Uzee: Maana, kuzuia uzee wa mapema,changamoto na jinsi ya kuwatunza wazee

Uzee: Maana, kuzuia uzee wa mapema,changamoto na jinsi ya kuwatunza wazee

Habari za asubuhi wapendwa,

Kuna wakati nilipata mwaliko wa kwenda nchini Uganda, tulifika Kampla na kupokelewa na mwenyeji wetu. Tulikuwa kikundi cha watu watano, tulipelekwa kwenye hoteli tuliyoandaliwa na kuambiwa tujiandae, baada ya masaa mawili mwenyeji wetu atarudi kutuchukua kwa chakula cha jioni.

Nyumbani kwa mwenyeji wetu ile karamu ilikuwa ya kukata na shoka, kulikuwa na vyakula vingi kuanzia; matoke, wali, samaki sato, nyama ya mbuzi (choma), mbuzi mchuzi, chapati, salad, matunda, nuts na vinginevyo. Katika kujitengea chakula, kaka mmoja nilimuona anakula salad tu, baada ya chakula tulijiwekea matunda na story za hapa na pale ziliendelea.

Baadae niligundua kaka yule ni daktari, alinifahamisha alipata scholarship baada ya kumaliza form six kwenda kusoma medicine China, alipofika kule aliamua kubadili na kusomea Chinese Medicine na katika process ya kusoma herbs ndiyo aligundua uharibifu wa chakula katika harakati za mapishi mpaka kumfikia mlaji.

Daktari yule aliniambia kwa miaka takriban 25 ameacha kula chakula kilichopikwa, alipoanza ilikuwa ngumu lakini sasa hivi hawezi tena kula chakula chochote kilichopitia moto. Kwa muonekano yule daktari anaonekana ana miaka 35, nilishangaa aliponiambia ameshagonga 50 kama miaka miwili iliyopita.

Dieat yake:
Breakfast; embe na ndizi mbivu au papai na ndizi mbivu pamoja na kikombe cha mchanganyiko wa nuts hii ndiyo supplement ya protein. Chai na kahawa ni sumu kubwa ya mwili, kunywa maji tu ukimaliza kula hivyo. Kwasababu digestion ya matunda ni haraka, hakikisha una matunda yaliyotaarishwa na unaweza kula baada ya saa moja au masaa mawili.

Lunch;
Kabich lililokatwa katwa, matango (cucumber), nyanya, unaweza kuweka limao kwa ladha pia ni source ya vitamin C, vipande vya mhogo au viazi vitamu unatafuna vibichi na kikombe cha mchanganyiko wa nuts unamalizia na maji.

In between hakikisha unaandaa matunda na cucumber kama bites kwasababu digestion inakwenda haraka.

Dinner;
Carrots zilizokatwa katwa, kachumbari ya nyanya kitunguu na cucumber unanyunyiza olive oil kijiko kimoja cha chakula, nanasi na kikombe cha mchanganyiko wa nuts na glass ya maji.

Wengine wanafanya water therapy yaani in between meals wanakunywa maji haya yanasaidia pa kutokusikia njaa.

Ukianza hivyo hutaweza kuwa na excess fat.
Hiyo ni nzuri,ila nyie wadada wetu wa kibongo bila ya kitambi hamtuelewi,wacha tu tule mi ugali na nyama choma.
 
Mugabe mwenyewe amegonga miaka 93 juzijuzi lakini tangu utotoni anakula chakula iliyopikwa
 
Ukila hivyo hauto kufaaa au? Maana kama kifo bado kipo palepale no need ya kujinyima kiasi hicho. Ponda raha kifo chajaaaa
 
Haya haya vitambi mbinuko mupoo sasa sky dinner ujamalizia nawaza kuagana na masontojo muulize bia anakunywa? [emoji22]
 
unajinyima ivyo alafu baada ya miaka mitatu unakufa kwa uzembe wa dereva wa bodaboda
 
Nijuavyo mimi, uzee ni 'matter of age' na siyo 'physical appearance'.
Diet kama hiyo inasaidia 'usionekane mzee' ingawa uzee hausimami.
 
Kwa mlo huo sidhani kama anaweza kupiga show za kibabe..huo mlo tegemea kuwa goigoi tu
 
Hahaaaaaaaaaaaa huyo mjamaa ukimpa shoka na kigogo chenye ukubwa wa mkono wake hapasui haki ya nani.
Hivyo n Vyakula Vya Ku maintain body na sio kuupa mwili nguvu
Xx kwa mtu ka mm Mzee wa kazi za mitulinga unanilisha kabeji na tango half nikapakue mifuko mia ya cement Kwe semi trela kweli ?????. Huu utani
 
KAMUGISHA: Uzee ni mtihani, kila mtu hutaka kuishi miaka mingi ila hakuna atakaye kuitwa mzee

NA FAUSTIN KAMUGISHA

KUNA methali ya taifa la Iceland isemayo kuwa, kila mmoja anataka kuishi maisha marefu, lakini hakuna anayetaka kuitwa mzee.

