Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maji ya mchele
Maji ya mchele hufanya kazi vizuri sawa na mchanganyiko wa chumvi na sukari katika kuurudishia mwili maji. Pika mchele kwenye maji mara mbili ambayo ungetumia katika hali ya kawaida. Ongeza chumvi kidogo kwenye maji. (Takriban ½ kijiko cha chai cha chumvi kwa kila lita ya maji.) Unaweza kuongeza sukari kidogo kama utataka. Kunywa kiasi kadri uwezavyo. Unaweza pia kula wali uliopo kwenye machangayiko huo.
 
Nafaka zingine za nyumbani
Kama huwa unatengeneza uji au chakula kingine aina ya ujuuji kwa ajili ya matumizi yako au ya watoto wadogo, chakula aina hiki kinaweza kuongezwa maji ili kiweze kutumika kumuongezea mtu maji mwilini. Unga wa mahindi, viazi au mhogo vyote vinaweza kusaidia kumuongezea mtu maji mwilini(kama vitapikwa vizuri, kupondwapondwa, kuongezwa maji mengi na pia kutiwa chumvi kidogo).

Uji mwepesi kama huo hauwezi kufidia hitaji la chakula. Kama uji utafanywa mwepesi na kutumika kama kinywaji cha kuongeza maji mwilini, pia uji mzito uandaliwe kwa ajili ya kula kama kawaida. Ili kupona haraka kutokana na upungufu wa maji mwilini, mpatie mgonjwa chakula sambamba na vinywaji.
 
Mtindi au maziwa mengine yaliyochachushwa
Hivi ni vinywaji vizuri kwa ajili ya kuurudishia mwili maji na pia hutoa protini. Kama mtindi utakuwa mzito sana, changanya na maji kidogo. Pia ongeza chumvi kidogo kwenye kila glasi.

Maziwa ya mama

Kama unanyonyesha mtoto anayeharisha, endelea kufanya hivyo. Mnyonyeshe mtoto mara nyingi zaidi – angalau kila baada ya kuharisha. Mruhusu anyonye kadri atakavyotaka. Mtoto mwenye dalili za upungufu wa maji mwilini anapaswa kupewa kinywaji mchanganyiko wa chumvi na sukari kila anapomaliza kunyonya.
 
Epuka vinywaji ambavyo huzidisha upungufu wa maji mwilini
Hapana!
Vinywaji vilivyokolezwa sukari,vinywaji vyenye kemikali ya kafini (caffeine), na pombe huzidisha tatizo la upungufu wa maji mwilini. Hivyo epuka:

Soda (Coke, Fanta, Pepsi) na vinywaji vingine vilivyokolezwa sukari.
Kahawa na chai iliyokolea sana.
Biya, mvinyo na pombe zingine.
 
Vipi kuhusu maji ya kawaida ambayo hayajachanganywa na chochote?
Unapokuwa umepungukiwa na maji mwilini,maji ya kawaida ambayo hayajachanganywa na chochote siyo bora kama vinywaji maalum kwa ajili ya kuuongezea mwili maji kwa sababu hayana virutubishi ambavyo mwili wako unahitaji. Unapokuwa umepungukiwa maji mwilini, kunywa maji ya kawaida kunaweza kusababisha uugue kwa sababu unahitaji pia chumvi na nishati. Lakini ni bora kumpa mgonjwa maji ya kawaida ambayo hayajachanganywa na chochote kuliko kutompa kinywaji chochote-angalau kwa muda
 
Lazima maji yachemshwe kwanza?
Maji ambayo yamechemshwa au kutibiwa kuua vijidudu ni bora zaidi. Kwa taarifa zaidi juu ya jinsi ya kuyafanya maji kuwa salama zaidi kwa ajili ya kunywa, bonyeza hapa.

Lakini kama huna kuni kwa ajili ya kuchemsha maji, au kupata maji safi ni shida, tumia maji uliyonayo hadi utakapoweza kuboresha usalama wa maji yako.
 
Paketi ya chumvichumvi kwa ajili ya kuongeza maji mwilini

Paketi za chumvichumvi kwa ajili ya kuongeza maji mwilini zinaweza kupatikana kwenye duka la dawa, kiliniki, au sokoni. Kama vilivyo vinywaji vya kuurudishia maji mwili ambavyo hutengenezewa nyumbani, paketi hizi zina mchanganyiko wa chumvi na sukari kwa kiasi kinachostahili kutibu upungufu wa maji mwilini. Pia ndani kuna madini ya potasiamu, saitreti, na zinki-virutubishi ambayo husaidia sana watu wanaoharisha. Mahali ambapo bidhaa hii inaweza kupatikana, hutoa njia rahisi ya kutengeneza kinywaji cha kuurudishia mwili maji. Kumbuka kuongeza kiasi sahihi cha maji – kawaida lita 1 ya maji kwa kila paketi. (Lakini soma maelekezo kwenye paketi kwa sababu kuchanganya na maji kidogo sana au maji mengi sana kunaweza kusababisha ugonjwa kuzidi.)
 
Kama paketi za chumvichumvi hizi (ORS) hazipatikani kwa urahisi, ni bora zaidi kutengeneza kinywaji chako mwenyewe cha kuurudishia mwili mali – gharama yake ni nafuu zaidi. Tumia fedha zako kwa kununua mboga mboga, maharagwe, mayai, au vyakula vingine vinavyofaa kiafya. Kinywaji chako ulichotengeneza nyumbani kinalingana katika ubora na paketi iliyotengenezewa kiwandani, na chakula chenye virutubishi kitakusaidia kupona haraka.
 
6e346052f929802bcfac41a6ed5c3584.jpg
Kanye
 
Back
Top Bottom