Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Kunywa mbegu ya nyonyo moja ukimaliza bleed kila mwezi
 
Ongea na mwenza wako asiwe anamwagia ndani ni nzuri ikiwa tu ni mwelewa ingawa ina risk, umeikataa kalenda ila ndo njia best kuliko zote kwa mtu asietumia za hosp.
Sijaikataa hakika, ila imenishinda Mkuu imenishinda kabisa maana niseme ukweli tungeizingatia nisingeingia kwenye jukumu la malez ya hivi, yanatesa sana
 
Sijaikataa hakika, ila imenishinda Mkuu imenishinda kabisa maana niseme ukweli tungeizingatia nisingeingia kwenye jukumu la malez ya hivi, yanatesa sana
Sasa utatumia njia ipi na ya hosp huzihiitaji?? Za asili? Kama za asili kuna ile ya mbegu ya mnyonyo ule kama mwekundu unakua unameza kila unapomaliza hedhi. ( hii niliiisikia ila sipo sure...)
 
Sasa utatumia njia ipi na ya hosp huzihiitaji?? Za asili? Kama za asili kuna ile ya mbegu ya mnyonyo ule kama mwekundu unakua unameza kila unapomaliza hedhi. ( hii niliiisikia ila sipo sure...)
Ntaitafuta Mkuu nijaribu, asante
 
Kwani ina maana mwanamke anayenyonyesha HAWEZI kupata mimba? Mbona nasikiaga mwanamke kapata mimba huku ananyonyesha? Mwanamke anaanza lini kubleed baada ya kujifungua?

Hizi njia za kuzuia mimba zinachanganya sana!

Suala la uzazi kila mwanamke analiexperience kivyake, wapo baadhi anapokuwa ananyonyesha hawez pata mimba, ila wengine wanapata.
Kubleed baada ya kujifungua hakuna specific time na hakuko constant, kila mwanamke anaexprience kivyake
 
Dawa inayotolewa kwa njiya ya sindano imetajwa kama mafanikio makubwa ya njia ya uzazi wa mpango kwa wanaume. Watafiti kutoka Marekani wamesema dawa hiyo imefikia asili mia 96 ya mafanikio baada ya kufanyiwa majaribio miongoni mwa wanaume 270.
xsperm-pic-bbc-69434379.jpg.pagespeed.ic.UyI0yB4Lf0.webp


Kati ya wanaume hao ni wanne pekee walioweza kuwafanya wenzi zao kutunga mimba. Hata hivyo dawa hiyo imeripotiwa kuwa madhara mengi miongoni mwa wanaume ikiwemo vipele usoni na kuwa na usununu. Watafiti wamekua wakitafuta dawa ya kupanga uzazi ya wanaume kwa miaka 20.

Wataalamu hao wamekua wakitafuta jinsi ya kupunguza idadi ya manii bila kusababisha madhara ya uzazi. Kimaumbile wanaume hutoa manii kila wakati na wanasayansi wamekua wakitaka kupunguza idadi kutoka milioni 15 hadi milioni moja.
Image caption Dawa mpya ya mpango wa uzazi kwa wanaume

Utafiti wa dawa hii ulilenga wanaume kati ya umri wa miaka 18 hadi 45, na walio na uhusiano na mwenzi mmoja wa kike. Walishiriki kwenye utafiti huo kwa mwaka mmoja. Walidungwa sindano hiyo na kupunguza idadi ya manii hadi milioni moja. Kisha hawakupokea dawa hiyo ili kubaini kasi ya kuongezeka kwa manii yao hadi milioni 15.

Baadhi walisema iliwachukua mwaka mmoja kabla ya idadi kamili na inayotakikana kurudi. Baadhi ya madhara kama vile mfadhaiko, usununu, vipele usoni na maumivu ya misuli yalisababisha wanaume 20 kujitoa kwenye utafiti. Mtafiti mkuu wa dawa hii Dkt. Festin amesema wanaangazia njiya nyingine ya kuboresha dawa hiyo ikiwemo kuiotoa kama mafuta.

Source:BBC
 
nimejifunza kuhusu hii mada njia bora ni kalenda peke ake mbarikiwe
 
HABARI wanajamii nilikuwa nasikiliza chombo kimoja cha habari kuhusu athari za njia hii ya kuzuia mimba ijulikanayo kama VASCATOMY yaani mirija ya mwanaume hufungwa ili isipitishe mbegu za mwanaume kuwa haina madhara ya kiafya kwa mwanamme.

Je ni kweli wanajamii na je ni njia gani nyingine ambayo inaweza kuwa safe kwa watumiaji kwa kuzuia mimba na kiafya .
 
Back
Top Bottom