Katika maisha utajitahidi kula mlo kamili, kufanya mazoezi, kupumzika, kujitunza vizuri kwa muda wa miaka sitini mwisho wa siku, funga fungua uzee unaingia. “Uzee hasa uzee unaoheshimika, una mamlaka makubwa, na una thamani kubwa kuliko raha zote za ujana,” alisema mwanafalsafa Cicero.

Mtunga-zaburi aliimba hivi kuhusu wazee waaminifu: “Bado wataendelea kustawi wakati wa kuwa na kichwa chenye mvi, wataendelea kuwa wanono na wabichi” (Zaburi 92:14).

Licha ya utukufu wa uzee, uzee ni mtihani. Katika uzee watu wanapoanza kusema kuwa unaonekana kama kijana ni namna nyingine ya kusema umezeeka. Katika uzee unaona kila kitu gharama iko juu. Katika uzee ni kama watu wanaongea kwa sauti ya chini. Katika uzee unagundua herufi za maneno katika gazeti ni ndogo hazisomeki vizuri. Katika uzee unaona mabasi yanaanza safari asubuhi na mapema sana. Katika uzee inakuchukua muda kuwatambua wanadarasa na wao kukutambua, wamebadilika na wewe umebadilika. Katika uzee unaona watoto wanaanza shule wakiwa wadogo mno kuliko nyakati zako.

Uzee kadiri ya Kamusi Kuu ya Kiswahili ni hali ya kuwa na umri mkubwa kwa kuishi miaka mingi. Kadiri ya Kamusi ya Karne ya 21 uzee ni hali ya kuzeeka. Kuzeeka ni kuingia katika umri mkubwa na kupungukiwa na nguvu na uwezo. Uzee una maana tofauti kwa watu tofauti.

Jane Ellen Harrison anaona uzee kama kuondoka kwenye jukwaa na kukaa kama mtazamaji na ukiwa umetimiza wajibu wako katika maisha na kutoa mchango wako katika jamii utaridhika kukaa chini na kutazama.

Maggie Kuhn anaona uzee kuwa si ugonjwa bali ushindi dhidi ya misukosuko ya aina yote, ni ushindi dhidi ya majaribu na mambo ya kukatisha tamaa. Kuna aliyesema kuwa uzee ni wakati ambao unajua majibu yote lakini hakuna anayekuuliza swali. Mimi kwangu uzee ni mtazamo. Unaweza kuwa kijana ukawa na fikra za kizee na unaweza kuwa mzee ukawa na fikra kama kijana.

“Mtu hajazeeka mpaka majuto yanapochukua nafasi za ndoto,” alisema John Barrymore.

Ili usije kujuta ukiwa mzee katika umri wa ujana na umri wa kati timiza ndoto zako. Katika ujana tabasamu ili katika uzee mifunyo kwenye uso ikuonyeshe tabasamu zilipokuwa. Licha ya ukweli huo unaweza kutimiza ndoto zako ukiwa mzee. Historia imebeba ukweli huo.

Mheshimiwa Emmerson Dambudzo Mnangagwa amekuwa rais wa Zimbabwe akiwa na umri wa miaka sabini na tano. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa mpatanishi mkuu wa pande zilizokuwa zinaasimiana huko Burundi akiwa na umri wa miaka sabini na nne.

Thomas Edison alishughulika sana katika mahabara yake alipokuwa na umri wa miaka themanini na tatu. Mwanasayansi Galileo alifanya ugunduzi wake mkubwa alipokuwa na miaka sabini na tatu.

Benjamin Disraeli alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa mara ya pili alipokuwa na umri wa miaka sabini. John Milton aliandika kazi yake inayoitwa Paradise Regained alipokuwa na umri wa miaka sitini na tatu.

Noah Webster alitunga Kamusi kubwa kama mlima alipokuwa na umri wa miaka sabini. Grandma Moses alichora michoro yake mingi baada ya kufikisha miaka tisini. Giuseppe Verdi alitunga kazi inayoitwa Othello akiwa na umri wa miaka sabini na tatu na wimbo unaoitwa Te Deum akiwa na umri wa miaka themanini na tano.

Katika uzee unaloweza kufanya lifanye. “Tukiwa na miaka ishirini tuna wasiwasi watu wanatufikiriaje. Tukiwa na miaka arobaini hatujali wanachofikiri. Tukiwa na miaka sitini tunagundua kuwa hawakuwa wakifikiria juu yetu hata kidogo,” alisema Jack Falson.

Zuri litende bila kuogopa macho ya watu na bila kuogopa wanachofikiria juu yako.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom