Uzi Maalum wa kumtaka mgombea Urais CCM kufanya mdahalo

Uzi Maalum wa kumtaka mgombea Urais CCM kufanya mdahalo

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Kichwa cha habari chahusika.

Hii ni mada maalumu ya kumtaka mgombea wetu wa CCM kufanya mdahalo na wagombea wenzie ili kupima uzito wa sera zao.

Hii itatupa fursa ya kuuliza maswali magumu na mepesi kuhusu sera zao. Katika mikutano ya hadhara hakuna fursa ya kuhoji.

Hili sio ombi ni lazima. Tunataka kuhoji mambo ya msingi ya nchi. Ikumbukwe tuliingia mkataba na rais Magufuli kupitia ilani ya CCM kwa hivyo tunataka kujua yaliyofanyika kupitia mnakasha.

Mambo ni mengi ila kwa uchache ni kuhusu:
1. Suala la ajira
2. Manunuzi ya ndege
3. Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato
4. Ulinzi na Usalama ikiwepo mauaji na utekaji
5. Uhuru wa kutoa maoni na Sheria kandamizi
6. Diplomasia na mambo ya kimataifa
7. Katiba mpya
8. Nyongeza ya mishahara
9. Uchumi wa kwenye makaratasi

Ongezeni na mengine
 
"Msichague viongozi wa upinzani, hata kama wanafaa" Jiwe, 2020.

Unatarajia mtu asiye na uwezo wa kujenga hoja, mropokaji kama huyo ndo akubali mdahalo?
Labda kama huo mdahalo uwe wake na Rungwe tu, Mheshimiwa Lissu asiwepo, maana jiwe kwa Lissu haingii hata robo kwenye hoja, ni mdogo kama piriton.
 
La Kwanza ndo angalau ni hoja, mengine ni utopolo mtupu na umbea umeandika, istoshe yeye ni raisi kampeni kwake ni kutimiza wajibu, tatizo mna vichwa vigumu sana kama vya samaki asiyekolea viungo, ndo mana mnataman fujo na vurugu c'se ndo chadema's last stand.
 
Ajitokeze kwenye mdahalo naamini anawesa kujieleza vizuru
Sioni sababu kwa nini yeye au wafuasi wake waogope?
 
Hapa
La Kwanza ndo angalau ni hoja , mengine ni utopolo mtupu na umbea umeandika ,istoshe yeye ni raisi kampeni kwake ni kutimiza wajibu ,.. tatizo mna vichwa vigumu Sana kama vya samaki asiyekolea viungo, ndo mana mnataman fujo na vurugu c'se ndo chadema's last stand
Hapana nazani hata LA 5,6 na 7 ni muhimu pia tena Sana!
Maana wapinzani wake wanachukulia sana credit huko. Labda inahitajika ufafanuzi
 
Magu hawezi kupambana na Lissu kwa hoja yoyote. Huyu jamaa udhaifu wake unafichwa tu na mavyombo ya dola yanayo mzunguka. Sina uhakika hata kama akiulizwa Historia ya ukombozi wa Tanzania kama anajua. Jamani huyu kwenye mambo ya uelewa wa mambo hawezi. Akijitokeza kwenye mdahalo na Lissu mimi nahama nchi
 
Huyo hana uwezo wa kufanya Mdahalo wala kuojiwa na TV..Hana uwezo huo.Miaka yote ya urais wake umeona ameweza kuhojiwa na TV yoyote? Uwezo wake ni kukaa kwenye mkutano ambao yeye ndo msemaji mkuu au msikilizaji mkuu.Hana uwezo huo.
 
Kichwa cha habari chahusika.

Hii ni mada maalumu ya kumtaka mgombea wetu wa CCM kufanya mdahalo na wagombea wenzie ili kupima uzito wa sera zao.

Hii itatupa fursa ya kuuliza maswali magumu na mepesi kuhusu sera zao. Katika mikutano ya hadhara hakuna fursa ya kuhoji.

Hili sio ombi ni lazima. Tunataka kuhoji mambo ya msingi ya nchi. Ikumbukwe tuliingia mkataba na rais Magufuli kupitia ilani ya CCM kwa hivyo tunataka kujua yaliyofanyika kupitia mnakasha.

Mambo ni mengi ila kwa uchache ni kuhusu:
1. Suala la ajira
2. Manunuzi ya ndege
3. Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato
4. Ulinzi na Usalama ikiwepo mauaji na utekaji
5. Uhuru wa kutoa maoni na Sheria kandamizi
6. Diplomasia na mambo ya kimataifa
7. Katiba mpya

Ongezeni na mengine
Mdahalo Kama utakuwa kwa lugha ya MALKIA itapendeza
 
Magufuli hawezi kukubali mdahalo, mtaamini ninachokisema kwani anaelewa fika kuwa utambomoa vibaya mno na kumpaisha Lissu.

Mnaona safari hii hata wale Pollsters amewatisha hadi wametokomea kusikojulikana, uchwara ni noma.
 
Ulichosema juu ya kua midahalo au mahojiano maalum kwa wagombea wetu wa Uraisi hilo 100% niko nawe maana pia inatupa uwezo wa kufahamu uelewa binafsi wa mgombea na hilo ni muhimu kwetu kwa uamuzi wa viongozi wetu tunaowataka. Kwenye hayo maswali ndio yana msingi mkubwa ila nadhan unatamani hichi kipindi kifanane na msimamo wako, sina upande wowote kwa vyama, naamini ktk maslah ya wengi kuna mfumo utawekwa ili kupata maoni ya wengi ktk kipindi husika.
 
Wafanye mdahalo wa lugha wanayoitumia kututungia masheria na kuwafanyia interview tunapoomba ajira.
Vinginevyo hiyo lugha ifutwe ibaki kiswahili.
Madaktari hospitalini watuandikie kwa Kiswahili tuu.
 
Back
Top Bottom