Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Uyo Mungu, yupo kwenye imagination zetu tu, lakin hayupo... Na kama mnasema yupo, ni Mungu gani uyo ambae yupo, Mungu wa waislam, yaweh, Zeus Mungu wa wagiriki au Warumbe na mkisi Mungu wa Waganda, au yule wa wahindu. Miungu wapo wengi Sana Dunia hii, unatuaminishaje kwamba wako ndo sahihi?
 
Safi kabisa, Dunia inazunguka jua Kwa kasi ya karibu km 1000 Kwa saa ! Ni maajabu hayo MUNGU YUPO
Hii inaitwa Logical non sequitur.

Unaunganisha vitu viwili tofauti visivyo na uhusiano wowote ule kuunda hitimisho potofu.

Hujathibitisha Mungu huyo yupo, Unarukia kusema kuzunguka kwa Jua ni maajabu ya Mungu.

Huyo Mungu ni nini? Thibitisha kwanza uwepo wake.

Jua lipo na linathibitishika lipo.
 
Sawa mkuu
 
Kama Mungu angekuwepo, kusengukuwepo Shetani, Mungu muweza wa yote na mjuvi wa vyote alimuumba vipi Shetani? Utagundua concept ya Shetani ilikopiwa na wakristo kutoka katika dini za dualism ambapo huwa Kuna miungu wawili, mmoja wa wema mwingine wa mabaya... Hii ilifanyika baada ya watu kuwa wanjiulza kama Mungu yupo kwanini Kuna mema na mabaya, ndo ukristo ukaanzisha iyo concept ya Shetani baadae, na ndo maana kwenye agano la kale hakuna sehemu Shetani ametajwa, alikuja kutajwa kwenye agano jipya kwenye biblia
 
Uwepo wa vita, magonjwa umaskini vinathibitisha kuwa uyo Mungu muwezo wa yote na mwenye upendo hayupo, kama aliweza kuumba ulimwengu kwa kutamka... Anashindwa nn kutamka na vta, magonjwa na umaskini vikaisha
Hawa watu waamini Mungu ukiwauliza maswali kama haya wanajifanya kama vile hawayaoni.

Wanapita na ku view Kimya Kimya.
 
Mi nachoweza tu kusema ni kua kwa tulipofikia, binadamu hana limit tena ya ufikiriaji. Ni eidha tu labda kitokee kitu ambacho hakijawai kuonekana kabisa ndo watu wanaweza shindwa kukielewa ila baada ya muda kitachunguzwa na majibu yatapatikana.
vitu ni vingi mno ambavyo sio vipya ni vya zamani na havielezeki kisayansi

miaka na miaka watakwambia "this is a subject of ongoing research"

mfano kitu cha kawaida tu kwa maelfu ya miaka wanajiuliza namna ya kuzuia binadamu asizeeke

lakini bado akili hijafikia hapo

labda kuna kuna kipindi watafanikiwa

ila ni vitu vingi ambavyo sio vipya na vinakosa majibu ya kisayansi kwa miaka na miaka
 
Kuna Mungu wa aina mbili kwa watu wanaoamini dini, Mungu wa kwanza, uyu ni yule ambae haonekani, huwez kumskia Wala kumshika, na watu wa dini wanakuwa wanjanja baada ya hapo, Wana Mungu wa aina ya pili, uyu tunamjua vizuri sana kupita maelezo, Ni Mungu mwenye hasira, tunajua anapenda tufanye nn na tusifanye nn, tuvae nn na tule nn na tusinywe nn. Sasa jiulize ni Mungu gani mnaesema yupo? Huyu ambae hatumjui? Au yule ambae tunajua kila ktu kuhusu yy. Mwisho wa siku kiuhalisia Mungu hayupo na hajawah kuwepo
 
Sitaki kujidai kwamba namjua saana MUNGU, wewe unamjua MUNGU kuliko hata Mimi, lakini ninachojua nikwamba MUNGU ANATHIBITISHWA KWA MATENDO YAKE MAKUU, UKIFUNUA TU BIBLIA UNAKUTANA NA MWANZO 1:1 INasema "HAPO MWANZO MUNGU ALIZIUMBA MBINGU NA NCHI......" Mimi najua yupo.....
 
Hii hoja yako yaweza kua debated na hoja kutoka kwenye Society formation.

Mojawapo ni kwamba jamii kuundwa ilitokea makubaliano ambayo jamii inasurrender haki zao zote isipokua ya kuishi. In return authority itaoffer protection kwa jamii.

Kisha authority itatengeneza taratibu na sheria ambazo zitakua ndiyo miongozo.

Hivyo basi, watu hatuui kwa sababu authority ishaonyesha ukiua na wewe utauawa. Zikaundwa mpaka mahakama kufanya huu uamuzi.

Hivyo kabla kabisa binadamu hajaletewa dini alikua na authority.
 
