Uzee: Maana, kuzuia uzee wa mapema,changamoto na jinsi ya kuwatunza wazee

Uzee: Maana, kuzuia uzee wa mapema,changamoto na jinsi ya kuwatunza wazee

KAMUGISHA: Uzee ni mtihani, kila mtu hutaka kuishi miaka mingi ila hakuna atakaye kuitwa mzee

NA FAUSTIN KAMUGISHA

KUNA methali ya taifa la Iceland isemayo kuwa, kila mmoja anataka kuishi maisha marefu, lakini hakuna anayetaka kuitwa mzee.

Katika maisha utajitahidi kula mlo kamili, kufanya mazoezi, kupumzika, kujitunza vizuri kwa muda wa miaka sitini mwisho wa siku, funga fungua uzee unaingia. “Uzee hasa uzee unaoheshimika, una mamlaka makubwa, na una thamani kubwa kuliko raha zote za ujana,” alisema mwanafalsafa Cicero.

Mtunga-zaburi aliimba hivi kuhusu wazee waaminifu: “Bado wataendelea kustawi wakati wa kuwa na kichwa chenye mvi, wataendelea kuwa wanono na wabichi” (Zaburi 92:14).

Licha ya utukufu wa uzee, uzee ni mtihani. Katika uzee watu wanapoanza kusema kuwa unaonekana kama kijana ni namna nyingine ya kusema umezeeka. Katika uzee unaona kila kitu gharama iko juu. Katika uzee ni kama watu wanaongea kwa sauti ya chini. Katika uzee unagundua herufi za maneno katika gazeti ni ndogo hazisomeki vizuri. Katika uzee unaona mabasi yanaanza safari asubuhi na mapema sana. Katika uzee inakuchukua muda kuwatambua wanadarasa na wao kukutambua, wamebadilika na wewe umebadilika. Katika uzee unaona watoto wanaanza shule wakiwa wadogo mno kuliko nyakati zako.

Uzee kadiri ya Kamusi Kuu ya Kiswahili ni hali ya kuwa na umri mkubwa kwa kuishi miaka mingi. Kadiri ya Kamusi ya Karne ya 21 uzee ni hali ya kuzeeka. Kuzeeka ni kuingia katika umri mkubwa na kupungukiwa na nguvu na uwezo. Uzee una maana tofauti kwa watu tofauti.

Jane Ellen Harrison anaona uzee kama kuondoka kwenye jukwaa na kukaa kama mtazamaji na ukiwa umetimiza wajibu wako katika maisha na kutoa mchango wako katika jamii utaridhika kukaa chini na kutazama.

Maggie Kuhn anaona uzee kuwa si ugonjwa bali ushindi dhidi ya misukosuko ya aina yote, ni ushindi dhidi ya majaribu na mambo ya kukatisha tamaa. Kuna aliyesema kuwa uzee ni wakati ambao unajua majibu yote lakini hakuna anayekuuliza swali. Mimi kwangu uzee ni mtazamo. Unaweza kuwa kijana ukawa na fikra za kizee na unaweza kuwa mzee ukawa na fikra kama kijana.

“Mtu hajazeeka mpaka majuto yanapochukua nafasi za ndoto,” alisema John Barrymore.

Ili usije kujuta ukiwa mzee katika umri wa ujana na umri wa kati timiza ndoto zako. Katika ujana tabasamu ili katika uzee mifunyo kwenye uso ikuonyeshe tabasamu zilipokuwa. Licha ya ukweli huo unaweza kutimiza ndoto zako ukiwa mzee. Historia imebeba ukweli huo.

Mheshimiwa Emmerson Dambudzo Mnangagwa amekuwa rais wa Zimbabwe akiwa na umri wa miaka sabini na tano. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa mpatanishi mkuu wa pande zilizokuwa zinaasimiana huko Burundi akiwa na umri wa miaka sabini na nne.

Thomas Edison alishughulika sana katika mahabara yake alipokuwa na umri wa miaka themanini na tatu. Mwanasayansi Galileo alifanya ugunduzi wake mkubwa alipokuwa na miaka sabini na tatu.

Benjamin Disraeli alikuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa mara ya pili alipokuwa na umri wa miaka sabini. John Milton aliandika kazi yake inayoitwa Paradise Regained alipokuwa na umri wa miaka sitini na tatu.

Noah Webster alitunga Kamusi kubwa kama mlima alipokuwa na umri wa miaka sabini. Grandma Moses alichora michoro yake mingi baada ya kufikisha miaka tisini. Giuseppe Verdi alitunga kazi inayoitwa Othello akiwa na umri wa miaka sabini na tatu na wimbo unaoitwa Te Deum akiwa na umri wa miaka themanini na tano.

Katika uzee unaloweza kufanya lifanye. “Tukiwa na miaka ishirini tuna wasiwasi watu wanatufikiriaje. Tukiwa na miaka arobaini hatujali wanachofikiri. Tukiwa na miaka sitini tunagundua kuwa hawakuwa wakifikiria juu yetu hata kidogo,” alisema Jack Falson.

