Maisha ni safari ndefu iliyogawanyika katika makundi makuu matatu; UTOTO, UJANA NA UZEE!
Hata Uwe mtanashati vipi leo lakini kumbuka ipo siku Utazeeka, Hata uweke mekup ya urembo namna gani leo tambua ipo siku utazeeka, Uzee ni baraka ambayo si kila mtu ataipata, Uzee ni tamati njema, Uzee ni tunu yenye utam na uchungu mwingi, Uzee ni mda Wa mavuno uliyopanda ujanani;
Kwahiyo basi kutokana wengi kuwa jeuri, viburi na wenye ujuaji mwingi kiasi cha kuwaona watu wazima ni takataka, Nimeona leo niweke hapa uzi huu maalum juu ya changamoto na matatizo yatokanayo na umri mkubwa yaani uzee ili iwe funzo na msaada kwetu vijana pia tujuzane mambo ya wazee, tuelimishane njia mbalimbali za kuwatunza wazee, tuelezane mahitaji ya wazee, Tuelezane maandalizi ya kuzeeka n.k
Kwa uchache nimeorodhesha baadhi tu ya matatizo ya ambanayo na uzee;
- Dehydration- Binadamu unapofikia uzeeni, mwili wake huhitaji maji mengi zaidi kuriko wakati wa ujana, jambo ambalo hupelekea wazee wengi kupata choo kwa taabu sana (Constipation), jambo ambalo huchangia kuongeza ndita usoni mwao kwa maumivu,pia misuli ya kuchuchumaa huchoka kiasi kwamba hawahitaji mda mrefu kuchuchumaa kujisaidia.
- INI kufail: kutokana na mikiki mikiki ya dunia katika ujana wao, wazee wengi hukumbwa na tatizo la kufail kwa INI, tatizo ambalo hupelekea miguu kuvimba pengine kupata maumivu makali ya mgongo n.k,
- Stroke na kisukari; Uzee unakuja na magonjwa kama hayo kutokana mwili kutofanya kazi ipasavyo.
- Kiwango cha Ute kwenye mifupa hupungua: hii mtu anapofikia uzee uzalishaji wa ute hupungua, tatizo ambalo huchangia mifupa kusagana kirahisi kwenye Maungio kiasi kwamba mwili hushindwa tena kusimama wima kama mwanzo, hilo hupelekea wazee wengi kupinda mgongo na wengine kutafta magongo ili kuupa mwili sapoti.
- Akili huanza kuwa kama mtoto: Kutokana na mwili kuchoka pia na akili huchoka kutokana na kukosa mzunguko mzuri wa damu na oksjen ya kutosha, hii hupelekea akili kubwa kuanza kuwa domants, jambo ambalo hupelekea wazee wengi kuhitaji msaada kutoka kwetu sisi vijana.
- Macho na masikio kuwa hafifu! kutokana na ubongo kupoteza kumbukumbu basi huathiri hadi macho na masikio kupungua nguvu hivyo ni vyema kuongea na wazee kwa mbele huku tukiwa tunawatazama usoni ili kuwaongeza faraja .
- Macho kuwa mekundu: wazee wengi wameuwawa kisa macho kuwa mekundu kwa tuhuma za kichawi lakini ukweli ni kwamba macho mekundu huchangiwa na moshi mkali pamoja na kukosa usingizi, Moshi wa moto hususani wa kuni na kibatari huchangia kwa kiasi kikubwa, Vibatari vingi huko kijijini vinatumia diseli kuriko mafuta ya taa, hii huongeza maumivu kwenye macho.
- Midomo kulegea, zipo changamoto nyingi hutokea mwili unapolegea, maumivu makali yatokanayo mwili kukosa maji na ute huzalisha matumizi ya Ugolo na Tumbaku, jambo ambalo hulegeza midomo na taya.
- Usiri; kutokana na upungufu wa nguvu za kutafta basi hupelekea wazee wengi kuwa watunzaji wazuri wa vitu pamoja na usiri (kuficha), Mzee akikufichia kitu ndani utapata tabu sana kukipata,Wengine huficha vitu na kusahau mahali walipoficha, jambo ambalo hupelekea vitu hivyo kuoza au kupotea
- Kusali; kutokana na kukata tamaa basi njia pekee wazee ni ile ya kujiandaa na kifo kwa kuwa wacha Mungu kwelikweli;
Hivyo basi Ukiwa kama kijana jifunze kuwaheshimu wazee kutokana na changamoto hizo, ni vyema kujiandalia Uzee mwema.
- Wapishe wazee kwenye huduma mhimu ambazo zitawapunguzia maumivu ya kusimama mda mrefu kusubiri huduma,
- Wazee unapowaona wamekosea Tumia usitaarabu kuwaelekeza kwasababu vile wao wanavyopungukiwa akili basi tambua kwamba ndivyo ww unavyoongezeka akili
Mambo ya kuzingatia unapoishi na wazee
- kutokana na Digestive system kupungua kasi kwa umri ni vyema sasa tukawapa wazee wetu vyakula vya matunda na mbonga mboga nyingi katika uzee wao,
- punguza mwanga mkali eneo ambalo mzee ana lala ili apate usingizi,
- ili kuamsha ubongo wao, hakikisha unawapatia michezo ya kuamsha bongo kama bao na draft ili kushtua bongo zao,
- Waache wazee wacheze na wajukuu kwa wingi hii huwapa faraja na kuondoa upweke,
- ni vyema kuishi na wazee mbali na mji/kijijini ili kupata sehemu tulivu.
- Usimkataze mzee wako anapofagia au kulimalima hapo nyumbani ukidhani anadhalilika, tambua hiyo ni sehemu ya tiba kubwa mno kwake muache afue, na afanye usafi apendavyo yeye,
- ikiwezekana mjengee nyumba mzee pembeni ili awe huru kabisa peke ake muulize kama anapenda kupika mnunulie jiko ili apike michicha na mbogamboga hii itamuongezea uwezo na ari ya kuishi vizuri.
Hayo ni baadhi tu ya matatizo Uzeeni, Mengine mtanisaidia karibuni!