lakini kama mwenye nyumba akaweka pazia na kuondoa kabisa ushawishi wa baadhi ya watu kupenda kuchungulia bila shaka tabia hii itapigwa marufuku. Ingawa kitendo hiki ni cha aibu wakati mwingine mtuhumiwa wa upigaji chabo amekuwa akishawishiwa na muathirika kutokana na ushawishi anaokutana nao kutoka kwa mwathirika.
Kila mpangaji atakayepika chakula ni lazima ampakulie na kumpelekea kwenye sahani yake. kwa mfano mpo wapangaji nne basi wote wanne wapeleke sahani za ugali na mboga kwake..
Kila mpangaji akipata mgeni lazima amtaarifu muda aliofika na atako ondoka.
Kutokana na masharti hayo wapangaji wengi wamelazimika kuimbia nyumba hiyo huku wengine wakiacha kodi ya miezi hadi saba kwani ukishapanga kwake pesa hairudishwi.
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu amesisitiza kuwa madalali wengi wa vyumba wamekuwa wakii tumia nyumba hiyo kujipatia fedha kwani muda wote vyumba vipo kwa kuwa waweza panga leo kesho uka amua kuondoka kutokana na masharti magumu ya Bibi huyo.
Hata hivyo kutokana na masharti magumu ya nyumba hiyo majirani karibu na eneo ilipo wana ikwepa kama ukoma huku wale wanao toka maeneo mengine wakiu vaa mkenge na baadae kujuta kuifahamu.
Mwananchi unashauriwa kuwa makini ukitaka kupanga nyumba sehemu usiyo ifahamu au ni mgeni kabisa jaribu kwanza kufanya uchunguzi mdogo ili uweze kujua nyumba hiyo ina matatizo gani kabla ya kuhamia kwa kuwa wapo wenye moyo wa huruma wata kuambia ukweli ukaokufanya uchukue maamuzi sahihi.