Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

Uzazi wa Mpango - Njia za kuzuia, aina ya Uzazi wa mpango na ushauri

HBARI wanajamii nilikuwa nasikiliza chombo kimoja cha hbari kuhusu athari za njia hii ya kuzuia mimba ijulikanayo kma VASCATOMY yaani mirija ya mwanaume hufungwa ili isipitishe mbegu za mwanaume kuwa haina madhara ya kiafya kwa mwanamme .Je ni kweli wanajamii na je ni njia gani nyingine ambayo inaweza kuwa safe kwa watumiaji kwakuzuia mimba na kiafya .
Nitafute mimi nikupe dawa ya Asili ili mpenzi wako au mke wako asiweze kushika mimba mpaka muda munaotaka.Ukihitaji dawa ya uzazi wa mpango ya Asili isiyokuw ana amdhara,Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Elimu ya uzazi wa mpango bado haijawafikia vijana wengi sana hasa tanzania, wengi wao hudhani labda
matumizi ya dawa na njia za uzazi wa mpango ni kwa ajili ya malaya, watu waliokwisha zaa na kadhalika. lakini hii sio kweli kwani njia hizi ni nzuri kwa rika zote yaani vijana na watu wazima ambao wanashiriki ngono ila kwa sasa hawako tayari kupata mtoto.

kutotumika kwa njia hizi kumesababishwa kuzaliwa kwa watoto wengi ambao hawakupangwa, kujiua kwa wasichana kwa kukwepa aibu na utoaji wa mimba wa mara kwa mara.
utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba msichana akiingia kwenye mahusiano kwa miaka mitatu bila kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango anaweza kutoa mimba nne mpaka tano lakini pia asilimia kubwa ya wanachuo wa tanzania ambao huingia kwenye mahusiano vyuoni hawawezi kumaliza chuo bila kutoa mimba hata moja.

kuna njia nyingi sana za uzazi wa mpango ikiwemo vitanzi, vijiti, kondomu,kutumia kalenda, sindano,vidonge, upasuaji wa kufunga mirija na kadhalika. kondomu ni njia bora sana kwani huzuia ukimwi na mimba pia lakini ukweli ni kwmba kama kondomu zingekua zinatumika vizuri basi hao watoto tusingewaona mtaani hivyo kama wewe hauko tayari kuzaa sasa hivi kwa sababu yeyote ile nakushauri utumie njia ya kijiti.

njia hii ikoje?
kijiti cha plastiki chenye homoni za uzazi huwekwa kwenye mkono wa mwanamke, homoni ndani ya kijiti hicho huzuia mimba kwa kwa kuzuia yai kutoka kwenye kiwanda yaani ovari kwenda kwenye kizazi . kijiti hiki huwekwa bure kwenye hospitali zote za serikali tanzania.

kwanini njia hii ni bora kuliko zote?

hurudisha uwezo wa kuzaa haraka: kama unatumia kijiti hata kama kiliwekwa wiki iliyopita, ukibadilisha mawazo ukataka mtoto kinatolewa na mwezi huohuo unapata mtoto, tofauti na njia ya sindano ambayo ukichomwa leo kuna uwezekano wa kukaa mpaka miaka miwili bila kupata mtoto.

ni rahisi kutumia: kijiti hiki kikishawekwa hospitali huhitaji kukumbuka chochote tofauti na vidonge ambavyo wakati mwingine mtu huweza kusahau asimeze akajikuta amebeba mimba.

inafanya kazi kwa muda mrefu sana; kama wewe ni binti mdogo au wewe ni mama ambaye una mtoto tayari na hauhitaji mtoto kwa sasa njia hii ni nzuri kuliko zote kwani huweza kuzuia mimba kwa miaka mitano mfululizo kwa asilimia mia.

haiingilii utoaji wa maziwa ya mama; vidonge vya uzazi wa mpango vyenye homoni zote mbili yaani oestrogen na progesterone kitaalamu kama microgynon huweza kupunguza wingi wa maziwa kwani wingi wake kwenye mfumo wa binadamu husababisha kupungua kwa homoni ya maziwa kitaalamu kama prolactin hormone.

haiongezi uzito; inaaminika vidonge vya uzazi wa mpango huongeza uzito kwa kuzuia kiasi kikubwa cha maji kisitoke ndani ya mwili kwa njia ya mkojo na pia kuongeza hamu ya kula, lakini utafiti kwa wanaotumia vijiti haujaonyesha madhara haya.

muda zaidi wa kushiriki tendo la ndoa: matumizi ya kijiti huzuia kutoka kwa damu ya kila mwisho wa mwezi ambayo kwa wengine huambatana na maumivu makali na kukosa raha ya kushiriki tendo la ndoa hivyo ukitumia kijiti utapata faida hii.damu inaweza ikatoka hata mara mbili kwa mwaka tu.

sio rahisi kwa watu wengine kujua: wasichana wengi hasa vijana hawapendi maisha yao ya ngono yafahamike, na hasa njia hizi za uzazi wa mpango watu wakijua unatumia wanakuona muhuni, kitu ambacho sio kweli, hivyo matumizi ya kijiti ni siri sana na sio rahisi kwa watu wengine kujua tofauti na vidonge ambavyo sio rahisi kuvificha.

mwisho; utafiti unaonyesha utoaji wa mimba umewanyima wanawake wengi watoto, msanii maarufu wema sepetu ambaye kwa sasa anatafuta mtoto kwa shida sana aliwahi kukiri kwamba aliwahi kutoa mimba zamani kidogo na huenda anajutia maamuzi yake.hivyo kama wewe ni msichana mdogo na hutaki kuzaa kwa sasa au wewe ni mama hutaki mtoto mwingine kwa sasa tumia njia hii ya uzazi wa mpango itakusaidia sana.
 
