Uzi maalum kwa wale wanaomuamini Mungu muumba

Uzi maalum kwa wale wanaomuamini Mungu muumba

Good day, Good people!

Hivi Karibuni kumezuka mfululizo wa nyuzi kibao hapa JF na zote zikipinga uwepo, uweza, na utendaji kazi wa Mungu. Kiukweli zimenifanya nikazama ndani kufikiri kwa kina zaidi juu ya uwezo wa Mungu na nimepata haya ya kuzungumza na kushare na nyinyi kidogo, ila ningependa kuona na nyie mkiandika sababu zinazowafanya kuamini Mungu yupo na ndie aliezitanda mbingu na nchi.

Iko hivi, Miaka michache iliyopita kumekuwa na wimbi la wanasayansi nguli waliokuwa "notorious atheist"(kindakindaki wasioamini mungu kabisa) kwa miaka kibao kuanza tena kuamini, kukubali na kukiri uwepo wa Mungu hadharani ila tukio maarufu zaidi lilikuwa la mwanasayansi mashuhuri alieshawishi watu wengi zaidi wamkane Mungu kuamua kumgeukia Mungu na kuandika kitabu nilichoambatanisha hapo chini jamaa anaitwa Mr Antony flew kuamua kukiri kwamba namnukuu "God exist and he is the master of the people and universe" But sababu kubwa kwao ilikuwa ni wao kutoka nje ya Dunia na kujionea maajabu mengi lukuki ambayo yaliwalazimu kuamini namna universe and Earth zinavyofunction kwa namna ya kustaajabisha yenye kufuata utaratibu naalumu wa laws and regulation za ajabu basi wakakiri kuna mystic higher spirit ambae ni best designer ever wao wanamwita "supreme being" mwenye uwezo wa ajabu sana, maana walichokiona ni kila kitu kinafanya kazi kwa mfumo wa laws of nature ambazo zina viashiria vya kuwekwa na mtu/roho kubwa maana haviwezekani kujipangilia vyenyewe katika usahihi wa kimfumo kama vile na kufuata utaratibu kwa usahihi kwa mabilion ya miaka bila kuparaganyika au kujikanganya. Cha kwanza;

Earth distance
Hawa wanasayansi waligundua kuna umbali sahihi kabisa Kati ya jua na Dunia.. Na ingetokea Dunia ingesogea kidogo kuelekea jua lilipo basi Dunia ingeungua sana na pia ingetokea Dunia ingesogea mbele kidogo tu kuliacha jua basi Dunia ingekuwa na barafu jingi sana Kwa kukosa joto na isingeruhusu maisha yawepo lakini kaiweka umbali sahihi na lilipo jua ili ipozwe na kuchemshwa na jua la wastani. Haiwezi kutokea out of nowhere there must be designer wa kufanya hizi complex and sophisticated calculation. Na pia unajua dunia ikisimama kwa sekunde moja inakuwaje? Wote tutavurumushwa hadi kwenye sayari ya Jupiter tukafie huko maana inatembea kwa kasi...but kwa miaka dahari Dunia haijawahi kusimama maana ikisimama Kwa kasi inayoenda basi miili yetu itaokotwa Jupiter. Sijui unanielewa hapa!? Ni kwa huruma tu ya Mungu anaiacha inazunguka dearly kwa Upendo wake for billions of years. Ninashukuru Mungu kwa hili.

Earth size
Sikia hii unajua kwamba hii size ya dunia ndio sahihi na salama kwa maisha yetu sababu inafanya dunia iwe na mchanganyiko sahihi wa gas za oxygen na nitrogen kiasi kinachosuport maisha Duniani hili viumbe tuishi. Dunia ingekuwa ndogo tu basi kungekuwa na kiasi kikubwa sana cha hydrogen hivyo kusababisha maisha yasiwezekane hapa Duniani. Kama ambavyo ukienda mile 50 juu ya uso a dunia huipati hii perfect gas mixture ya Duniani. Hayajajileta haya yote kafanya Mungu wetu kwa uweza wake mkuu sana.

