Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hakuna sababu ya kuona haya kumwambia daktari wa meno kuhusu harufu mbaya kinywani inayokusumbua, kwa vile kumwambia na kujadili tatizo lako ni njia ya kuelekea kwenye tiba ya uhakika. Matumizi ya nyuzi-safishi kila siku, kusafisha meno na ulimi kwa mswaki walau mara mbili kwa siku yaweza kuondoa harufu mbaya kinywani kwa kiasi kikubwa.
 
6- Chakula bora ni muhimu kwa afya bora ya kinywa na meno

Ulaji wa vyakula na vinywaji vyenye sukari na visivyo na virutubisho vya mwili vinapochanganyikana na vimelea vya magonjwa (bakteria) hutengeneza tindikali ambayo hushambulia ukuta wa nje wa jino. Kushambuliwa kwa enameli na tindikali husababisha mashimo kwenye meno na magonjwa ya fizi.
 
7- Bila matibabu, magonjwa ya kinywa na meno hayaponi wala kupata nafuu

Pale daktari wako wa meno anapokupa mpango mkakati wa matibabu ya kinywa na meno yako, jukumu lako ni kuzingatia maagizo na maelekezo ya daktari ili upate matokeo mazuri. Inapotokea una mashimo makubwa kwenye meno, bado inawezekana kutibu meno kuanzia kwenye mzizi kabla meno hayajang'olewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…