Uwepo wa vita, magonjwa umaskini vinathibitisha kuwa uyo Mungu muwezo wa yote na mwenye upendo hayupo, kama aliweza kuumba ulimwengu kwa kutamka... Anashindwa nn kutamka na vta, magonjwa na umaskini vikaisha
ulitaka afanye kama unavowaza weww kwamba hivyo vitu visiwepo ndo ijue yupo,

hayo ni matarajio yako tu,
kwamba kwasababu kuna magonjwa vita na umasikini ndo hayupo ?

hivi ni vitu unavyoviona vipo vinakutisha kwasababu ndo top ya vitu vibaya uvijuavyo

je kama kuna namna nyingine kubwa zaidi ameviepusha na ndo maana tupo humu kila siku kwa ma milioni ya miaka ?

hivyo vitu vimewai kuimaliza dunia ikaisha

ndo maana kwenye bandiko ni kua akili ya binadamu inategemea sana experience vitu ulivyoona na kusikia

umesikia njaa, mafuriko vita magonjwa, umeona ndo vikubwa kuliko vyote

hatuna experience na vikubwa ambavyo vikitokea labda tunaisha wote

ndo maana unasema kwanini magonjwa yapo.

swali: magonjwa yapo na hivyo vitu vyote tangu zamani lakini mbona tuna survive, na dunia imekwepo kwa miaka mingi sana ?
 
Kusurvive kwetu hakuhusiani na Mungu, kwenye magonjwa sayansi ya tiba ndo imesaidia kudhibiti magonjwa na sio Mungu. Na ndio maana hata ww ukiugua huendi kanisan Wala msikitini, utaenda hospital kutibiwa..
 
Hujui Mungu yupo bali una amini tu yupo kwa vile umekuta na umeaminishwa Mungu yupo.

Ungekuwa unajua Mungu yupo ungeweza kumthibitisha yupo na wala usinge hitaji imani ya kujua kwamba Mungu yupo.

Biblia kusema Mungu yupo ni hadithi za kutungwa sawa na hadithi za uwepo wa Dragons 🐉 watemao moto midomoni mwao ambapo kiuhalisia sio kweli.
 
Imagination ndo sifa kubwa iliyoweza kututofautisha na viumbe wengne, na kutufanya tuitawale Dunia, na tuwe na uwezo wa kuingamiza pia. Mwanadamu pekee kati ya wanyama wote duniani ndio anaweza kuwa na Imagination kali.. mwanadamu anaweza kutengeneza story ambayo sio ya kweli na akaiamini... Hii imesaidia kutufanya tuwe wamoja.. lakini kiuhalisia, hakuna Mungu huko juu Wala hakuna shetani, ni imagination zetu tu. That's why hutaweza kuthibitisha hata siku Moja sababu Mungu, Shetani, malaika, wachawi hawapo.
 
N
 
Kusurvive kwetu hakuhusiani na Mungu, kwenye magonjwa sayansi ya tiba ndo imesaidia kudhibiti magonjwa na sio Mungu. Na ndio maana hata ww ukiugua huendi kanisan Wala msikitini, utaenda hospital kutibiwa..
usitoe mifano ya magonjwa, ni minor sana na Mungu ametupa uwezo wa kuyashughulikia,

ongelea mambo ambayo binadamu hajawai ku experience na hawezi kuyashughulikia

mimi nakuoa mfano ukaufatilie mwenyewe

mwaka 2019 kuna asteroid ilikua inakaribia kabisa kui gonga Dunia, na inge gongana na dunua, dunia ingepasuliwa haswa iwe nyang'any'anya, iwe rojorojo

astonoers wa hapa duniani ambao unaamini research zao na kuona wamekua advanced na wanajua vingi

wali detect hatari ya kugongana siku chache kabla na pia hawakua na namna ya kuzuia

waki calculate speed yake na position ya Dunia ikaonekana inagongana na Dunia July 25 2019

ila siku chache baadae haikuendelea na hiyo direction ila ilipishana na dunia kwa kilometers chache sana

ikawa imepita

hiyo ni moja wapo ambayo tutasema pia tume experience hatari yake,
wew unaongelea, njaa, vita magonjwa kwamba yapo kwasababu Mungu hayupo ?

kuna vitu vingine vya hatari kuliko hata Collision pia probably vinaepushwa ni kwamba tuu hatujui
 
Sure kaka, Mungu yupo.
Sometimes ukifikiria sana at the end unafika point unakubali yupo aliyeumba huu ulimwengu.
Kuna wakati huwa na imagine tupo na zaidi ya mabilioni ya sayari lakini mwamba akachagua Earth for humans, huwezi sema tu eti from no where binadam tu tukawa kwenye hii sayari.
 
Sasa iyo asteroid kutokugonga Dunia kunathibitsha vipi uwepo wa Mungu, maana kama Mungu angekuwepo hata izo asteroids za hatari asingeziumba, afu baadae aje azikwepeshe tena...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…