Brain,
Ubongo unavyofanya kazi unathibitsha jinsi Mungu alivyo na uweza wa ajabu...unajua ubongo unachakata taarifa zaidi ya million kwa sekunde kwa wakati mmoja yaani simultaneously. Haya ni maajabu yaliyopitiliza akili na uwezo wa kibinadamu kufahamu nini kisababishi cha haya yote. Maana ubongo unaweza kuwa unafiri kingine, then hapo hapo ubongo unapima mapigo ya moyo, unapima temperature ya pale chini ulipokanyaga, unatafsiri harufu mbalimbali, e.t.c

DNA code informs,
Hii ndio imewafanya kila mtaalamu Duniani anaesoma biology kushangaa akili kubwa isiyomithilika iliyotumika kwenye Ku code zile DNA kwenye cell maana kila cell ina billion of DNA zilizokuwa coded kwa usahihi na uwezo wa hali ya juu zikitunza taarifa za kila mmoja kwa usahihi Zinazothibitsha kuna kazi ya akili sana imefanyika...nani nafanya hapo sasa ndio wanasayansi wanarudi mezani na kukiri uwepo wa "mystical supreme spiritual being" God, Wanakwambia hata tupewe miaka billion hatuwezi kufanya coding ya DNA hata kwa mtu mmoja kamwe na hakuna kiumbe binadamu aliezaliwa na mwanamke anaeweza kufanya hii kazi. Nani kafanya sasa hii kazi..wenyewe huwa wanajijibu kwamba "there is supreme being spirit" who coded this DNA. Maana hata kwenye computer lazma kuwe na mtu wa kufanya code ili computer ifanye kazi unless hautakuwa computer...!

Na maelezo ya DNA yanathibitisha Mungu anatujua sote zaidi tujijuavyo sisi wenyewe maana kila mtu kamuumba kwa utofauti wa kipekee sana. Tumuheshimu Mungu.. Kuna jamaa humu alimwita eti "Mungu zuzu" C'mooooon guys hiki kiburi cha maisha ya Duniani kisitupe jeuri ya kumdhiaki na kumtukana Mungu...tumuheshimu Mungu!! kama baba yako tu asie na uungu wowote anataka heshima basi hopefully Mungu atakuwa zaidi yake...let give him thanks and praises he won't deceive us.

Hayo ni baadhi tu, kuna mengi yanayo tuthibitishia Mungu anaishi...ana uweza..na yupo.

View attachment 795233View attachment 795234View attachment 795235View attachment 795236
Asante mkuu. Nimekuelewa vizuri.
 
hapo inategemea.
wasumeria(Sumer) au wababylon au wakazi wa kusini mwa mesopotamia wanasadikiwa kuanza kuandika karne mbili kabla ya wamisri.
lkn pia kucopy na kupaste sio lazima maandishi. ndio maana nimekwambia hata uchawi na dini za kiafrika sio orgin bali ni c/p. they wewe there in ancient mesopotamia mamiaka kibao tu.

hapo ndipo uchawi,maandishi mengi ya kupinga Mungu huku wakikumbatia miungu yalichupukia. Yakaingilia Misri, yakiibukia ugiriki na rumi kisha kusambazwa kwa lugha tamu na usomi katka dunia ya sasa. mengi yanayofanyika leo Kupinga Mungu ni marudio mkuu.
first civilised society ni kemet(ancient egypt)
hao wengine sijui umewaokotea wapi
 
Alipokuja aliacha kila kitu akaja kama mwanadamu wa kawaida akaishi kama mwanadamu tofauti ni jinsi gani mimba yake ilipatikana....aliishi kama mwanadamu wa kawaida ili basi tuamini ya kwamba anatoka katika kiti cha enzi na kupitia maisha tupate ukombozi na pia kutufundisha habari za ufalme wa mbinguni. Kifo cha Yesu na ufufuko wake ndio uliokamilisha kazi ya kukomboa wanadamu. Baada ya kufa sikuya tatu alifufuka akarudi kwenye kiti chake.
unaamini yule mzungu ndiye mungu unayemuamini wewe?
 
first civilised society ni kemet(ancient egypt)
hao wengine sijui umewaokotea wapi
Hapo tutaingia kwenye mjadala ambao haujapata hitimisho kati ya Sumer(along side ancient rivers Tigris and euphrates) na egypt (civilization along river nile) nani wa kwanza kujanjaruka.
Ila kwa ushahidi wa kisasa ambao Unaumana na Biblical history Sumer au babeli imekuwepo katika civilization kuliko hata hiyo misri unayoiamini mkuu.
hermes ndio orginator hata wa ibada nyingi za huko misri na kuna miungu mingi tu yenye majina sanjari na miungu ya babeli.
We are coming from ancient babylon and the word is returning to babylon with the speed of photon.
nothing new.

God exist. haya unayoyaona yalianzia Sumer, babylon siku kadhaa baada ya 17/7 wa kiyahudi baada ya safina kutua juu ya mlima hararati na watu wakaanza kuzaliana na kuasi upya kisha kusambaa dunia nzima.
 
