Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3. Siku yako ilikuaje?: Muulize masuala ambayo mpenzi wako anakutana nayo katika shughuli za kila siku. Muulize kuhusu huyo mfanyakazi mwenzie anayemkera au kazi kubwa waliyokuwa wakifanya. Kumpa nafasi mpenzi wako kushare sehemu zingine za maisha yake kutasaidia kuunganisha dots kati ya muda mnaokuwa pamoja.
 
4. Unga mkono maamuzi mazuri ya mpenzi wako: Mpe moyo mpenzi wako kwa kumjulisha kuwa unaunga mkono maamuzi yake. Unaweza ukaenda mbali zaidi kwa kujaribu kumsaidia afanikishe malengo aliyojiwekea. Maisha yamejaa vikwazo vingi, na ile hisia kuwa una mtu mwingineupande wako zinaweza kukusaidia kuvivuka. Msiwe couple tu, kuweni timu. Kumkumbusha mpenzi wako kuwa upo nyuma yake kutaimarisha uhusiano wenu.
 
5. Mwambie mpenzi wako kuwa Umependeza: Kama umekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, ni rahisi kujisahau katika mengi. Ni muhimu kumkumbusha mpenzi wako kuwa anakuvutia. Kumjulisha kuwa ‘gauni hilo limekupendeza sana’ kutamfanya ajisikie vizuri na kukumbusha kwanini ulimchagua yeye.
 
6. Samahani ni neno zuri kwa mpenzi wako: Kila mtu hukosea wakati fulani. Wakati mwingine hujikuta tukiongea maneno kwa hasira na baadaye kugundua kuwa hatukuwa sahihi. Ubishi hauna nafasi kwenye uhusiano wenye furaha, hivyo omba msamaha unapofanya kosa. Omba msamaha kwa kukasirika. Omba msamaha kwa kuumiza hisia za mpenzi wako. Omba msamaha hata kwa vitu ambavyo sio kosa lako.
 
9. NakuheshimuKama ulivyo uhusiano wa marafiki, heshima ni kitu muhimu kwako na mpenzi wako. Mpe nafasi ya kukushauri au kukupa mawazo kwenye mambo yanayokutatiza. Mtu anapohisi anaheshimiwa, hujisikia pia furaha na salama, vitu ambavyo ni muhimu kwenye uhusiano wowote mzuri.
 
kumheshimu mpenzi wako ni kumjulisha pale usipokubaliana naye. Hakuna mtu anapenda kuoa mtu anayekubaliana na kila kitu na hakuna mwanamke anayetakakuzaa watoto na mwanaume asiye na msimamo. Mnaweza kuwa timu, lakini nguvu ya timu yoyote ipo kwenye mawazo na matendo ya kila mmoja.
 
Kuwa na maoni yako na yaseme kwa mtindo wa heshima. Kumpa mpenzi wakomtazamo tofauti kunaweza kumsaidia kupata suluhisho kwa tatizo ambalo hakuwa ameliwaza.11. Usiku mwemaTunaishi kwenye wakati ambapo mawasiliano ni rahisi mno. Kwa kubonyeza tu kitufe tunaweza kutuma ujumbe kuvuka bahari, hivyo hakuna kisingizio cha kushindwa kusema ‘usiku’ mwema.Haimjulishi mpenzi wako tu kuwa unataka kulala, bali pia inamjulisha kuwa unamfikiria. Hata kama hamjaongea siku nzima na hasa kama mmejibizana,
 
FAIDA ZA NYAMA YA SAMAKI

Samaki (Husausan Saladini, Tuna, Salmoni nk) wana kiasi kikubwa cha virutubisho mafuta viitwavyo Omega-3-Fatty Acids – Omega-3 fatty acids ni mafuta muhimu sana kwa afya zetu kwa ujumla. Husaidia kudhibiti na kushusha presha na kiasi cha rehemu mwilini (Cholesterol) na husaidia kupunguza uvimbe.
 
Pia husaidia sana kulinda miili yetu na kukinga seli zetu dhidi ya kemikali hatari mwilini ziitwazo “free radicals”. Kinga hii ni muhimu sana kwetu na husaidia uhai wa seli na miili yetu
Samaki wana kiasi kikubwa cha protini – Kama unahitaji protini nyingi basi kula samaki wa kutosha
 
Samaki wana kiasi kikubwa cha madini na vitamini – Kama unahitaji vitamini na madini mengi basi kula samaki wa kutosha pia. Wana vitamini/madini ya calcium (Husaidia kujenga meno na mifupa imara), phosphorus (Husaidia kujenga meno na mifupa imara), vitamin D (Husaidia Calcium kuweza kuingia mwilini na kuimarisha mifupa.
 
Upungufu wa Vitamini D hupelekea mtu kuwa na matege), vitamin B2 (Husaidia kuimarisha kinga ya mwili na nywele, ngozi, mifupa na meno), iron, zinc (Husaidia kuboresha kinga ya mwili), iodine , magnesium (Husaidia kusinyaa na kufanya kazi kwa misuli) na potassium (Husaidia utengenezaji wa protini na kujengwa kwa misuli).
 
Wataalam wa afya tunakushauri kula zaidi samaki kuliko nyama ya ng’ombe, mbuzi na kondoo. Kula samaki wa kutosha na usiache muda mrefu bila kula samaki. samaki ni nyama nyeupe, haina matatizo sana kama nyama nyekundu za ng’ombe, mbuzi na kondoo.
 
Back
Top Bottom