Uzi gani una-trend hapa Jamii Forums lakini haukuvutii?

Uzi gani una-trend hapa Jamii Forums lakini haukuvutii?

Mimi Uzi wa mgogoro wa Russia na Ukraine nauchukia Sana,Kuna siku nilijaribu kufungua nakuta Ni liuzi lirefu na vitu havieleweki nikasema siwezi shoboka na mambo ya nchi za watu.

Tangu siku hiyo huo Uzi huwa naupita kwa Kasi ya 5G
Huo Uzi hauwezi pita siku sijapitia kujua habar za wababe wa dunia[emoji4]
 
1. Kwanni utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini

2. Uzi wa kupeana likes

3. Uzi wa vyakula: Mwanzisha uzi alipost mkate una panya ndani yake. Hiyo picha ilinifanya niuchukie uzi mzima.

Mie kuna ule wa Vituko Mtandaoni, Tupia Cha Kwako[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
1.kula tunda kimasihara.

2. Jamiiforums usiku wa manane.

3. kupeana likes sijui na comments.

4. Kwanini utumishi……..

5.Uzi wa kubet

Hizo nyuzi sijawahi kufungua hata siku moja.

Hata hivyo uzi wangu pendwa wa Chakula kuna watu hawajawahi kuufungua, kweli mtu chake.
 
"Hatima ya maisha yangu iko mikononi mwa kijana wa Buguruni" [emoji848] Huu uzi una trend kweli! Ila sijawahi kuulewa unahusu kitu gani hasa.

Kuna siku nilijaribu kuufungua, nikakuta watu wanatukanana! Nikabakia tu mdomo wazi.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Hata mimi sijawahi elewa wanachat nin mulee
 
"Hatima ya maisha yangu iko mikononi mwa kijana wa Buguruni" 🤔 Huu uzi una trend kweli! Ila sijawahi kuulewa unahusu kitu gani hasa.

Kuna siku nilijaribu kuufungua, nikakuta watu wanatukanana! Nikabakia tu mdomo wazi.
Huu mbona mzuri sana tu boss sema mwanzoni unaweza usiuelewe
 
Mimi ni huu uzi wa wazee wenzangu njooni tuweke mikeka

Sielewi wanachojadili maana kila nikifungua nakuta ni maumivu tu watu wanasema kesho lazma tumle muhindi. Sijaelewa kwanini uzi unatrend sana lakini mazungumzo mengi kule ni ya majonzi.

Uzi mwingine una-trend ila sijawahi kuulewa ni ule wa "Tupia picha ya mdada wowote mzuri" ule uzi ukiuendekeza utakuwa Diego Maradona kila siku.

Wewe ni uzi upi huuelewi lakini muda wote una-trend na comments za kutosha?
Yaani ule uzi wa kijinga sana wakusema eti …. after hopeless years sijui kitu gani, yaani ningekuwa na uwezo ningempiga BAN mleta maada ya maisha
 
"Je umeshawahi Kula tunda kimasihara? Sijawahi kuuelewa kwakweli ajabu eti ni wa tangu 2014
 
Uzi wa Selfika na Post picha
Uzi wa vyakulaa
Uzi wa Kijana wa buguruni alivyobeba hatma ya maisha yangu
Uzi wa Dar vs Nairobi
Uzi maalumu wa kupeana like na comment
Kati ya hizo ulizotaja tatu ni zangu
 
1. Kwanni utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini

2. Uzi wa kupeana likes

3. Uzi wa vyakula: Mwanzisha uzi alipost mkate una panya ndani yake. Hiyo picha ilinifanya niuchukie uzi mzima.
Namba 3.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom