Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuna baadhi ya watu wanaamini wanaotakiwa kutunza ngozi ni wanawake tu ila sio kweli kwasababu hata mwanaume mtanashati lazima aitunze ngozi yake ili kuonyesha umaridadi wake na unadhifu wake. Ngozi isiyo na matunzo mazuri huondoa mvuto wa mtu kwa sababu unaweza ukawa na chunusi, harara na upele au hata mikunjo ya usoni ambayo itaondoa mvuto na umahiri wako. Hivyo bas kila mtu lazima atunze ngozi yake ili kuondoa mikunjo iliyopo usoni, chunusi, harara na hata miwasho iliyo katika ngozi. Vipo vitu mbalimbali vinavyosababisha ngozi kutokuwa nzuri na ya kuvutia vitu hivyo ni pamoja na ;
 
Kutokunywa maji ya kutosha kwa siku.
Kutumia losheni zenye kemikali nyingi
Kutopata lishe bora
Hali ya hewa
Kuwa na kiwango kikubwa cha homoni mbalimbali mwilini
Kurithi
Ujauzito
Matumizi ya vidonge vya kuzuia mimba
Msongo wa mawazo uliokithiri
 
Nawa uso wako kwa maji ya vuguvugu na sabuni , hii husaidia kuondoa uchafu uliopo kwenye ngozi yako na mafuta yaliyopo kwenye ngozi yako. Ili ngozi iwe safi hakikisa unaisafisha kila siku na ukiweza kutwa hata mara mbili ili isikae na uchafu, safisha asubuhi na jioni kila siku. Na kwa sabuni tumia sabuni za asili kama za sabuni ya liwa, ukwaju, limao kwa sababu hazina kemikali.
 
Kwa watu wenye ngozi zenye asili ya mafuta tumia maji ya malimao kupaka usoni mpaka shingoni lakini akikisha yasiingie machoni na kaa nayo kwa dakika tano kisha osha. Limao linasaidia kuondoa mafuta yaliyopo kwenye ngozi yako na pia kuondoa madoa yaliyoko kwenye ngozi yako. Kwa wasio na mafuta usoni unaweza ukatumia tango kwa ajili ya kusafishia. Unatumia juisi ya matango na unaipaka usoni na kukaa nayo dakika tano tuu na baada ya hapo unasafisha kwa maji safi ya uvuguvugu ili kuondoa maji ya limao na matango.
 
Back
Top Bottom