Uzi gani una-trend hapa Jamii Forums lakini haukuvutii?

Uzi gani una-trend hapa Jamii Forums lakini haukuvutii?

Huyu hayuko serious. Hivi kuna Uzi unafurahisha Kama ule? Mimi nikiona nimekuwa bored tu naufungua huo. Kuna watu walikuwa na mamilioni mule wamefilisika Hadi wamerudi kwa wazazi 😀😀😀
Anakusalimia mjeda wako na amesema siyo vizuri kutwa kwenye mitandao.
 
Mimi Uzi wa mgogoro wa Russia na Ukraine nauchukia Sana,Kuna siku nilijaribu kufungua nakuta Ni liuzi lirefu na vitu havieleweki nikasema siwezi shoboka na mambo ya nchi za watu.

Tangu siku hiyo huo Uzi huwa naupita kwa Kasi ya 5G
Kimsingi ni Uzi ambao hata mimi siukubali kabisa kuna mwamba huwa yeye anacomment tu Slava Ukraine.
 
Mimi ni huu uzi wa wazee wenzangu njooni tuweke mikeka

Sielewi wanachojadili maana kila nikifungua nakuta ni maumivu tu watu wanasema kesho lazma tumle muhindi. Sijaelewa kwanini uzi unatrend sana lakini mazungumzo mengi kule ni ya majonzi.

Uzi mwingine una-trend ila sijawahi kuulewa ni ule wa "Tupia picha ya mdada wowote mzuri" ule uzi ukiuendekeza utakuwa Diego Maradona kila siku.

Wewe ni uzi upi huuelewi lakini muda wote una-trend na comments za kutosha?
“Umevaa nini leo? Tupia uturingishie”
 
Huo uzi siupendi sana sana maana hata sijawahi kuuelewa na sijui watu gani humu huwa wanacomment humo na kuuweka on trending wakati wengi humu tumeonesha kutoupenda
Huo uzi ukiwa una kazi uwezi kuuelewa kabisa lakini kwa wanao tafuta kazi serikalini wanaelewa sana maana yake!
 
1. New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

Huo uzi sijawahi kuuelewa kabisa kwanzia mwaka juzi umeanzaa, kwanza wananiuzi na kiingereza chao. Sijawahi kujua wanaongea nini , wanaongea kiingereza kigumu sana

2. Makapuku Forum (Hawa sijui wamepotelea wapi siku hizi)

3. Uzi wa kupeana Likes, Comment chochote upate likes

4. Kula Tunda Kimasihara (Naona ni kama mambo ya kitoto maana kwangu mm kila siku nikila tunda huwa ni mimasihara , so sijawahi kuona jipya)

5. Wazee wenzangu wa kuweka mzigo , Njooni tubashiri mechi za leo ( Hawa jamaa kila siku wanapigwa na mhindi ila hawakati tamaa)
 
Mpaka muda huu uzi wa watumishi unaongoza ukifuatiwa na wazee wa kuweka mzigo[emoji23][emoji23].
Tuendelee wazee
 
1.kula tunda kimasihara.

2. Jamiiforums usiku wa manane.

3. kupeana likes sijui na comments.

4. Kwanini utumishi……..

5.Uzi wa kubet

Hizo nyuzi sijawahi kufungua hata siku moja.

Hata hivyo uzi wangu pendwa wa Chakula kuna watu hawajawahi kuufungua, kweli mtu chake.
Sizipedi zote ulizozitaja,na Huwa nazipita
 
Nilirudisha kaka.
Jaza upya hi form, Kisha copy peleka kwa mwenyekiti dronedrake na katibu wake mshamba_hachekwi
Screenshot_20231230-170320.png
 
Back
Top Bottom