Mungu yupo Jana nmetumiwa meseji toka mwaka 2020 .. Sababu ya act nlyotaka kuifanya .. Tena mesej imetumwa siku ya birth day yangu aisee nyie hii dunia INA maajabu sana aisee
 
Hapo tutaingia kwenye mjadala ambao haujapata hitimisho kati ya Sumer(along side ancient rivers Tigris and euphrates) na egypt (civilization along river nile) nani wa kwanza kujanjaruka.
Ila kwa ushahidi wa kisasa ambao Unaumana na Biblical history Sumer au babeli imekuwepo katika civilization kuliko hata hiyo misri unayoiamini mkuu.
hermes ndio orginator hata wa ibada nyingi za huko misri na kuna miungu mingi tu yenye majina sanjari na miungu ya babeli.
We are coming from ancient babylon and the word is returning to babylon with the speed of photon.
nothing new.

God exist. haya unayoyaona yalianzia Sumer, babylon siku kadhaa baada ya 17/7 wa kiyahudi baada ya safina kutua juu ya mlima hararati na watu wakaanza kuzaliana na kuasi upya kisha kusambaa dunia nzima.
hakuna kitu kama hicho
alexander the invader kutoka mesopotania alifundishwa ustaarabu egypt alipofanya uvamizi wake wa kihuni
usilete habari za kutunga za safina nilishakwambia
hakukuwahi kuwepo gharika ya nuhu
kasome kitabu cha Dr.Ben Yosef Jochannan (Africa,the source of western civilization) na uachane hao watoto wanaotupia ujinga huko wikipedia
 
hakuna kitu kama hicho
alexander the invader kutoka mesopotania alifundishwa ustaarabu egypt alipofanya uvamizi wake wa kihuni
usilete habari za kutunga za safina nilishakwambia
hakukuwahi kuwepo gharika ya nuhu
kasome kitabu cha Dr.Ben Yosef Jochannan (Africa,the source of western civilization) na uachane hao watoto wanaotupia ujinga huko wikipedia
hahaha mkuu nikusahihishe kwanza naona kuna magap kwenye sentensi au hao jamaa wanakupotosha au umebobea kwenye story za upande mmoja.

Alexander hakuwahi kuwa mmesopotamia. Alikuwa Mgiriki kijana mwanafunzi wa SOCRATE.

ndio maana nimekukumbusha tu.

Safari ilianzia Babylon, Ikaenda Misri, wagiriki wakajifunza huko akiwemo na Aristotle wengi wamekuwa wanafunzi wa philosophia huko misri. Warumi kwa kuwahusudu wagiriki wakaiga kwao kila kitu hadi miungu ila wakaipa majina yao.

Mungu yupo. hizo story za hao wazee na waandishi achana nazo.
 
Mtoa mada hongera sana kwa uchambuzi wako mzuri sana.....huu uchambuzi kibinadamu umeweza kukupa uelekeo wa uwepo wa Mungu je ukiingia kiroho itakuwaje?
"Nyani Ngabu,
Nimesoma comment yako naomba nikusaidie ufahamu kidogo kuhusu huyu Mungu anaetajwa na tunaemwamini kwa ajili ya utukufu wake,
Nilichoona kwako unamtaka Mungu katika flesh yani kama unavyomuona Nyani Ngabu ndivyo unataka umuone Mungu hakika kwa aina hiyo hutamuona Mungu kwa sababu Mungu ni roho, tokeao msingi wa kuumbwa kwa ulimwengu huu roho ya Mungu na neno ndiyo iliyoyafanya haya tuyaonayo na kuyabeza.....soma Mwanzo 1:2 nanukuu "Nayo nchi ilikuwa ukiwa tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji, Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.3 Mungu akasema iwe nuru ikawa nuru" ukiendelea utaona vile uumbaji ulivyoendelea hapa nilitaka kukuonyesha tu kwamba Mungu ni roho.

Ili umwelewe Mungu na matendo yake unahitaji kumtafuta kwa roho...Soma Yohana 4:24 Mungu ni roho nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli, kweli ambayo ni neno lake.

