Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Sasa wewe unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo?

Utafiti upi unathibitisha pasi shaka kwamba Mungu yupo?

Mungu ni nini?
siwezi, na hakuna utafiti unaoweza kuthibitisha mpaka sasa,

ndo maana nilikwambia akili ya binadamu ina limit,
nawe maswali yako yanaishia ndani ya hiyo limit,

unataka wathibitishe kwa kutumia njia za utafiti ?
hizihizi ambazo bado kuna mambo common kabisa na hayana majibu ya kisayansi ?
ndo unataka zitumike kuthibitisha uwepo wa Mungu ?

hizihizi njia ambazo zinaonekana saivi advanced za kufanya utafiti na ugundizi mbali mbali, baada ya muda zitaonekana inefficient kaabisa na zimepitwa na muda, watakapokua na namna nyingine bora zaidi

conclusion: bado kuna mambo mengi hayahesabiki, ambayo hatujayajua, mengine labda tutajua siku za karibuni, mengine labda itachukua maelfu ya miaka

kwahiyo huwezi kutumia common sense na njia za kisayansi kuthibitisha kwamba Mungu hayupo,

hizi njia na tafiti za kisayansi unazoziona advanced sana leo hii ni bado kabisa yaani, zinaonekana advaced kwakua ndo uwezo wa juu zaidi tuliofikia kiakili, ila bado sana sasa.. hata baada ya ma elfu ya miaka bado kuna vitu vitaendelea kujulikana na haviishi ili uone ni jinsi gani akili ya binadamu inaishia, "ni kama unatumia kijiko kuhamisha maji kutoka baharini"

wewe ukichota kijiko kimoja ukakioeleka sehemu nyingine unaona kuna maji umeyahamisha lakini je bahari utaimaliza lini ?

soma bandiko vizuri maana unarudia maswali hayohayo
 
Imeandikwa aliumba kwa siku Saba tuu, leo ulimwengu unapanuka na sayari na majua yana undwa kila uchwao
Acha ujinga
 
Uko sahihi. Hata mimi wakati fulani nimehoji kupitia uzi. Kwa binadamu nini kinafuata baada ya ufahamu? Tumeishia kwenye consciousness. Hiyo next level ndio uungu
 
Uko sahihi. Hata mimi wakati fulani nimehoji kupitia uzi. Kwa binadamu nini kinafuata baada ya ufahamu? Tumeishia kwenye consciousness. Hiyo next level ndio uungu
ni kweli kabisa uungu huenda pia upo level za juu zaidi...
 
hoja zao ni zilezile zinajirudia kilasiku hadi unazikariri
atakwambia kama Mungu yupo, wote tungekua tunajua tusinge bishana
Anakwambia kama yupo basi na yeye kaumbwa.....
An mzee ukibishana nae anakuleta kwenye ka cycle flani hvi apo utoboi yeye anakua pembeni anakucheka tu na maswali yake ya thibitisha ahahaha
 
Anakwambia kama yupo basi na yeye kaumbwa.....
An mzee ukibishana nae anakuleta kwenye ka cycle flani hvi apo utoboi yeye anakua pembeni anakucheka tu na maswali yake ya thibitisha ahahaha
Cycle ndo hiyohiyo maana limit ya ufikiri inaishia humohumo kwaiyo, kwaiyo mtu akitoa hiyo mada anajiona amefikiri hadi mwisho,

ila kuna vingine vingi havielezeki, na havi make sense kwasababu uwezo wa akili haufikii huko,

ndo maana hata zamani kunavitu vilikia havi make sense mfano tu simu ila baada ya kugunguliwa vinaonekana kawaida

viko vingi ni infinity haviishi hata miaka elf10 ijayo bado watakua wanagundua vitu vipya kabla ya hata kufikia kumuelewa Mungu na kuthibitisha yupo kama wanavyodai
 
siwezi, na hakuna utafiti unaoweza kuthibitisha mpaka sasa,
Sasa kama huwezi kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu, Utasemaje yupo?

Huoni kwamba unafosi mawazo yako uchwara yasiyo na uthibitisho wowote ule?
ndo maana nilikwambia akili ya binadamu ina limit,
nawe maswali yako yanaishia ndani ya hiyo limit,
Kama wewe ubongo wako una limit uliwezaje kujua na unathibitishaje Mungu huyo yupo?

Na si mawazo yako tu yasiyo na uthibitisho wala uhalisia wowote ule?
Hujathibitisha Mungu yupo, ila unadai yupo!

Huoni kwamba unafosi mawazo yako yasiyo na uhalisia wowote ule?
 
Haijalishi wangapi wanapinga uwepo wa Mungu, bado yeye ni Muweza wa yote na ni Mungu wa wote.
Pia haijalishi ni wangapi wanaamini uwepo wa huyo Mungu, Bado Mungu huyo hayupo na wala hajawahi kuwepo kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo.

Mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea huyo Mungu kwa vile Hayupo, hajawahi kuwepo na hatawahi kuwepo kujiongelea, kujidhihirisha na kujitetea mwenyewe.
 
🤔🤔🤔🤔🤔
 
Safi kabisa, Dunia inazunguka jua Kwa kasi ya karibu km 1000 Kwa saa ! Ni maajabu hayo MUNGU YUPO
 
Mi nachoweza tu kusema ni kua kwa tulipofikia, binadamu hana limit tena ya ufikiriaji. Ni eidha tu labda kitokee kitu ambacho hakijawai kuonekana kabisa ndo watu wanaweza shindwa kukielewa ila baada ya muda kitachunguzwa na majibu yatapatikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…