika nitawatoroka kabla sijatambulishwa
Thomas Simkanga | 16

kwa mafaza lord wa kule unajua unapofanya kazi hizi za madawa ya kulevya na hawa watu ikitokea ukitoroka lazima utauawa. Nikapiga moyo konde kwamba tukirudi bila shaka uelekeo utakuwa wa Afrika ya kusini.
Siku ya safari ilifika tukachukua mzigo wa thamani ya $ 70,000 Ilikuwa huo mzigo tukaukabidhi Mbeya kwa father mmoja hivi, ambae alikuwa ndio msam- bazaji huko east afrika. Safari ilianza saa 11 alfajiri tukiwa tunatumia gari aina ya Toyota V-8, ilikuwa gari nzuri sana ambayo hata polisi kuisimamisha ikiwa barabarani sio rahisi sana kwani wasipo ona plate no wanawea kuzani ni ya kiongozi mkubwa serikalini.
Kitu ambacho niliona sio cha kawaida ni kwamba kwenye ile gari tulikuwa na plate namba za TZ, Malawi na Zambia. Hivyo wakati tunatoka pale tulitumia plate namba za Zambia. Umbali wa kutoka Lusaka hadi Lilogwe Malawi ni Km 716.4 kwa hivyo tulitarajia kufika boda ya kasumulo upande wa Tanzania siku hiyo hiyo na mbeya tungefika usiku. Safari ilikuwa salama kabisa kuto- ka Lusaka hadi boda ya Malawi eneo Linaloitwa Chipata, baada ya kuvuka boda umbali kidogo tu tulibadilisha plate number tukafunga za Malawi safari ikaendelea.
Tukatembea kama saa moja hivi tukafika Lilogwe, Tukapata chakula kisha sa- fari ikaendelea kuitafuta kasumulo ambapo pia sio mbali sana, tulipo tembea mwendo wa kama Km 30 hivi, dereva akatwambia nyuma kuna gari ya polisi inatufatilia anaikumbuka mara ya mwisho walipopita ile njia iliwafukuzia lakini ni bahati tu waliwahi kuingia ardhi ya Zambia. Kwa hivyo itakuwa walikuwa wameweka mtego, akaongeza mwendo tukaicha mbali sana kisha yule mkuu wetu wa safari akasema inabidi watu wawili washuke na mzigo waingie porini halafu gari einde mbele kisha ipunguze mwendo polisi iwakute ikisha mal- izana nao watawarejea ili kuendelea na safari. Ikaamuliwa nishuke Mimi na jamaa mwingine alieitwa Jim.
Tukaingia porini gari ikaondoka na watu watatu, sisi tukabaki pale tukaingia porini umbali wa mita 300 hivi kutoka barabarani. Tukatulia kulikuwa na msi- tu mkubwa sana na hilo eneo halikuwa na mawasiliano yoyote. Kwa mbali tukaona gari ya polisi imepita kwa kasi sana, tukatulia ili tujue kitakachotokea mbele. Baada ya Kama dk 20 hivi zikarudi Gari zote yaani ya polisi na ile yetu. Gari yetu ilikamatwa na polisi kwa kosa la kutumia plate namba bandia kwa hivyo walikuwa wanapelekwa polisi, pia walikuwa na kosa lingine la kuende-
Thomas Simkanga | 17

sha gari katika nchi nyingine bila vibali. Kwa bahati nzuri wale jamaa tayari walikuwa na passport, katika ule msafara ni mimi tu ambae nilikuwa bado sina passport.
Tukaachwa porini na bwana Jim tukiwa na mali ya $ 70,000 mabosi wetu wakarudishwa Lilogwe chini ya ulinzi wa polisi. Hatukuwa na mawasiliano yoyote, tulichokuwa nacho ni pesa $ 50 kila mmoja ambazo tulipewa kwa ajili ya kujihami
 
Back
Top Bottom