Asee safi sana. Nilijihisi nipo jangwani ( Kalahari ?) na tena milimani na nchi ya kichawi Ukukuana, niliposoma kitabu "King Solomon mines"Mambo hayo ni kama kujihisi kama ametua kwenye mwezi anaposoma habari za mwanaanga aliyekwenda mwezini, kujihisi kama anasafiri jangwani akiwa juu ya mgongo wa ngamia au kujihisi kama yuko kwenye kisiwa fulani katika bahari pana ya Hindi.
SahihiVile vile vitabu vinaweza kumrudisha mtu miaka mingi nyuma akajihisi akiwa kwenye ngome ya Chifu Mkwawa anaposoma habari za mtawala huyo maarufu wa zamani wa Wahehe.
Huwa nawaonea huruma wasiopenda kusoma vitabuJambo la kufurahisha zaidi ni kuwa katika ulimwengu wa maandishi kuna kitabu, jarida au mtandao kwa kila jambo ambalo mtu anaweza kutarajia kusoma habari zake. Hata hivyo, faida hii haipatikani kwa mtu ambaye uwezo wake wa kusoma ni mdogo na wala hana ari ya kusoma.
[emoji106] [emoji106] [emoji106]3.Kusoma hukufanya uwe mtu bora
Kwa hakika kusoma kunaweza kukufanya uwe mtu bora hata kuliko ulivyowahi kuwaza au kufikiria. Kusoma hukuongeza haiba yako kwa kukufanya uwe mtambuzi wa mambo mbalimbali, mchangamfu, mjanja kimaisha, mtu unayependeza na mwenye mvuto kwa watu.