Zuri litende bila kuogopa macho ya watu na bila kuogopa wanachofikiria juu yako.



Sent using Jamii Forums mobile app
Namkubari sana huyu padre anajua kachambua vizuri mada mbalimbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha ni safari ndefu iliyogawanyika katika makundi makuu matatu; UTOTO, UJANA NA UZEE!

Hata Uwe mtanashati vipi leo lakini kumbuka ipo siku Utazeeka, Hata uweke mekup ya urembo namna gani leo tambua ipo siku utazeeka, Uzee ni baraka ambayo si kila mtu ataipata, Uzee ni tamati njema, Uzee ni tunu yenye utam na uchungu mwingi, Uzee ni mda Wa mavuno uliyopanda ujanani;

Kwahiyo basi kutokana wengi kuwa jeuri, viburi na wenye ujuaji mwingi kiasi cha kuwaona watu wazima ni takataka, Nimeona leo niweke hapa uzi huu maalum juu ya changamoto na matatizo yatokanayo na umri mkubwa yaani uzee ili iwe funzo na msaada kwetu vijana pia tujuzane mambo ya wazee, tuelimishane njia mbalimbali za kuwatunza wazee, tuelezane mahitaji ya wazee, Tuelezane maandalizi ya kuzeeka n.k

Kwa uchache nimeorodhesha baadhi tu ya matatizo ya ambanayo na uzee;
  • Dehydration- Binadamu unapofikia uzeeni, mwili wake huhitaji maji mengi zaidi kuriko wakati wa ujana, jambo ambalo hupelekea wazee wengi kupata choo kwa taabu sana (Constipation), jambo ambalo huchangia kuongeza ndita usoni mwao kwa maumivu,pia misuli ya kuchuchumaa huchoka kiasi kwamba hawahitaji mda mrefu kuchuchumaa kujisaidia.
  • INI kufail: kutokana na mikiki mikiki ya dunia katika ujana wao, wazee wengi hukumbwa na tatizo la kufail kwa INI, tatizo ambalo hupelekea miguu kuvimba pengine kupata maumivu makali ya mgongo n.k,
  • Stroke na kisukari; Uzee unakuja na magonjwa kama hayo kutokana mwili kutofanya kazi ipasavyo.
  • Kiwango cha Ute kwenye mifupa hupungua: hii mtu anapofikia uzee uzalishaji wa ute hupungua, tatizo ambalo huchangia mifupa kusagana kirahisi kwenye Maungio kiasi kwamba mwili hushindwa tena kusimama wima kama mwanzo, hilo hupelekea wazee wengi kupinda mgongo na wengine kutafta magongo ili kuupa mwili sapoti.
  • Akili huanza kuwa kama mtoto: Kutokana na mwili kuchoka pia na akili huchoka kutokana na kukosa mzunguko mzuri wa damu na oksjen ya kutosha, hii hupelekea akili kubwa kuanza kuwa domants, jambo ambalo hupelekea wazee wengi kuhitaji msaada kutoka kwetu sisi vijana.

  • Macho na masikio kuwa hafifu! kutokana na ubongo kupoteza kumbukumbu basi huathiri hadi macho na masikio kupungua nguvu hivyo ni vyema kuongea na wazee kwa mbele huku tukiwa tunawatazama usoni ili kuwaongeza faraja .
  • Macho kuwa mekundu: wazee wengi wameuwawa kisa macho kuwa mekundu kwa tuhuma za kichawi lakini ukweli ni kwamba macho mekundu huchangiwa na moshi mkali pamoja na kukosa usingizi, Moshi wa moto hususani wa kuni na kibatari huchangia kwa kiasi kikubwa, Vibatari vingi huko kijijini vinatumia diseli kuriko mafuta ya taa, hii huongeza maumivu kwenye macho.
  • Midomo kulegea, zipo changamoto nyingi hutokea mwili unapolegea, maumivu makali yatokanayo mwili kukosa maji na ute huzalisha matumizi ya Ugolo na Tumbaku, jambo ambalo hulegeza midomo na taya.
  • Usiri; kutokana na upungufu wa nguvu za kutafta basi hupelekea wazee wengi kuwa watunzaji wazuri wa vitu pamoja na usiri (kuficha), Mzee akikufichia kitu ndani utapata tabu sana kukipata,Wengine huficha vitu na kusahau mahali walipoficha, jambo ambalo hupelekea vitu hivyo kuoza au kupotea
  • Kusali; kutokana na kukata tamaa basi njia pekee wazee ni ile ya kujiandaa na kifo kwa kuwa wacha Mungu kwelikweli;
Hivyo basi Ukiwa kama kijana jifunze kuwaheshimu wazee kutokana na changamoto hizo, ni vyema kujiandalia Uzee mwema.

