Uzi gani una-trend hapa Jamii Forums lakini haukuvutii?

Mwanadiplomasia Mahiri

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2019
Posts
491
Reaction score
1,907
Mimi ni huu uzi wa wazee wenzangu njooni tuweke mikeka

Sielewi wanachojadili maana kila nikifungua nakuta ni maumivu tu watu wanasema kesho lazma tumle muhindi. Sijaelewa kwanini uzi unatrend sana lakini mazungumzo mengi kule ni ya majonzi.

Uzi mwingine una-trend ila sijawahi kuulewa ni ule wa "Tupia picha ya mdada wowote mzuri" ule uzi ukiuendekeza utakuwa Diego Maradona kila siku.

Wewe ni uzi upi huuelewi lakini muda wote una-trend na comments za kutosha?
 
"Hatima ya maisha yangu iko mikononi mwa kijana wa Buguruni" 🤔 Huu uzi una trend kweli! Ila sijawahi kuulewa unahusu kitu gani hasa.

Kuna siku nilijaribu kuufungua, nikakuta watu wanatukanana! Nikabakia tu mdomo wazi.
 
Ushoga na ushoga vinaongezeka Kwa Kasi yaani sijawahi hata usogelea

Pia Kuna kwanini utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…