Uzi maalum kwa wale wanaopinga uwepo wa Mungu

Mbona hueleweki ?

Na nkuulize swali kama binadamu hana ukomo wa fikra na huwa siku zote anaendelea kupunguza asivyovijua,
kwanini wewe usiendelee kusubiri siku ambayo utakua umepata jibu kuhusu uwepo wa Mungu ?

Maana hauna majibu kamili lakini umehitimisha kuwa hakuna Mungu
 
Huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Haonekani, Hashikiki, Hasikiki, Haisiki wala hapimiki.

Hata ukijaribu kufanya utafiti, uchunguzi na udadisi wa kuwepo huyo Mungu haiwezekani.

Ninyi mmehitimisha kusema Mungu yupo ilihali hata hamuwezi kuthibitisha kwamba yupo.

Huoni kwamba hayupo?

Huoni kwamba unafosi mawazo yako yasiyo na uthibitisho wowote ule?

Ukisema kitu kipo kithibitishe kipo, Kama huwezi kuthibitisha kipo ni kwamba hakipo.
 
Mbona mimi nlishajithibitishia kitambo sana, Kuhusu hilo wala sina wasi wasi
 
Mbona mimi nlishajithibitishia kitambo sana, Kuhusu hilo wala sina wasi wasi
Tutajuaje na kuhakikishaje unayosema ni kweli?

Maana uthibitisho sio suala la kuamini ni suala la kuhakiki.

Kuamini tu, unaweza kuamini hata uongo.

Sasa uthibitisho una angalia na kuichambua hiyo imani, Je unachoamini ni kweli au uongo?
 
Tutajuaje na kuhakikishaje unayosema ni kweli?

Maana uthibitisho sio suala la kuamini ni suala la kuhakiki.

Kuamini tu, unaweza kuamini hata uongo.

Sasa uthibitisho una angalia na kuichambua hiyo imani, Je unachoamini ni kweli au uongo?
Nnachoamini ni ukweli kwasababu nmejithibitishia,

Mbona neno uthibitisho nmeandika chief, Hauelewi ?

Imani yangu kuhusu Mungu haina shaka yoyote ile kwakua nimejithibitishia kwa 100%
 
Nnachoamini ni ukweli kwasababu nmejithibitishia,

Mbona neno uthibitisho nmeandika chief, Hauelewi ?

Imani yangu kuhusu Mungu haina shaka yoyote ile kwakua nimejithibitishia kwa 100%
Hii ni logical fallacy

Hapa tu tayari usha changanya vitu viwili tofauti visivyo na uhusiano wowote ule na kuunda hitimisho potofu.

Huwezi kuwa na uthibitisho kitu kipo, halafu hapohapo uwe na imani kwamba kitu hicho kipo.

Otherwise, unaanza kuchanganyikiwa kiakili.

Ni sawa na useme una imani mwanzilishi wa JF ni Maxence Melo wakati hapohapo unajua fika na una uthibitisho kwamba Jamii forums ilianzishwa na Maxence Melo.
 
Basi ngoja nkurekebishie kauli, NAJUA Mungu yupo.
 
We ndo unachanganyikiwa mzee, nakuhukakishia ww ungezaliwa India bila shaka ungekuwa mhindu na unampigania mungu Krishna na kumtetea
 
wale wanaopingaga uwepo wa Mungu walikuja hapa wengine wakakimbia na wengine wakafuta comments,
 


DNA ina uwezo mkubwa wa kuhifadhi data ambao binadamu bado hajui namna ya kuufikia,

inaweza kuhifadi movie zote duniani lilizoachiwa ndani ya miaka 100 iliyopita ado ikawa haijatumika hata 1% ya uwezo wake wa kuhifadhi data
 


DNA ni zaidi ya Lugha

mfano unaposema lugha ya compute Python, Java, C++, C, JavaScript etc

Zaidi ya pair bilioni 3 kwenye DNA zimepangwa katika namna inayotoa taarifa ya kueleweka kumuhusu kiumbe huyo: awe na sifa zipi mfano

Jinsia, Rangi, Tabia, group la damu, urefu etc...... mambo yote kum husu kiumbe

ukikuta ku kitabu kimeandikwa lazima utajua hakijajiandika chenyewe, DNA ni zaidi ya kitabu, zaidi ya programming language yoyote duniani, ilikuaje ikajiandika ?
 


DNA imetengenezwa kwa protein, Lakini pia DNA ndo inayotengeneza protein,

Theory ya evolution inasema kitu kinatoka kwenye more simple version kina evolve kua more comlex

lakini protein isingepatikana bila DNA kiwepo na D A isingepatikana bila protein kuwepo Lazima vitu vyote viwepo kwa pamoja ndo huo mzunguko uendelee

Je ilitokeaje vyote kuwepo kwa pamoja kibahati mbaya ?

inakuaje unakuta ufunguo wa solix na kufuli ya solix ambayo inafunguliwa na huo ufunguo kwa bahati mbaya ?
 


kila seli ina DNA, seli huwa ina jigawa ( zina zaliana ili kuongezea maana zingine hufa )

kila seli inapo jigawa seli inayozaliwa inatakiwa pia kuwa na DNA yenye code zile zile

DNA Ina mfumo maalum wa kuhakikisha seli mya ina DNA ambayo ipo sawasawa isiyo na makosa,

inafanya error checking kuhakikisha DNA ipo sawa na haina taarifa zitakazoleta madhara na mabadiliko katika mwili.
 


Lugha ya DNA ni moja kwa viumbe vyote

DNA inatumia mfumo wa A, T, C, G

viumbe vyote kuanzia binadamu na wanyama wengine hadi mimea

mfumo unaotumiwa kuhifadhi taarifa zao, au luga inayotumiwa kuhifadhi taarifa zao ni moja,

hii inaonyesha viumbe vyote vimekuwa designed na nguvu moja haiwezekani kua vyote vimekuja ki bahati mbaya na vikajikita vimefanana,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…