Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usidanganyike kwamba kuna kitu kimoja ukifata ndio utafanikiwa kwenye maisha, njia ya mafanikio ina vikwazo na changamoto nyingi. Usirudishwe nyuma na changamoto hizi kwa sababu ya mambo uliyofundishwa shuleni kwamba jibu sahihi ni moja tu.
 
4. Maana ya mafanikio.
Kila mtu kwenye maisha anataka kupata mafanikio makubwa, ila ni wachache sana ambao wanajua maana halisi ya mafanikio. Shuleni ulifundishwa kwamba kufanikiwa na kupita kiwango fulani cha maksi au hata kuwapita wengine darasani kwa ufaulu wa maksi.
 
Kwa bahati mbaya sana kwenye maisha mafanikio hayapimwi hivyo. Ukiangalia mafanikio kwa kutaka kuwashinda wengine au kuwa sawa na wengine utaishi maisha yako yote kukimbiza upepo. Maana ukijitahidi ukanunua gari kuna mtu utamkuta ana magari mengi zaidi yako, ukasema mafanikio ni kujenga nyumba kwa sababu kila mtu ana nyumba utakutana na mtu mwenye nyumba kubwa, nzuri na nyingi kuliko ya kwako. Kwa akili hii utaumia kichwa na kuona maisha yako hayana maana.
 
Kama unafikiri mwenzi wako ndio atakupa furaha basi kuna siku utaumizwa sana, kama unafikiri fedha nyingi ndio zitakupa furaha uko kwenye tatizo kubwa. Furaha ipo ndani yako na utaipata kutokana na maisha unayoishi na mambo unayoyafanya kwako na kwa watu wengine.
 
6. Kufaulu darasani hakumaanishi kufaulu kwenye maisha.
Mazingira ya darasani yanatabirika, kaa darasani, soma kwa bidii, jiandae na mtihani na utafaulu. Mazingira ya kwenye maisha hayatabiriki hata chembe, unaweza kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na bado yakatokea mambo yakakurudisha nyuma.
 
Back
Top Bottom