Inaweza kuwa njia nzuri,as an the kutufahamisha lakini kuzuia damu ya hedhi isitoke nawakati ni uchafu umbao utarundikana ndani ya tumbo haiwezi kuleta matatizo baadae.?
 
Njia hii bado ina maudhi kwa baathi ya wanawake mana hutumia mfumo wa hormone.....kwangu mimi njia bora ni kuweka loop(IUD) japo wanaweke wengi huogopa njia hii.

Kwa wanandoa nashauri kutumia kalenda(kama mwanamke mzunguko wake ni wa siku 28 hadi 30) na kondomu za dharula kwenye kabati lenu zisikosekane.
 
Inaweza kuwa njia nzuri,as an the kutufahamisha lakini kuzuia damu ya hedhi isitoke nawakati ni uchafu umbao utarundikana ndani ya tumbo haiwezi kuleta matatizo baadae.?
Huo uchafu na dam unaozungumzia ni yai lililopasuka na kuharibiwa na hormone baada yakukaa mda mrefu kwenye mirija ya uzazi bila kurutubishwa,

lilitoka kwenye kiwanda cha ovari ad kwenye mirija(fallopian tubes) ili lirutubishwe na mbegu za kiume kabla yakutua mfuko wa uzazi,

hivo ukitumia njia ya kijiti inazuia yai kutengenezwa kwenye kiwanda cha ovari hivyo hakutakua na uchafu wa kutoka maana uchafu ni yai lenyewe lililozuiliwa kutengenezwa kiwandan
 
Hapo tu kwenye kuzuia hedhi isitoke ndo hiyo njia imekuwa mbaya.
Yaani mwaka mzima two times sasa hiyo miezi yote inayobaki huo uchafu unaenda wapi?
 
Njia niipendayo na mara zote nimekuwa nikiitumia ni njia ya kutumia kalenda.
 
Huo uchafu na dam unaozungumzia ni yai lililopasuka na kuharibiwa na hormone baada yakukaa mda mrefu kwenye mirija ya uzazi bila kurutubishwa,

lilitoka kwenye kiwanda cha ovari ad kwenye mirija(fallopian tubes) ili lirutubishwe na mbegu za kiume kabla yakutua mfuko wa uzazi,

hivo ukitumia njia ya kijiti inazuia yai kutengenezwa kwenye kiwanda cha ovari hivyo hakutakua na uchafu wa kutoka maana uchafu ni yai lenyewe lililozuiliwa kutengenezwa kiwandan
umemaliza yote...mimi sitii neno lingine hapo
 
Inaweza kuwa njia nzuri,as an the kutufahamisha lakini kuzuia damu ya hedhi isitoke nawakati ni uchafu umbao utarundikana ndani ya tumbo haiwezi kuleta matatizo baadae.?
Hapana haileti madhara haya...madhara machache kwa baadhi ya watu ni ya kihormonal tu
 
Njia hii bado ina maudhi kwa baathi ya wanawake mana hutumia mfumo wa hormone.....kwangu mimi njia bora ni kuweka loop(IUD) japo wanaweke wengi huogopa njia hii.

Kwa wanandoa nashauri kutumia kalenda(kama mwanamke mzunguko wake ni wa siku 28 hadi 30) na kondomu za dharula kwenye kabati lenu zisikosekane.
Mpira kwa wanandoa haijakaa vizur lkn, we unaonaje...mkipalamiana jikon au bafuni au knye korido (if u know wat i mean) inakuwa shida kuzitafuta hizo kondom pia unakuwa kama upo na mchepuko tu
 
Calendar and withdrawal Ndo njia salama nyingine zote zinausumbufu wake japo inategemea mtu na mtu mwingine kwake Nzuri Kwa mwingine ni shida na mpka uje upatie hii ndo Nzuri kwako ni changamoto
 
Wakuu,naomba kueleweshwa njia nzuri za uzazi wa mpango.
Naogopa nisije bebanisha watoto kama timu ya mpira.

Njia nizisikiazo ni kama vile SINDANO,VIJITI AU KITANZI na VIDONGE
ila faida na hasara ya njia hizo ndo sizijui.

hii ya kupanga kalenda kwa kuangalia siku za mwanamke inanichanganya,naomba nielekezwe nayo!

Natanguliza shukrani zzangu kwa imani kuwa tatzo langu limetatuliwa.
 
Kalenda inasemekana kuwa ni njia salama ukiweza kuifuata......

Sindano hapana...
Vidonge hapana....
Kitanzi nimesikia jana kutoka kwa mtu wangu wa karibu kuwa kimemletea shida ya tumbo ila alivyotoa halimuumi tena.....

Kijiti labda
 
Nashukuru sana [HASHTAG]#Manka[/HASHTAG].
 
Kuna mtu nimekutana nae alilazwa Kwa ajili ya tumbo akaambiwa kitanzi kimemchimba kizazi wamempiga masindano ya kutosha antibiotics wamemwambia pakipona wanamtoa. Na anadai ameweka Kama miezi mitatu tu
 
Kijiti side effect yake utableed heavily tena mabonge bonge so sikushauri. My sis and some of my pals tried it, ilibidi watolewe. Nenda marie stopes mwenge utapata maelezo zaidi kutoka kwa gyno na atakupima on which method will fit u best. E.g. kama you are above 34, wanashauri uache vidonge.
 
mh,inamaana mkuu there is no method that can be suitable to all?
 
Back
Top Bottom