Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Jaman habari zenu , naombeni ushauri juu ya njia nzuri zaidi kiafya ya uzazi wa mpango maana naskia nyingine zina madhara plz naombeni msaada mwanangu bado mdogo na shemeji yenu anataka kitu.
 
Mi ninayo ya asili na haina madhara naiuza laki na nusu. ukihitaji njoo inbox
 
Kila mkingonoka nawa mikono maj ya barid pia zle sehemu zetu osha na maj ya bard kabla ya nusu saa..
 
.Njia ya unyonyeshaji hii inafaa kwa wale huwa hawapati siku zao kabisa maadamu wanamnyonyesha mtoto.
.Njia ya kalenda .
 
Ndugu wanajamvi mimi ni mwanaume nina umri wa miaka 34 nataka kufunga kizazi changu nina watoto 6. Baadhi ya watu wanasema kama nitafunga kizazi nitakufa mapema saaana naombeni ushauri ndugu yangu kwani naona nikiendelea kuzalisha nitawatesa watoto wangu na nisingependa mke wangu atumie uzazi wa mpango...tafadhali msaaada
 
swali zuri sana nipo makini kufatilia majibu pengine yakanifaa muda utakapofika watoto wakinitosha
 
MziziMkavu na wengine wajuzi tafadhali msaada kwa bwana huyu na.wengine wenye hitaj kama lake
 
Last edited by a moderator:
Mwanamke aliyetumia sindano za uzazi wa mpango humchukua mda gani kupata ujauzito pindi aachapo kutumia?

Inatarajiwa aweze kurudi katika hali ya kawaida miezi mitatu baada ya kuacha kutumia (tangu sindano ya mwisho), kwa maana ya kwamba kuwa na uwezo wa kubeba ujauzito.Hata hivyo baadhi(wachache) huchelewa kidogo kubeba ujauzito, uchelewaji huu hauwezi kuzidi miezi 24(miaka miwili).
 
Muache mke wako mwenyewe ndo aje aulize tumpe dozi yake, wewe janaume ungeuliza swali kama hili "mwanaumwe mpiga punyeto inamchukua mda gani kuja kuzalisha?
 
Mwanamke aliyetumia sindano za uzazi wa mpango humchukua mda gani kupata ujauzito pindi aachapo kutumia?

Inatarajiwa aweze kurudi katika hali ya kawaida miezi mitatu baada ya kuacha kutumia (tangu sindano ya mwisho), kwa maana ya kwamba kuwa na uwezo wa kubeba ujauzito.Hata hivyo baadhi(wachache) huchelewa kidogo kubeba ujauzito, uchelewaji huu hauwezi kuzidi miezi 24(miaka miwili).
 
Habari zenu binafsi,
Natamani wanangu wapishane miaka kuanzia mitatu(3) ila sijui ni njia gani iliyo salama kwa uzazi wa mpango. Nimekutana na wanawake wanaotumia sindano, vidonge, kitanzi, vijiti na hata condom. ingawa wanaume wengi hawapendi kutumia condom. katika wanawake wote hao kila mmoja ananiambia madhara ya njia yake. Lakini pia sikuishia hapo niliwahi kwenda kwa Dr. mmoja akasema "sikushauri kutoa mimba ila ni bora kutoa mimba kuliko kutumia uzazi wa mpango".
Naomba mnijuze wajuvi njia ipi iliyo salama..?
 
attachment.php

Tembe za uzazi wa mpango kwa mwanaume zazinduli, zatokana na mti huu wa Gendarusa

Wanasayansi wanadai kuwa dawa mpya iliyozinduliwa ya mpango wa uzazi kwa wanaume imefanikiwa kwa asilimia 99.

Dawa hio imetengezwa kutoka kwa mmea ujulikanao kama Gendarusa ambao wanaume wa kisiwa cha Papua wamekua wakitumia kujizuia kuwashikisha wake zao mimba.

Mmea huo unasemekana kuwa na madini ambayo yanatatiza uwezo wa mbegu za kiume kuzalisha kwa kuzimaliza nguvu na pia kuzifanya kutoweza kuingia katika mayai ya mwanamke.

Profesa Bambang Prajogo, mtafiti mkuu wa mradi huo anasema ana furaha sana kuripoti kwamba dawa hio itaanza kuuzwa mwaka 2016 baada ya miaka mingi ya utafiti na majaribio.

Ingawa dawa hio ya mpango wa uzazi kwa wanaume ina athari zake, kama vile wanaume kuongeza uzazi wanapoitumia wanasayansi wanaamini kuwa athari hizo ni ndogo sana ikilinganishwa na dawa zinazotumiwa na wanawake kwani hauthiri sana homoni zao.

Dawa hio inaweza kumezwa saa moja tu kabla ya tendo la ndoa. Lakini wazee wa jamii hio huchanganya dawa hio na chai na kuinywa dakika thelathini kabla ya tendo la ndoa.

Hata hivyo wanaume wanaambiwa wasiwe na wasiwasi kwani wanapata uwezo wa kuzalisha tena siku thelathini baada ya kusitisha utumizi wa dawa yenyewe.

Chanzo: BBC
 

Attachments

  • IMG_65189797324887.jpeg
    IMG_65189797324887.jpeg
    90.2 KB · Views: 1,420
Back
Top Bottom