Uzi kwa ajili ya kupeana michongo

Nenda Gardaworld utapata kazi ukikidhi vigezo
 
Habari zenu ndugu na jamaa.

Naimani nyote ni wazima.

Kama hadaa yangu niendelee kutoa shukran za dhati sana kwa wanaoendelea kushare michongo mbalimbali.

Naomba Muendelee na moyo huo huo kwa kuwa tunajivunia kuwa sehemu ya watu tunaothubutu kuisaidia jamii yetu kujikwamua katika hali ngumu zinazowakabili.

Hivyo bhasi tuendelee kuwa faraja kwa wale waliokata tamaa hasa katika maswala ya utaftaji wa ajira, tukawe msaada kwao.

Ahsanteni sana na Mungu awabariki.

Tupeane michongo
Tupeane michongo
Tupeane michongo
Tupeane michongo.
 
Kule niliwahi kwenda sema wao huwa wakihitaji watu wenye urefu wa 5.7 , ila hakuna namna ilinibidi niachane nao .
Kama una laki 2 sema tufanye mchongo.

hizi kazi kama huna vigezo lazima uwe na hela.

watu wafupi kama nyie huwa tunawapeleka kigoma hukoo hakuna kwenda Head quarters Dar mtarudishwa na makofi juu😅😅😅
 
Kama una laki 2 sema tufanye mchongo.

hizi kazi kama huna vigezo lazima uwe na hela.

watu wafupi kama nyie huwa tunawapeleka kigoma hukoo hakuna kwenda Head quarters Dar mtarudishwa na makofi juu[emoji28][emoji28][emoji28]
Mkuu inbox tuwasiliane wala hakuna shida , au naomba namba yako
 
Wakuu ni nimesomea ukatibu wa afya...utawala afya mwenye connection karibu nipo kibaha.
 

Uandikaji wa barua za kuomba kazi pamoja na CV ni moja ya changamoto kubwa sana kwa wanaoomba kazi! Kwa zaidi ya miaka 15 nimekuwa panelist kwenye kupitia barua za wanaoomba kazi, ku short list, na hatimaye kuwafanyia interview/usaili. Kama humu kuna mtu ambaye anahisi vipengele hivi viwili bado vinampa changamoto asisite kuomba msaada ili nimsaidie, pia naweza kujibu maswali yoyote ambayo mtu anayo juu ya vipengele tajwa hapo juu! Kuna candidates wengi ambao barua zao na CV huwa hatupotezi hata dakika 2 kuzipitia! Ni lazima uongeze uwezekano wa kupata kazi kwa kuhakikisha barua yako na CV vipo Sawa sawa! Imagine nafasi ya kazi labda ni moja na mlioomba ni 100! Unafikiri kila barua na CV vinasomwa na kupitiwa?!...Hapana! Hata ungekuwa wewe usingeweza. Lazima zitumike namna za kuzipunguza hizo barua na CVs ili kuwapata wachache ambao watapita kwenye “vigezo” vya ujumla na hatimaye ndipo tuweze sasa kuzisoma na kuona kama wanafaa au la!
 
Shukran sana kiongozi umetukumbusha kitu muhimu sana ndugu yangu.

Mungu akujaliie kwa hili dogo.

Halikadhalika kama hutojali ungejaribu kutoa japo sample ya CV's na barua zinazostahili kwa manufaa ya wasomaji wa uzi huu..

Shukran sana[emoji120]

Tuendelee kupeana michongo na ushauri wenye manufaa.


Tupeane michongo
Tupeane michongo
 

Mkuu legend binafs hii namini inaweza kuwa tatizo kwangu

Nisaidie kunielekeza vitu muhimu ninavyotakiwa niweke ktk CV na barua ya kuomba kazi na ikiwezekana na vitu nisivyotakiwa kuweka nielekeze Pia

Ukiniwekea na sample ya CV na barua zilizo sahihi nitashukuru zaidi

Ahsante
 
Wakuu habari za weekend,
Kuna binti anahitaji kazi iwe dukani,mgahawa,usafi kwa yeyote mwenye details za mchongo kwenye field hizo atupie hapa.
Asanteni
 
Wakuu habari za weekend,
Kuna binti anahitaji kazi iwe dukani,mgahawa,usafi kwa yeyote mwenye details za mchongo kwenye field hizo atupie hapa.
Asanteni
Anahitaji kazi halali yoyote ni msichana.
Ikiwa ya duka,
Mgahawa,
Usafi. N.K


TUPEANE MICHONGO
TUPEANE MICHONGO
TUPEANE MICHONGO
TUPEANE MICHONGO
 
mchongo kwa sasa ni kilimo tu,ukilima ekar 2 za alizet lazma utatoka na m4+,mafuta tz imekuwa tatzo wajanja tunachangamkia fursa hii
 
Daah , Nashukuru Sana mkuu Mungu azidi kukubariki endelea kunisupport nipate japo nipate ata sehemu ya kujitolea maana mtaani kungumu sana
mimi nadhani bora kwa sasa ungeenda kujiandikisha pale TAESA opposite na D.I.T ili wakutafutie intern ujishikize kwa kuanzia ukiwa huko ni rahisi kupata mchongo kuliko kukaa nyumbani maana wao wenyewe huwa wanatoa posho na huko utakapo pangiwa kufanya huwa pia wanakupa posho
 
Afu na hapo garama za uwekezaji mpaka kuvuna Ni kiasi gani?
gharama zake so kubwa sana,mbegu peke ake ni 30,000 kwa hzo ekar mbil,haihtaj mbolea kama shamba linalutuba ata ya wastan na halihtaj mvua ya kutoxha ili listawi ,hasa pale linapochanua huhtaj ukame ili kupata alzet zenye mafuta meng
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…