  • Wapishe wazee kwenye huduma mhimu ambazo zitawapunguzia maumivu ya kusimama mda mrefu kusubiri huduma,
  • Wazee unapowaona wamekosea Tumia usitaarabu kuwaelekeza kwasababu vile wao wanavyopungukiwa akili basi tambua kwamba ndivyo ww unavyoongezeka akili
Mambo ya kuzingatia unapoishi na wazee

  • kutokana na Digestive system kupungua kasi kwa umri ni vyema sasa tukawapa wazee wetu vyakula vya matunda na mbonga mboga nyingi katika uzee wao,
  • punguza mwanga mkali eneo ambalo mzee ana lala ili apate usingizi,
  • ili kuamsha ubongo wao, hakikisha unawapatia michezo ya kuamsha bongo kama bao na draft ili kushtua bongo zao,
  • Waache wazee wacheze na wajukuu kwa wingi hii huwapa faraja na kuondoa upweke,
  • ni vyema kuishi na wazee mbali na mji/kijijini ili kupata sehemu tulivu.
  • Usimkataze mzee wako anapofagia au kulimalima hapo nyumbani ukidhani anadhalilika, tambua hiyo ni sehemu ya tiba kubwa mno kwake muache afue, na afanye usafi apendavyo yeye,
  • ikiwezekana mjengee nyumba mzee pembeni ili awe huru kabisa peke ake muulize kama anapenda kupika mnunulie jiko ili apike michicha na mbogamboga hii itamuongezea uwezo na ari ya kuishi vizuri.
Hayo ni baadhi tu ya matatizo Uzeeni, Mengine mtanisaidia karibuni!
 
Asante kwa mada nzuri pamoja na maandishi yako mazuri.

Nchi yenye wazee wengi duniani ni Japan. Wazee wanaume kule wanafika umri wa miaka 86 kwa wastani na wanawake miaka 90. Lakini wote ni wazima kabisa bila zile magonjwa ya uzeeni. Mmoja ya sababu ni wanakula samaki sana, yaani lishe bora na wako active sana. Lakini pamoja na afya nzuri na hela za kutosha, kitu kinochowasumbua sana ni UPEKWE!!! Hata Ulaya hiyo upekwee ndiyo inahatarisha sana maisha ya wazee! Hata kwetu hii imeanza kujitokeza sehemu za mjini!
 
Asante kwa mada nzuri pamoja na maandishi yako mazuri.

Nchi yenye wazee wengi duniani ni Japan. Wazee wanaume kule wanafika umri wa miaka 86 kwa wastani na wanawake miaka 90. Lakini wote ni wazima kabisa bila zile magonjwa ya uzeeni. Mmoja ya sababu ni wanakula samaki sana, yaani lishe bora na wako active sana. Lakini pamoja na afya nzuri na hela za kutosha, kitu kinochowasumbua sana ni UPEKWE!!! Hata Ulaya hiyo upekwee ndiyo inahatarisha sana maisha ya wazee! Hata kwetu hii imeanza kujitokeza sehemu za mjini!
hao samaki wanaokula ni vibua au sato? maji baridi au ya chumvi? nini chanzo cha upweke?
 
hao samaki wanaokula ni vibua au sato? maji baridi au ya chumvi? nini chanzo cha upweke?

Chanzo cha upweke ni u busy wa maisha kwa vijana! Kule unaweza usionane kabisa na mtoto wako. Na ukifikia Hali ya kutojiweza hupelekwa jumba la kulea wazee hata kama ulikua na watoto wengi maana hawawezi kukulea wao na wao wanakula ujana! Kwakweli uzee ktk developed countries ni mateso!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chanzo cha upweke ni u busy wa maisha kwa vijana! Kule unaweza usionane kabisa na mtoto wako. Na ukifikia Hali ya kutojiweza hupelekwa jumba la kulea wazee hata kama ulikua na watoto wengi maana hawawezi kukulea wao na wao wanakula ujana! Kwakweli uzee ktk developed countries ni mateso!


Sent using Jamii Forums mobile app
aisee
 
hao samaki wanaokula ni vibua au sato? maji baridi au ya chumvi? nini chanzo cha upweke?

Kule Japan chakula yao ni aina ya samaki inayoitwa tuna kwa kiingereza. Lakini kila kitu kinachovuliwa baharini wanaitumia. Halafu hawatumii mafuta sana, inachemshwa kidogo na mara nyingi huliwa hivi hivi mbichi, ili marutubisho yasipotee. Kuhusu upekwe mkuu Lusungo amenisaidia hapa juu
 
pia unaweza dhulumiwa na watoto Wa siku hizi macho kodo
tena hata kukuua. ila hapa ni kuwa make sure una pesa za kukutunza. ukitegemea watoto!! wana yao. na ikiwezekana kama kuna chao wape mapema. ila bakiza chako unachojua kitakusuma utakapokatikia basi!!
 
Back
Top Bottom