Kupungukiwa maji mwilini
Katika sura hii:
Maumivu tumboni, kuhara, na minyoo
Maumivu tumboni au kwenye utumbo
Kupungukiwa maji mwilini
Kutapika
Kuhara
Minyoo
Matatizo mengine ya tumboni
Muwasho au maumivu kwenye njia ya haja kubwa
Matatizo mengi ya tumbo yanaweza kuepukika
Madawa
Kupungukiwa na maji mwilini humaanisha kuwa hakuna maji ya kutosha mwilini. Tatizo hili linaelezewa kwenye sura hii kwa sababu chanzo chake kikuu ni kuharisha. Kupungukiwa na maji mwilini kunaweza kutokana pia na kutapika, mwili kupata sana joto kutokana na jua kali, kufanya kazi kubwa kupita kiasi, au kuvaa nguo nyingi nzito. Hasa kwa watoto wadogo, tatizo la kupungukiwa na maji mwilini linaweza kuongezeka haraka na kuweza kusababisha mauti.
Bila kuzingatia kisababishi, tiba ambayo mtu yoyote anaweza kutoa nyumbani kwa mtu mwenye dalili za kupungukiwa na maji mwilini ni kumuongezea maji mwilini kwa kumpatia vinywaji kwa wingi. Kwa njia hii unaweza kuponya maisha yake.