Hoja yako inakoelekea ukifuatiliwa utakwama. Atakuja mtu hapa atakuuliza wewe unayeamini katika Mungu uliwahi kumuona?
Mijadala hii ya kiimani ni mizito ndiyo maana haina mshindi na mara nyingi huishia katika ugomvi na kutukanana tu. Tafuta threads hapa zinazojadili uwepo wa Mungu uone ninachokiongelea.
Binafsi huwa nakwepa mijadala ya aina hiyo kwa sababu haisaidii cho chote katika kuimarisha imani yangu. Egyptology leo hii ni uwanja mpana na unaojitegemea na watu wanasoma haya mambo kwa kina. Usifanye majumuisho ya kiujumla katika mijadala ya aina hii kwa sababu ukibanwa hutaweza kujitetea mbali na kutoa povu na kusema kuwa ndivyo unavyoamini.
Na kwa nini tusile likes tu hapa na kuyaacha haya mambo? Hamieni jukwaa la dini huko kuna mijadala mizito kuhusu mambo haya...