Mapungufu uliyosema ya Mungu sijayaona ila mapungufu ni yakwetu sisi wanadamu kwa kuliacha pendo lake na kuasi. Utaniuliza kwa nini sasa Mungu aumbe mwanadamu ambaye atamuasi. Kwanza ufahamu kwamba Mungu hakuanza kuwepo baada ya kuumbwa kwa dunia la hasha... Mungu alikuwepo kabla hata dunia haijaumbwa, ukisoma Mwanzo Hiyo hiyo Mwanzo 1:26 Inasema Natumfanye mtu kwa Mfano wetu......naomba uchukue neno wetu alafu ujiulize kwanini wetu na si wangu? Neno la pili ni Mfano linamaana gani kwa nini si kama mimi? Hii inadhihirisha sisi ni kama kopi ya Mungu na neno wetu inadhihirisha kwamba mbinguni walikuwepo zaidi ya maelfu ya malaika wake ambao ndio alisaidiana nao katika uumbaji. Kama ningetumia tafsiri nyingine ningesema Mungu ndo alikuwa Engineer mkuu na maelfu au mabilioni ya malaika wake walikuwa kama wasaidizi. Inaonyesha ni kiasi gani Mungu ana uwezo na nguvu kusimamia mradi mkubwa namna hii design na kumpliment project kubwa hivi si kazi ndogo ilikuwa ni day and night mpk siku ya saba ndipo alipopumzika ebu kuweni na adabu kidogo mumheshimu na mumpe sifa zake Mungu mimi nitakupa sifa zote kwa ukuu wako mana hata Nyani Ngabu ni kazi yako iliyonjema sana. Uumbaji wa Mungu si sawa na hivi Viproject vyetu ambavyo hata wakati mwingine tunashindwa kudeliver matokeo mazuri. Hii mada ni pana sana natamani kushare nanyie kwa kadri Mungu atakavyonijalia sema sijui kufungua uzi niwe mkweli najua nijamaliza kujibu maswali yako naomba niendelee kukujibu kidogo kidogo ili nisiharibu uzi wa mwenzangu barikiwa sana.

Mungu ni imani tu. Na imani ni kitu cha kufikirika tu.

Mtaishia kusema mungu yupo mungu yupo lakini kujibu maswali mepesi juu ya huyo mungu hamuwezi.

Saying it so doesn’t make it so.
 
hahaha mkuu nikusahihishe kwanza naona kuna magap kwenye sentensi au hao jamaa wanakupotosha au umebobea kwenye story za upande mmoja.

Alexander hakuwahi kuwa mmesopamia. Alikuwa Mgiriki kijana mwanafunzi wa SOCRATE.

ndio maana nimekukumbusha tu.

Safari ilianzia Babylon, Ikaenda Misri, wagiriki wakajifunza huko akiwemo na Aristotle wengi wamekuwa wanafunzi wa philosophia huko misri. Warumi kwa kuwahusudu wagiriki wakaiga kwao kila kitu hadi miungu ila wakaipa majina yao.

Mungu yupo. hizo story za hao wazee na waandishi achana nazo.
inawezekana nimechanganya mesopotania na macedonia...alexander ana asili ya moja ya hayo majina mawili..neno greec lilikuja badae
alexander na wavamizi wenzake by the time wanafika kemet walikuta watu wana ustaarabu wa miaka elfu kadhaa
hata homer(wagiriki wanamtukuza ndiye mwandishi wa kwanza) alienda kujifunza uandishi misri
akina socrates,aristotle,plato wote walienda misri kujifunza
taifa la ugiriki lilizaliwa miaka si zaidi ya 1000 before common era
warumi kujifunza kutoka kwa ugiriki ni baada ya kuwafukuza wagiriki misri na kukuta lugha yao imetamalaki kule
 
Nizuie basi. Au kama vipi muombe mungu wako anizuie.
Huu ni ukorofi wa wazi kabisa umeambiwa huu ni Uzi special kwa wale wanaomuamini Mungu. Sasa wewe usiemuamini sijui unatafuta nini humu!?

Afu unasema tumwambie Mungu wetu akuue..kama Kova mwenyewe hafanyi kazi kwa unlawful orders kama zako basi Mungu wetu ni zaidi... Hawezi kufanya Kazi kwa unlawful order zako hizi chief.
 
Mm kuna baadhi ya comment nikizisoma zinaniletea ukakasi mdomoni, JAMANI ACHENI KUKUFURU, BINAADAMU ATUNA UJANJA, ATUJUI MUDA GANI MTU ATAREJEA KWA MUUMBA, VIBURI IVYO ATA KINA FIRAUNI WALIKUA NAVYO NA KILICHOWATOKEA TUNAKIELEWA, NA ULE NI MFANO KUWA MUNGU YUPO, OMBENI MSAMAHA NA MURUDI KWA MOLA WENU HARAKA HAMJACHELEWA
 
Back
Top Bottom