Katashekadm
JF-Expert Member
- Feb 14, 2018
- 728
- 775
Yaani Rais afanye mdahalo na mgombea!Kichwa cha habari chahusika.
Hii ni mada maalumu ya kumtaka mgombea wetu wa CCM kufanya mdahalo na wagombea wenzie ili kupima uzito wa sera zao.
Hii itatupa fursa ya kuuliza maswali magumu na mepesi kuhusu sera zao. Katika mikutano ya hadhara hakuna fursa ya kuhoji.
Hili sio ombi ni lazima. Tunataka kuhoji mambo ya msingi ya nchi. Ikumbukwe tuliingia mkataba na rais Magufuli kupitia ilani ya CCM kwa hivyo tunataka kujua yaliyofanyika kupitia mnakasha.
Mambo ni mengi ila kwa uchache ni kuhusu:
1. Suala la ajira
2. Manunuzi ya ndege
3. Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato
4. Ulinzi na Usalama ikiwepo mauaji na utekaji
5. Uhuru wa kutoa maoni na Sheria kandamizi
6. Diplomasia na mambo ya kimataifa
7. Katiba mpya
8. Nyongeza ya mishahara
9. Uchumi wa kwenye makaratasi
Ongezeni na mengine
Siyo kila wakati unajitoa ufahamu!